Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ni wazi ukomavu wa kisiasa na kidemokrasia ndani chama cha demokrasia na maendeleo chadema, miongoni mwa wanaogombea uongozi wa kitaifa, wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema taifa wanachama na mashabiki bado haijapevuka vizuri mioyoni na kwenye fikra zao.
Shari inayombatana na masharti juu ya namna gani uchaguzi huo unavyofaa kufanyika ina viashiria vya liwalo na liwe vinavyoashiria kukibomoa na kukisambaratisha kabisa chama hiki kikongongwa cha siasa nchini.
kuna wagombea uongozi na wafuasi wao ndani ya chadema wanaenda kwenye uchaguzi huo muhimu sana ngazi ya taifa wakiwa na dhamira na nia moja tu tena kwa kiapo kwamba nisipokua mwenyekiti mimi bora tukose wote, la sivyo chadema ife.
Vita vya maneno na vijembe vya kisiasa na namna wagombea uongozi wanavyovuana nguo hadharini na kutoa siri za vikao vya ndani, ni wazi chadema haina mwisho mwema kuelekea uchaguzi huo wa Jàn.21, 2025.
My friends ladies and gentlemen,
una maoni gani kwenye hili.
Chadema itavuka salama kweli?
Taharuki, mabishano na malumbano ya nini sasa miongoni mwa wagombea muhimu?🐒
Mungu Ibariki Tanzania