Ni wazi ukomavu wa kisiasa na kidemokrasia ndani chama cha demokrasia na maendeleo chadema, miongoni mwa wanaogombea uongozi wa kitaifa, wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema taifa wanachama na mashabiki bado haijapevuka vizuri mioyoni na kwenye fikra zao.
Shari inayombatana na masharti juu ya namna gani uchaguzi huo unavyofaa kufanyika ina viashiria vya liwalo na liwe vinavyoashiria kukibomoa na kukisambaratisha kabisa chama hiki kikongongwa cha siasa nchini.
kuna wagombea uongozi na wafuasi wao ndani ya chadema wanaenda kwenye uchaguzi huo muhimu sana ngazi ya taifa wakiwa na dhamira na nia moja tu tena kwa kiapo kwamba nisipokua mwenyekiti mimi bora tukose wote, la sivyo chadema ife.
Vita vya maneno na vijembe vya kisiasa na namna wagombea uongozi wanavyovuana nguo hadharini na kutoa siri za vikao vya ndani, ni wazi chadema haina mwisho mwema kuelekea uchaguzi huo wa Jàn.21, 2025.
My friends ladies and gentlemen,
una maoni gani kwenye hili.
Chadema itavuka salama kweli?
Taharuki, mabishano na malumbano ya nini sasa miongoni mwa wagombea muhimu?🐒
Mungu Ibariki Tanzania
Usipokua wa haki hakuna haja ya kuwa na chama hicho.
Kimejonasibu chenyewe kuwe ni chama cha demokrasia . Sasa tusipoiona hiyo demokrasia tunapaswa kukikataa .
CCM watu wameanza kuikataa kwa sababu kinajiita chama cha mapinduzi ili hali hatuoni mapinduzi kwenye kilimo, hatuoni mapinduzi kwenye viwanda,hatuoni mapinduzi kwenye teknolojia ,hatuoni mapinduzi kwenye uchumi ,hatuoni mapinduzi kwenye madini ,hatuoni mapinduzi kwenye mfumuko wa bei . Hatuoni mapinduzi kwenye Ajira ,Hatuoni mapinduzi kwenye elimu .Hatuoni mapinduzi kwenye kuwaondoa mafisadi madarakani .CCM imepindukia na mafisadi na sasa kimekua chama cha wahuni na mafisadi wachache na wapiga kura wao wamebaki ni machawa .
Kuna Rais mmoja alikiita Chama cha mambuzi badala ya mapinduzi . Naona kama ilikua ni Roho mtakatifu alibadilishana ulimi wake ili kutaja jina halisi linalotakiwa kuitwa kwa chama hicho kongwe kinachosubiri kujifunza Demokrasia toka chadema kama wataweka uchaguzi wa huru ,haki na uwazi .
Hakuna jambo baya kama kuvuruga kura za watu . Ni dhambi mbaya sana kwenye jamii.
Leo watu tuliokuwa tunakaa pamoja na kupiga kura na kuhesabu bila vurugu wala kusimamiwa na mabunduki hali imebadilika kwa sababu ya kuvuruga kura halali . Hata kuuana ,kutokana na kujeruhi watu wakati wa uchaguzi au kampeni n.k ni kwa sababu ya kuwaza namna ya kuvuruga zoezi la kura halali .
Kwa hiyo tuwaache Chadema wafanye jambo litakaloipa uhalali wa kuikosoa serikali ya CCM au itakayowanyima kabisa kabisa kabisa uhalali wa kuikosoa CCM.
Walivuruga uchaguzi ni wazi kuwa chama hicho kitakuwa hakina tija kabisa ya siasa za Demokrasia . Bora tuache siasa za kumi kumi za CCM watifuane na kuuana wenyewe mpaka siku akitokea Capt .Mmoja mzalendo na kuibadili nchi kuwa kama Bukina Faso. Wanasiasa hawaipendi nchi zaidi ya matumbo yao ndio maana hawako tayari sio tu kuifia nchi kama wanajeshi bali hata kupoteza madaraka yao kikatiba kupitia kura wanazozipata kama raia.Yaani nchi ya kiraia na kidemokrasia halafu kuna kakundi kadogo kana fanya mapinduzi kijanja kijanja kuompitia vyombo vya dola na kujipa uhalali wa kukaa madarakani kama serikali ya kiraia. Bora iwe jeshi lijulikane kabisa na watu waachane na siasa wachape kazi na kuijenga nchi kizalendo bila unafiki.