CHADEMA bado haijakomaa kidemokrasia, mioyo na fikra za baadhi ya wagombea uongozi wa kitaifa

ni muhimu sana kwa wagombea uongozi walau wawe na hekima na busara za kuficha nia zao ovu kabla ya uchaguzi,

vinginevyo fedheha na aibu watakazozipata baada ya uchaguzi, zitawafanya kutotamani tena kubaki chadema.

na hiyo ni kumaanisha kutokomaa na kutopevuka kisiasa na kidemokrasia 🐒
 

Usipokua wa haki hakuna haja ya kuwa na chama hicho.

Kimejonasibu chenyewe kuwe ni chama cha demokrasia . Sasa tusipoiona hiyo demokrasia tunapaswa kukikataa .

CCM watu wameanza kuikataa kwa sababu kinajiita chama cha mapinduzi ili hali hatuoni mapinduzi kwenye kilimo, hatuoni mapinduzi kwenye viwanda,hatuoni mapinduzi kwenye teknolojia ,hatuoni mapinduzi kwenye uchumi ,hatuoni mapinduzi kwenye madini ,hatuoni mapinduzi kwenye mfumuko wa bei . Hatuoni mapinduzi kwenye Ajira ,Hatuoni mapinduzi kwenye elimu .Hatuoni mapinduzi kwenye kuwaondoa mafisadi madarakani .CCM imepindukia na mafisadi na sasa kimekua chama cha wahuni na mafisadi wachache na wapiga kura wao wamebaki ni machawa .

Kuna Rais mmoja alikiita Chama cha mambuzi badala ya mapinduzi . Naona kama ilikua ni Roho mtakatifu alibadilishana ulimi wake ili kutaja jina halisi linalotakiwa kuitwa kwa chama hicho kongwe kinachosubiri kujifunza Demokrasia toka chadema kama wataweka uchaguzi wa huru ,haki na uwazi .

Hakuna jambo baya kama kuvuruga kura za watu . Ni dhambi mbaya sana kwenye jamii.

Leo watu tuliokuwa tunakaa pamoja na kupiga kura na kuhesabu bila vurugu wala kusimamiwa na mabunduki hali imebadilika kwa sababu ya kuvuruga kura halali . Hata kuuana ,kutokana na kujeruhi watu wakati wa uchaguzi au kampeni n.k ni kwa sababu ya kuwaza namna ya kuvuruga zoezi la kura halali .

Kwa hiyo tuwaache Chadema wafanye jambo litakaloipa uhalali wa kuikosoa serikali ya CCM au itakayowanyima kabisa kabisa kabisa uhalali wa kuikosoa CCM.

Walivuruga uchaguzi ni wazi kuwa chama hicho kitakuwa hakina tija kabisa ya siasa za Demokrasia . Bora tuache siasa za kumi kumi za CCM watifuane na kuuana wenyewe mpaka siku akitokea Capt .Mmoja mzalendo na kuibadili nchi kuwa kama Bukina Faso. Wanasiasa hawaipendi nchi zaidi ya matumbo yao ndio maana hawako tayari sio tu kuifia nchi kama wanajeshi bali hata kupoteza madaraka yao kikatiba kupitia kura wanazozipata kama raia.Yaani nchi ya kiraia na kidemokrasia halafu kuna kakundi kadogo kana fanya mapinduzi kijanja kijanja kuompitia vyombo vya dola na kujipa uhalali wa kukaa madarakani kama serikali ya kiraia. Bora iwe jeshi lijulikane kabisa na watu waachane na siasa wachape kazi na kuijenga nchi kizalendo bila unafiki.
 
Actually,
hayo ni matokeo ya wagombea na wafuasi wao kujiapiza kua watashinda uchaguzi licha ya kua hawana wingi wa kura kushinda uchaguzi.

hali hiyo imejenga hali ya mihemko na ghadhabu iliyosababisha kuwe na usugu wa dhana ya ushari kwenye fikra na mawazo ya wananchi kwamba wanaibiwa kura kitu ambacho si kweli kabisa.
Huna sera nzuri zenye ushawishi, huna wafuasi wengi, unashindaje uchaguzi?

kua maskini au tajiri Tanzania ni uamuzi binafsi wa mtu.

Gentleman,
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na majeshi ya ulinzi na usalama yana wajibu wao wa msingi katika kulinda nchi na sio vinginevyo 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…