Lilikuwa jambo la msingi kusimama kwa muda kupisha zoezi la chanjo kuanza bila ya kutatizika.
Muda wa kuitumia karata ya wingi wetu vizuri ili kuyajaza magereza yao sawa sawa umewadia.
Ni muhimu sana tukawaweka wazi wakatuelewa pasi na shaka kuwa:
"hatuogopi kukamatwa na tuko tayari mno kukamatwa kuliko hata kubakia majumbani mwetu."
Huu pia ni muda muafaka wa kuziweka tofauti zetu ndogo ndogo pembeni na wote wenye uhitaji wa katiba mpya kama sisi.
Tuombane misamaha faraghani na hadharani. Tanzania ni muhimu zaidi kuliko yeyote mwenye akili zake kichwani.
Tushirikiane sote, tuyashirikishe makundi na vyama vyote tunavyoweza kushirikiana navyo. Hayupo mmoja mwenye umuhimu zaidi kwenye mpambano mtakatifu huu kuliko mwingine.
Aboubakar Mbowe atafarijika mno kusikia tunaendelea kwa kasi ile ile.
Mkakati wa kuwahami wahanga ni wa muhimu sana. Umekuwa ukiombwa huu kwa muda sasa pasipo na mrejesho.
Ifahamike kuwa ni muhimu mapambano ya kudai katiba mpya yakaeleweka kuwa ni kwa kujitolea kwa hali na mali. Hii isifanywe kuwa fursa na mtu yeyote na kwa namna yoyote (hasa na mawakili).
Miito ya kujitolea iwe wazi kwa wote wakiwamo Sirro na serikali kwa ujumla wao. Wajue kuwa tunataka tume huru sasa na si vinginevyo.
Ni Lazima kuwapo uratibu wa karibu ili kuhakikisha wahanga wanatunzwa sawa sawa kama askari wetu mashujaa wa mstari wa mbele.
Wananchi wako tayari, wanachohitaji ni organization na uongozi thabiti kuendelea na mapambano muda wote bila kujali nani watakuwa wamekamatwa. Wananchi hawawezi kuamka kama mvua bila uongozi uliodhamiria.
Uongozi una gharama ni muhimu wenye hofu wakaachia ngazi sasa. Hizi ni zama mpya.
Ifahamike mafanikio ya Zambia au uwepo wa nchi marafiki hakutatusaidia lolote kama tutaendelea kutegeana.
Habari hii iwafikie kwa ufasaha pale ufipa kabla uvumilivu wetu haujafika mwisho.
Ninawasilisha.