#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

Ukishaongea mambo ya moral justifiction ndiyo umeshaanza ku qalify kitu. Hizo ndizo habari za kulazimisha nurses wachanje.

Na ukilazimisha nurses wachanje, hujalazimisha wananchi wachanje.

Kwa sababu, kama nurse hataki kabisa kuchanja anaweza kuacha kazi.

Mbowe haja qualify hii issue. Ameongea kwa raia wote chanjo ilazimishwe. This is wrong, unethical and will violate minority rights za watu kama Jehovah Witnesses ambao hawakubali chanjo kwa sababu za kidini. Mimi sina dini lakini natetea haki za watu wenye imani zao.

By the way, atatoa tamko ku walk back hii kauli, kwa sababu hata watu wa chama chake wameikataa. Haibebeki.
👏👏👏 Ubarikiwe sana Mkuu.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeomba huduma ya utoaji chanjo ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19), iwe ya lazima badala ya hiari kama ilivyotangazwa na Serikali.

Wito huo umetolewa leo Jumatatu, tarehe 19 Julai 2021 na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, akizungumza na wanahabari jijini Mwanza.

“Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, iweke utaratibu mzuri wa chanjo kuwa ya lazima kwa Watanzania,” amesema Mbowe.

Aidha, Mbowe ameitaka Serikali iongeze juhudi katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na maambukizi ya COVID-19, kwa kuwa wengi hawachukui tahadhari dhidi ya janga hilo.

“Lakini public awareness (uelewa kwa umma) haiko, wala usifikiri Watanzania hawana akili, wamedanganywa hawajui washike la rais au la nani,” amesema Mbowe.

Mbowe ameongeza “ wameweka usugu hawaogopi Corona, wanafikiri ugonjwa huu wanaambukiza wachache.”

Wakati huo huo, Mbowe ameiomba Serikali iweke mkakati wa kutoa matibabu ya COVID-19 bure kwa wananchi, kwa kuwa wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

“Kitu kikubwa hatujakijua ni gharama za matibabu, kimsingi gharama za COVID-19 ilipaswa kusimamiwa na Serikali kwa asilimia 100,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Sababu janga limetengazwa la kidunia na Shirika la Afya Duniani (WHO). Serikali na nchi zake zinawajibika kuwatibu na kuwakinga wananchi.”

Serikali ya Tanzania, imesema imekamilisha muongozo wa kuingiza na kutoa chanjo ya COVID-19, na kwamba zitaingizwa nchini hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi, alisema chanjo hiyo itatolewa bure kwa Wananchi watakaohitaji.

Mwanahalisi
Naona Madalali wanchanjo wameshawashikisha hongo nono huko Ufipa, wendawazimu wakubwa!
 
Ni kweli lakini sio lazima.
Kwa mfano ni lini waathirika wa HIV wakalazimishwa kutumia ARV?
Ni lazima pale inapobidi hasa katika hali ya dharura kama hii ya sasa ya Covid-19. Ndio maana katika nchi zilizoathirika zaidi, wahudumu wa afya wasipofanya hivyo wanaweza kupoteza ajira zao. Utaratibu huu wa chanjo unafahamika duniani kama mandatory vaccination.

Mandatory vaccination, pia vaccine mandates ndizo hizo sera za chanjo za lazima. Ulazima wa chanjo ambao ni halali (justifiable) ni ule unaokubalika kitabibu duniani kote ambao unakuwepo kwa dharura ili kuokoa maisha ya watu walio wengi hasa wale ambao bado hawajachanjwa.

Sera ya kulazimisha chanjo kwa nchi kama Ufaransa kwa mfano, imeweka utaratibu wa kuruhusu raia waliopata chanjo peke yao kutumia baadhi ya huduma za umma kama vile usafiri wa treni n.k.

Serikali haitumii nguvu ya dola physically kuchanja watu (kama wengi wanavyodhani) bali inaweka mazingira ya kuwepo kwa consequences kwa wale watakaogoma kuchanjwa.

Nchi zingine pia zimeweka sera za kuzuia watu ambao bado hawajapata chanjo kuingia ama kufanya kazi katika sehemu kadha wa kadha kama vile kumbi za starehe, viwanja vya michezo, taasisi kama vile shule n.k. ili kuwalazimisha wale wasiochanjwa kubadili maamuzi.

Nchi inaweza kuweka mazingira ya namna hiyo ama ya namna yeyote ile ambayo yanakubalika (justifiable) katika kuhakikisha raia wake wanapata chanjo ili kidhibiti kikamilifu athari zinazotokana na kusambaa kwa magonjwa yanayohatarisha uhai.

Fahamu kwamba haki ya wewe kuishi ama kuwa hai ndiyo haki muhimu zaidi katika haki zote za binadamu, hivyo kuna ulazima ambao ni halali na unaokubalika wa haki hiyo kulindwa kikamilifu pale inapobidi.
 
Fahamu kwamba haki ya wewe kuishi ama kuwa hai ndiyo haki muhimu zaidi katika haki zote za binadamu, hivyo kuna ulazima ambao ni halali na unaokubalika wa haki hiyo kulindwa kikamilifu pale inapobidi.
Kuna watu wanakufa kwa njaa, ushasikia hawa nguruwe wanasema "kila mtu lazima ale ili asife"?

Au hiyo haki ya kuishi ni kwa baadhi ya aspects wanazoamua "miungu watu" kadhaa tu?
 
HIVI KWELI KWAMBA MBOWE HAKUONGELEA HIZO TOZO ZA KIDHALIMU KWA WANANCHI AMEONGELEA KORONA TU?

MBOWE, MBOWE, MBOWE HUKUSIKIA KILIO CHA WATANZANIA KUHUSU HIZO KODI ONEVU, ZA MANYANYASO NA DHULUMA?
Atakuwa amelamba uwakala Wa kupambania chanjo ili avute mpunga Wa kutosha toka ubeberuni. Sisi atatuwaza saa ngapi na jamaa anajulikana kwa namna alivyo very opportunist
 
Inasikitisha chama kinajiita cha demokrasia alafu kinashinikiza watu walazimishwe kuchanjwa.
That's nonsense
Na hapo hawajashika usukan wa nchi
Je tukiwapa ⁉️
 
Chadema ina viongozi wengi wenye maono ya mbali, leo madaktari ndio wanaiona hoja ya Mbowe ilikuwa na mashiko.

 
Chadema ina viongozi wengi wenye maono ya mbali, leo madaktari ndio wanaiona hoja ya Mbowe ilikuwa na mashiko.

Take it from me,usishangae na wao wakaishia jera,
Hivi ni kwa nini hamtaki kuelewa maana ya hiari?
 
Chadema ina viongozi wengi wenye maono ya mbali, leo madaktari ndio wanaiona hoja ya Mbowe ilikuwa na mashiko.


Ni umbumbu wa hali ya juu kutokusikiliza wataalamu wabobezi katika nyanja zao na kujikita kusikiliza mtu kama huyu:

IMG_20210918_202217_811.jpg


Eti kuwa kakubebea maono.

Hiiiiii bagosha!
 
Back
Top Bottom