#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

πŸ‘πŸ‘πŸ‘ Ubarikiwe sana Mkuu.
 
Naona Madalali wanchanjo wameshawashikisha hongo nono huko Ufipa, wendawazimu wakubwa!
 
Ni kweli lakini sio lazima.
Kwa mfano ni lini waathirika wa HIV wakalazimishwa kutumia ARV?
Ni lazima pale inapobidi hasa katika hali ya dharura kama hii ya sasa ya Covid-19. Ndio maana katika nchi zilizoathirika zaidi, wahudumu wa afya wasipofanya hivyo wanaweza kupoteza ajira zao. Utaratibu huu wa chanjo unafahamika duniani kama mandatory vaccination.

Mandatory vaccination, pia vaccine mandates ndizo hizo sera za chanjo za lazima. Ulazima wa chanjo ambao ni halali (justifiable) ni ule unaokubalika kitabibu duniani kote ambao unakuwepo kwa dharura ili kuokoa maisha ya watu walio wengi hasa wale ambao bado hawajachanjwa.

Sera ya kulazimisha chanjo kwa nchi kama Ufaransa kwa mfano, imeweka utaratibu wa kuruhusu raia waliopata chanjo peke yao kutumia baadhi ya huduma za umma kama vile usafiri wa treni n.k.

Serikali haitumii nguvu ya dola physically kuchanja watu (kama wengi wanavyodhani) bali inaweka mazingira ya kuwepo kwa consequences kwa wale watakaogoma kuchanjwa.

Nchi zingine pia zimeweka sera za kuzuia watu ambao bado hawajapata chanjo kuingia ama kufanya kazi katika sehemu kadha wa kadha kama vile kumbi za starehe, viwanja vya michezo, taasisi kama vile shule n.k. ili kuwalazimisha wale wasiochanjwa kubadili maamuzi.

Nchi inaweza kuweka mazingira ya namna hiyo ama ya namna yeyote ile ambayo yanakubalika (justifiable) katika kuhakikisha raia wake wanapata chanjo ili kidhibiti kikamilifu athari zinazotokana na kusambaa kwa magonjwa yanayohatarisha uhai.

Fahamu kwamba haki ya wewe kuishi ama kuwa hai ndiyo haki muhimu zaidi katika haki zote za binadamu, hivyo kuna ulazima ambao ni halali na unaokubalika wa haki hiyo kulindwa kikamilifu pale inapobidi.
 
Fahamu kwamba haki ya wewe kuishi ama kuwa hai ndiyo haki muhimu zaidi katika haki zote za binadamu, hivyo kuna ulazima ambao ni halali na unaokubalika wa haki hiyo kulindwa kikamilifu pale inapobidi.
Kuna watu wanakufa kwa njaa, ushasikia hawa nguruwe wanasema "kila mtu lazima ale ili asife"?

Au hiyo haki ya kuishi ni kwa baadhi ya aspects wanazoamua "miungu watu" kadhaa tu?
 
HIVI KWELI KWAMBA MBOWE HAKUONGELEA HIZO TOZO ZA KIDHALIMU KWA WANANCHI AMEONGELEA KORONA TU?

MBOWE, MBOWE, MBOWE HUKUSIKIA KILIO CHA WATANZANIA KUHUSU HIZO KODI ONEVU, ZA MANYANYASO NA DHULUMA?
Atakuwa amelamba uwakala Wa kupambania chanjo ili avute mpunga Wa kutosha toka ubeberuni. Sisi atatuwaza saa ngapi na jamaa anajulikana kwa namna alivyo very opportunist
 
Inasikitisha chama kinajiita cha demokrasia alafu kinashinikiza watu walazimishwe kuchanjwa.
That's nonsense
Na hapo hawajashika usukan wa nchi
Je tukiwapa ⁉️
 
Chadema ina viongozi wengi wenye maono ya mbali, leo madaktari ndio wanaiona hoja ya Mbowe ilikuwa na mashiko.

 
Take it from me,usishangae na wao wakaishia jera,
Hivi ni kwa nini hamtaki kuelewa maana ya hiari?
 

Ni umbumbu wa hali ya juu kutokusikiliza wataalamu wabobezi katika nyanja zao na kujikita kusikiliza mtu kama huyu:



Eti kuwa kakubebea maono.

Hiiiiii bagosha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…