Pre GE2025 Chadema chini ya Lissu tumieni nguvu hiyo kukiimalisha CHAMA kuliko kutumia kuzuia uchaguzi.

Pre GE2025 Chadema chini ya Lissu tumieni nguvu hiyo kukiimalisha CHAMA kuliko kutumia kuzuia uchaguzi.

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Gabeji

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
1,530
Reaction score
1,903
Poleni na hongereni na kutafuta mkate wa kila siku. Chadema mpya hongereni na harakati za kuleta mabadiliko ya kikatiba kwa Tanzania.

Tumeona nia yenu ni njema sana ktk kuleta na kupigania haki ndani ya nchi yetu." Hoja hii ya No reform No election" ipo vzr sana, lakini kwa maoni yangu , ni vzr mh lisu pamoja na kamati kuu mkajikita katika kukijenga CHAMA zaidi kuliko kutumia nguvu kubwa ya kuzua uchaguzi mwaka huu na uchaguzi ukafanyika pasipo kufanikiwa. Kwa nn hamwezi kufanikiwa?
1. Uchawa umeota mizizi kila kona ya nchi.
2. Hakuna elimu ya kupigania haki Tanzania
3. Uoga, ubinfsi, usinichi, ni tatizo Tanzania
4. Historia na utamaduni wa watanzania. Unakuta mtu anatekwa, mbele yao, ndani ya basi, wanamwangalia tu,anapigwa ,anauwa,mbele ya watu wanamwangalia tu,
5. Tujiulize swali hili, ni wanafamilia wangapi wamepotea, wametwa, wameuwawa ? Tangu mjomba na mama waingie madaraka na hakuna wanafamilia waliojikusanya kwa pamoja na kuandamana kwenda kwa waziri mkuu? Ukiwa watu hawa wameshindwa kuandamana kudai uwai na haki za ndugu zao wa damu zaidi ya familia 200 ,je wataweza kuandamana kuzuia uchaguzi usifanyike? Simple logic Big No,

Nini kifanyike?

Nguvu hiyo ya kuzuia uchaguzi itumike kukijenga CHAMA, kueneza itikadi, kueneza sera, kutoa elimu ya kizalendo, kutoa elimu ya kupigania haki, sehemu mbalimbali, kwa mfano mikoa ya morogoro, lindi, mtwala, Ruvuma,katavi, pwani, tanga, chadema ipo kwa mbali sana au hakuna kabisa.
Mungu ibariki Tanzania by mwinjilist wenu Gabeji.
 
Back
Top Bottom