Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
- Thread starter
- #61
Naunga mkono hoja, na katika vikao hivyo, wasisitize heshima kwa viongozi, mtu akiishakuwa kiongozi, lazima aheshimiwe. Mfano Mwenyekiti Mbowe, amefanya vikao vya maridhiano na CCM na vikaleta manufaa makubwa Chadema, ikiwemo kupata ruzuku na kukubaliana kitu kinachoitwa kugawana nusu mkate.
Wakati wote wa vikao hivyo Makamo Mwenyekiti yeye alikuwa zake Ubelgiji kwa wazungu wake.
Chadema ilisaidiwa fedha za vikao vya Baraza Kuu, kufanya ziara nje ya nchi, na fedha za nauli kuwarejesha wakimbizi waliokimbilia nje ya nchi akiwemo yeye.
Aliporudi, badala ya kuwa ni mtu wa shukrani, akaanza kubeza maridhiano na kuwatukana viongozi wenzake hadharani kuwa hawana akili!. Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability? hebu msikilize mwenyewe hapa
View: https://youtu.be/Qa59DIQs2yI?si=9oIbwnDXvO-cDzed
Wakati Lissu anaponda maridhiano, angalia JJ Mnyika anasema nini kuhusu maridhiano,
View: https://youtu.be/x5yFws4dc1U
Hivyo naunga mkono hoja, Chadema lazima waitane, wakalishane chini, wasemezane, na kurekebishana.
P.
licha ya mbowe kufanya mazungumzo mazuri sana ya maridhianao na ccm, KM mnyika anaadmit bayana manufaa ya maridhiano jinsi yalivyowanufaisha waandamizi chadema, lakini pia wanasiasa nchini kwa ujumla, lakini makamu mwenyekiti haoni hayo mpaka anawazodoa wenzie hadharani, ati sijui ilikuaje mpaka BAWACHA wakamualika Raisi mkutano wao, bila kujua huo ulikua utashi wa kipekee sana wa kisiasa kuendeleza maridhiano ya dhati, ambayo yalikua yanaenda vizuri sana.....
mi nadhani yanayoendelea chadema yana sababu kadhaa ambazo miongoni mwao ni pamoja na,
kuna kiongozi mzito mwandamiz miongoni mwao anapanga kuhamia kwenda chama kingine kwasababu ya kutokua na uhakika wa kupewa nafasi kutimiza ndoto zake za kuwania nafasi ya juu nchini, lakini na yeye amekusudia mpaka ahakikishe ameimegua chadema kwa kiasi fulani kisha ndipo aondoke...

