Pre GE2025 Chadema fanyeni vikao vya ndani kukosoana, kurekebishana, na kusahihishana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
licha ya mbowe kufanya mazungumzo mazuri sana ya maridhianao na ccm, KM mnyika anaadmit bayana manufaa ya maridhiano jinsi yalivyowanufaisha waandamizi chadema, lakini pia wanasiasa nchini kwa ujumla, lakini makamu mwenyekiti haoni hayo mpaka anawazodoa wenzie hadharani, ati sijui ilikuaje mpaka BAWACHA wakamualika Raisi mkutano wao, bila kujua huo ulikua utashi wa kipekee sana wa kisiasa kuendeleza maridhiano ya dhati, ambayo yalikua yanaenda vizuri sana.....

mi nadhani yanayoendelea chadema yana sababu kadhaa ambazo miongoni mwao ni pamoja na,
kuna kiongozi mzito mwandamiz miongoni mwao anapanga kuhamia kwenda chama kingine kwasababu ya kutokua na uhakika wa kupewa nafasi kutimiza ndoto zake za kuwania nafasi ya juu nchini, lakini na yeye amekusudia mpaka ahakikishe ameimegua chadema kwa kiasi fulani kisha ndipo aondoke...
 
Alichofanya Tundu Lisu ni approach sahihi kabisa. Unapoona upuuzi popote unaukemea hadharani ama ndani. Haya mambo ya kupotezeana muda kwenye vikao vya ndani ndio kulea wapuuzi wanaopewa pesa chafu na ccm.
unakemea kitu kunacho kuathiri wewe mwenyewe na familia yako kisiasa. sawa kemea, si ukae ndani basi na wenzie mkemeane vizuri kama familia
 
kwahiyo uchaguzi wa chadema unaoendelea ni credible?

na,
kwani uchaguzi anao ulalamikia na kuukosoa Lisu unasimamiwa na serikali kupitia tume huru ya uchaguzi?

au uchaguzi wa chadema nao ni upuuzi wa mtu mweusi kama ambavyo unadai, japo ni lugha za mihemko za waliofilisika kwa hoja na kisiasa?
 
unakemea kitu kunacho kuathiri wewe mwenyewe na familia yako kisiasa. sawa kemea, si ukae ndani basi na wenzie mkemeane vizuri kama familia
Kwani amekemea hiyo tabia akiwa nje ya nchi? Hapo ujumbe umefika baina ya wapokea fedha chafu, watoa hizo fedha chafu. Ametusaidia sisi tusioingia kwenye hivyo vikao vya ndani kujua kuhusu hizo fedha chafu.
 
Hauna credibility, ndio maana Lisu ametoka kutujulisha wananchi juu ya uwepo wa hizo fedha chafu.

Uchaguzi unaosimamiwa na serekali huo sio uwepo wa fedha chafu tu, bali huo ndio uchafu halisi.
 
Hauna credibility, ndio maana Lisu ametoka kutujulisha wananchi juu ya uwepo wa hizo fedha chafu.

Uchaguzi unaosimamiwa na serekali huo sio uwepo wa fedha chafu tu, bali huo ndio uchafu halisi.
kwahiyo kuishia kuwajulisha itawasaidia nini bila kuchukua hatua?
 
Kwani amekemea hiyo tabia akiwa nje ya nchi? Hapo ujumbe umefika baina ya wapokea fedha chafu, watoa hizo fedha chafu. Ametusaidia sisi tusioingia kwenye hivyo vikao vya ndani kujua kuhusu hizo fedha chafu.
kwahiyo yeye anafadhiliwa na fedha safi za mabwenyeye wa magharibi, right?

ni vizuri akaeleza pia ameshapewa ngapi na mabwenyeye ya huko ng'ambo maana ni bayana ni fedha nyingi sana,

na ndio maana waliporuhusiwa kufanya mikutano ya hadhara kwa mara ya kwanza kabisa baada ya kuruhusiwa walifanya nae pamoja, na kama kamati kuu walikubaliana nadhani kuishia mwanza kama sio kahama wakati ule....

but kwa ubinafsi na wingi wa fedha alizokua nazo, yeye pekeyake na kundi lake wakataka kuendelea kufanya mkutano huko ngorongoro akakamatwa baada ya kugalagala barabarani, na viongozi waandamizi wenzie wakamchunia
 
Huko nyuma tulisema humu namna ambavyo ndugu Mbowe anang'ang'ania madaraka hata baada uongozi wake kuishiwa mbinu za kuisogeza mbele Chadema lakini tuliishia kutukanwa.
Sasa ni dhahiri tuliyoyaona miaka kadhaa nyuma yanaletwa hadharani.

Hata hivyo pamoja na mapungufu ya Mbowe sikubaliani na kashfa za Tundu Lisu dhidi ya suala la rushwa.
Kama Abdul na mama Abdul wanatoa , basi kuna wanaopokea rushwa hiyo ndani ya Chadema.
Kwa tuhuma zile tuamini kwamba Mbowe na Mnyika wanafaidika na rushwa hizo kwa manufaa yao binafsi.
Haya ni matusi si kwa mama Abdul tu, ni matusi mazito kwa viongozi wenzake ndani ya chama chake.

Chadema kina vikao mbalimbali vya nidhamu, ni vema wakakutane, wachambane huko, wapigane huko, wakija hadharani waheshimiane na jamii itawaheshimu.
Kuja kulopoka hadharani ni kuishiwa hoja na ushawishi.
 
Lisu ni mwanaharakati, siyo Statesman.

Ndio maana yule malaika wa kuzima alishindwa kumvumilia na kumtumia kikosi cha wauwaji, kumvumilia Lisu inataka moyo sana.
 
Lissu ana tamaa ya madaraka mno halafu ana dharau ila hana maisha marefu kwenye siasa bora kuishi na dr Silaa lakini siyo Tundu lissu.Yeye anafikiri ni msomi mwenye uwezo pekee,hana diplomasia,hekima,busara na hoja za kuleta maelewano ndani ya chama chake na Taifa zima. Anatumika nje,chadema wachukue tahadhari naye siyo mtu mzuri
 
Tundu Lisu ni dikteta.
Watanzania watafanya kosa kubwa sana kuchagua dikteta wa mfano wake.
Mbowe ingawa anang'ang'ania madaraka lakini hana dharau wala majivuno kama Lisu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…