Kinachonishangaza Wana chadema wengi ni wabishi balaa ,ajabu wapo dar .
Mnapoambiwa ukweli ufanyieni kazi.
Chadema ni Chama kinachodeal na nyomi la watu kwenye mikutano yao na wanaridhika balaa .
Labda nitoe mfano hai .Mimi naishi mjini na vijijini ,Kuna muda nakua mjini muda nakua vijijini ,ni nusu kwa nusu.
Ukweli usemwe kwa upande wa vijijini chadema bado haijakubalika kabisa na wananchi ,wengi wameaminishwa Kama ni Chama Cha wamwaga damu ,hizi ni propaganda za ccm huko kijijin na zimezaa matunda sabab wapo karibu na hao wanakijiji bega kwa bega.
Ukiona Kuna Kijiji chadema ime take over Basi jua hicho kijiji walau kina wasomi wengi na kina maendeleo ya kutosha na watu wa hicho kijiji wameelimika vyema .
Lakin kwa vijiji ambavyo elimu bado huko ndiko ccm imekamata haswa.
Sasa swali la kujiuliza ni vijiji vingap kwenye hii nchi vina wasomi wengi na kustarabika na kuijua dunia ya leo?
Jibu ni vijiji vichache Kati ya vilivyo vingi.
So chadema mnaposhauriwa kubalin ukweli ,kura zipo vijijini ,huko mjin Kuna mashabik wa siasa tu na siku ya kura hawatokei kabisa .
So nyomi kwenye mikutano haiwez kuitoa ccm kamwe km hamtabadirika na kukubal ukweli.
Wekezen vijijini ,nguvu iwe vijijini ,tembea Kijiji kwa Kijiji ,au kata kwa kata ili watu waelimishwe .
Bahat mbaya hatuwez kueleweka hapa Ila km hamtabadirika hamuwez kuitoa ccm madarakan ,kisingizio kitabak mnaibiwa kura Mara polisi .
Povu ruksa.