CHADEMA hatutaki mjisifie kujaza watu mikutanoni, bali kuwatoa Kimkakati CCM Madarakani

CHADEMA hatutaki mjisifie kujaza watu mikutanoni, bali kuwatoa Kimkakati CCM Madarakani

Ndio maana nasema iwepo tume huru ya uchaguzi ili ukweli wa kukubalika kwa chama ufahamike. Sio unasema una ukubwa na unakubalika, kisha wakati wa uchaguzi tunaona mabox ya kura yanaletwa vituoni yakiwa yamejazwa kura za CCM kwa uratibu wa vyombo vya dola.
Mkuu hata chadema ilimchukua Lowassa kutoka ccm na vyama vikaunganisha nguvu, hayo ndio mambo ya uchaguzi.
 
Kuwa CCM inategemea vyombo vya dola wala hilo halihitaji mjadala. CDM haiwezi kuwa bora iwapo bado katiba inatoa mwanya kwa chama kilichochoka kupanga nchi iendeshwe vipi.
Hata mbadala wa Mbowe hakuna nako unalaumu ccm?
 
No,

Sina upande ndomana unaweza niona hivyo,

CCM naiombea ife haraka iwezekanavyo, Bt napoangalia vyama vyenye uwezo wa kuiua CCM haviko serious napata hasira zaidi.

CDM naikubali na kuipenda ndomana naisema iongeze ubora.

Mkuu nilikushauri anzisha chama kifanye unavyotaka, hiyo CDM haibadiliki labda Mbowe aachie uenyekiti wa kudumu.
 
Mkuu hata chadema ilimchukua Lowassa kutoka ccm na vyama vikaunganisha nguvu, hayo ndio mambo ya uchaguzi.

Sikuwahi kuikubali mbinu ya kuokota wagombea tena wa CCM dakika za majeruhi. Hata hivyo kumchukua Lowassa huwezi kufananisha na kuletwa mabox ya kura yasiyo halali kwenye vyumba vya kura. Labda kama hujui unaongea nini?
 
Hata mbadala wa Mbowe hakuna nako unalaumu ccm?
Siungi mkono uwepo wa Mbowe kwenye nafasi hiyo zaidi ya miaka 10, lakini uwepo wa Mbowe muda wote huo ndio excuse ya wizi wa kura unaofanywa na CCM? Isije ikawa umelewa boss na hili jua kali.
 
Umesema kwel bila kujikita vijijin hahawez kuwatoa ccm.labda wameridhika na pesa ya ruzuku
 
Kampeni za uchaguzi 2020 walikuwa wanashindana na Magufuli kujaza uwanja.
Issue ya kujaza ni sehem tu ya kujimwambafy kwa vyama vya siasa ili mradi kujivunia popularity! Refer wale jamaa Brethren greens walivyokua wanajazwa kweny malori ili tu ionekane nyomi, but haikua agenda ya CCM!!
 
Mkuu nilikushauri anzisha chama kifanye unavyotaka, hiyo CDM haibadiliki labda Mbowe aachie uenyekiti wa kudumu.
It's too late kuanzisha chama by nw!

Hali ngumu ya kiuchumi italazimisha muunganiko wa makundi mbalimbali kupambania mabadiliko.

Tusubiri.
 
It's too late kuanzisha chama by nw!

Hali ngumu ya kiuchumi italazimisha muunganiko wa makundi mbalimbali kupambania mabadiliko.

Tusubiri.
Mnangoja nini boss wakati goli liko wazi?
 
Twende na HOJA ya KATIBA mpya na TUME HURU ya UCHAGUZI,

Wakikataa tutangana nanyi TINDO& co tkt maandamano ya AMANI.

Ndio nasema mnangoja nini kudai hiyo katiba mpya?
 
Ndio nasema mnangoja nini kudai hiyo katiba mpya?
Tulishaanza kitambo kudai, tunaendelea na kuunganisha makundi mbalimbali,

KATIBA mpya ni ya wananchi Kwa ujumla na Si Kwa ajili ya makundi ya kisiasa za vyama pekee.

Nauona ujio wa Dr Slaa CDM, hii ni njema ktk kudai KATIBA, maana Mzee huyu alisaidia sana Hadi KIKWETE kukubali kuanzisha mchakato Ule.
 
Sikuwahi kuikubali mbinu ya kuokota wagombea tena wa CCM dakika za majeruhi. Hata hivyo kumchukua Lowassa huwezi kufananisha na kuletwa mabox ya kura yasiyo halali kwenye vyumba vya kura. Labda kama hujui unaongea nini?
Point hapo ni kwamba kama Chadema inakubalika vya kutosha isingehitajika kuchukua wagombea kutoka ccm, ila wenyewe wanasema Lowassa kaongeza idadi ya kura na viti bungeni.
 
Kabla hata ya kura kupigwa huwa CCM ina uhakika wa kura za wahadzabe, kina mama, wazee, na makundi mengine ambao huonekana sio wasomi mbele ya CHADEMA. Wapinzani hawana kabisa mbinu za kushinda uchaguzi kwenye sanduku la kura huwa wanaweka nguvu kubwa sana mitandaoni huku wakidhani CCM wanafanya ujinga kugawa tshirts, kanga na sare zingine za chama kwa wapiga kura wake.
 
Siungi mkono uwepo wa Mbowe kwenye nafasi hiyo zaidi ya miaka 10, lakini uwepo wa Mbowe muda wote huo ndio excuse ya wizi wa kura unaofanywa na CCM? Isije ikawa umelewa boss na hili jua kali.
Mimi sizungumzii maoni yako binafsi kuhusu Mbowe, mie nasema kwamba hadi sasa chadema haina mbadala wa Mbowe.

Wizi wa kura wa ccm wenyewe mmeukubali na kuuridhia, hamkuukubali tu huo mnaoita ubakaji wa uchaguzi 2020 ila wizi wa kura kwenu mlishaukubali.
 
Kila nikimsikia mwana CHADEMA simsikii akinipa mikakati yenu ya kuitoa (kuing'oa) CCM madarakani bali nasikia tu wakijisifia kujaza watu (nyomi) katika mikutano yao huko mkoani/mikoani.

Nilishawahi kuwashaurini huko nyuma kuwa jiimarisheni sana katika kujijenga ngazi za chini ila nasikitika hili hamjalifanyia kazi na mnambwelambwela tu huku mkitafuta umaarufu na uungwaji mkono na Watanzania walioko mijini na wale wa mitandaoni wakati tafiti zinasema 85% ya wapiga kura wako vijijini.

Kwa Upuuzi wenu huu wa kila mwana CHADEMA kujisifia kujaza watu badala ya kuja na mikakati kabambe kupambana na kuitoa CCM,niwahakikishieni CCM iliyosheheni mafundi wa siasa na mikakati itaendelea kuitawala/kutawala Tanzania hata kwa miaka milioni 100 ijayo.
Kuna mtu aliniambia Genta amepona siku hizi kumbe kanidanganya!
 
Point hapo ni kwamba kama Chadema inakubalika vya kutosha isingehitajika kuchukua wagombea kutoka ccm, ila wenyewe wanasema Lowassa kaongeza idadi ya kura na viti bungeni.

Sijawahi kuamini huo uongo kuwa eti Lowassa anakubalika, na aliongeza kura upinzani hasa CDM, angeenda TLP apate kura milioni 6 ningeelewa ila sio CDM. CDM kuokoteza wagombea dakika za mwisho hasa CCM ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
 
Mimi sizungumzii maoni yako binafsi kuhusu Mbowe, mie nasema kwamba hadi sasa chadema haina mbadala wa Mbowe.

Wizi wa kura wa ccm wenyewe mmeukubali na kuuridhia, hamkuukubali tu huo mnaoita ubakaji wa uchaguzi 2020 ila wizi wa kura kwenu mlishaukubali.

Sasa mimi sio msemaji wa CDM, ni wazi ukiniuliza mimi nitakupa maoni yangu sio ya CDM. Sina popote nakubaliana na kiongozi yoyote kukaa madarakani zaidi ya miaka 10, ikiwemo huyo Mbowe. Hao wanaoamini kwa Mbowe nenda ukawaulize wao.

Onyesha popote tunapokubaliana na wizi, 2020 haukuwa wizi bali uporaji wa mchakato.
 
Sijawahi kuamini huo uongo kuwa eti Lowassa anakubalika, na aliongeza kura upinzani hasa CDM, angeenda TLP apate kura milioni 6 ningeelewa ila sio CDM. CDM kuokoteza wagombea dakika za mwisho hasa CCM ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
Usitake kuwafanya viongozi wa chadema ni wapumbavu kwamba wewe ndio unajua sana kuliko wao, wao wameona wakichanganya nguvu ya chadema na kukubalika kwa Lowassa kutaongeza nguvu na kweli tumeona ongezeko la idadi ya kura halafu wewe unasema ni uongo.
 
Back
Top Bottom