CHADEMA hatutaki mjisifie kujaza watu mikutanoni, bali kuwatoa Kimkakati CCM Madarakani

CHADEMA hatutaki mjisifie kujaza watu mikutanoni, bali kuwatoa Kimkakati CCM Madarakani

Sasa mimi sio msemaji wa CDM, ni wazi ukiniuliza mimi nitakupa maoni yangu sio ya CDM. Sina popote nakubaliana na kiongozi yoyote kukaa madarakani zaidi ya miaka 10, ikiwemo huyo Mbowe. Hao wanaoamini kwa Mbowe nenda ukawaulize wao.

Onyesha popote tunapokubaliana na wizi, 2020 haukuwa wizi bali uporaji wa mchakato.
Mimi sijakuuliza kuhusu chadema bali nakuhabarisha kuwa chadema hadi sasa hakina mbadala wa Mbowe.

Nguvu kubwa inatumika kuusema uchaguzi wa 2020 kiasi kwamba kwa mtu mgeni anaweza kufikiri chaguzi za nyuma zilikuwa shwari ndio maana unasema haukuwa wizi(ambao mlishauzoea) bali ni uporaji wa mchakato.
 
Usitake kuwafanya viongozi wa chadema ni wapumbavu kwamba wewe ndio unajua sana kuliko wao, wao wameona wakichanganya nguvu ya chadema na kukubalika kwa Lowassa kutaongeza nguvu na kweli tumeona ongezeko la idadi ya kura halafu wewe unasema ni uongo.

Ww kwako viongozi ni watu wenye akili sana, hivyo wakisema au kufanya lolote wako sawa. Kama ww uko hivyo, mimi siko hivyo. Kuongezeka kwa kura lilikuwa ni jambo lisilokwepeka kwa CDM. Huyo Lowassa angeenda kupandisha kura za TLP au Chauma.
 
Mimi sijakuuliza kuhusu chadema bali nakuhabarisha kuwa chadema hadi sasa hakina mbadala wa Mbowe.

Nguvu kubwa inatumika kuusema uchaguzi wa 2020 kiasi kwamba kwa mtu mgeni anaweza kufikiri chaguzi za nyuma zilikuwa shwari ndio maana unasema haukuwa wizi(ambao mlishauzoea) bali ni uporaji wa mchakato.

Mimi najua kuna mbadala wa Mbowe huko CDM. Hili sikulamishi bali ndio uhalisia.

Chaguzi za kabla ya 2020 kulikuwa na wizi wala hazikuwa chaguzi fair. Lakini uchaguzi wa 2020 ulikuwa ni maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Ww kwako viongozi ni watu wenye akili sana, hivyo wakisema au kufanya lolote wako sawa. Kama ww uko hivyo, mimi siko hivyo. Kuongezeka kwa kura lilikuwa ni jambo lisilokwepeka kwa CDM. Huyo Lowassa angeenda kupandisha kura za TLP au Chauma.
Wewe unaleta ubishi tu, nimekwambia chadema kama chama kina nguvu yake na Lowassa ana nguvu yake wameunganisha hizo nguvu. Sasa unaponitajia TLP na Chauma inaonesha hautaki kuelewa.

Kama viongozi wa chama ambao wanayajua ya ndani ya chama kuliko wewe wanaona uhitaji wa kuvuta watu kutoka upande wa pili ili kuongeza nguvu ila wewe uliyo nje kabisa ndio unajifanya unajua sana kuliko wao tena bila hoja zozote.
 
Hiyo nguvu iliyovutwa na CDM iko wapi Sasa hivi?
 
Kila nikimsikia mwana CHADEMA simsikii akinipa mikakati yenu ya kuitoa (kuing'oa) CCM madarakani bali nasikia tu wakijisifia kujaza watu (nyomi) katika mikutano yao huko mkoani/mikoani.

Nilishawahi kuwashaurini huko nyuma kuwa jiimarisheni sana katika kujijenga ngazi za chini ila nasikitika hili hamjalifanyia kazi na mnambwelambwela tu huku mkitafuta umaarufu na uungwaji mkono na Watanzania walioko mijini na wale wa mitandaoni wakati tafiti zinasema 85% ya wapiga kura wako vijijini.

Kwa Upuuzi wenu huu wa kila mwana CHADEMA kujisifia kujaza watu badala ya kuja na mikakati kabambe kupambana na kuitoa CCM,niwahakikishieni CCM iliyosheheni mafundi wa siasa na mikakati itaendelea kuitawala/kutawala Tanzania hata kwa miaka milioni 100 ijayo.
Chadema haiwezi kuitoa CCM madarakani, kama nyie wananchi hamtoi ushiriakiano.
 
Hapa unashauri au unaumizwa na mikutano ya CHADEMA kuwa na nyomi kubwa?

Moja ya ishara ya chama cha siasa kuwa kinakubalika ni ni pale ambapo ukiitisha mkutano wa hadhara watu wanaitikia na kuja wenyewe kwa wingi (nyomi) na Kwa hiari yao bila ushawishi wa kanga au kofia au pesa kama wafanyavyo CCM..

Kupitia mikutano hiyo mipango na mikakati ya ushindi katika chaguzi mbalimbali huelezewa Kwa watu. Aidha chama hutumia fursa hiyo kuweka wazi sera za chama.

Vivyo hivyo, kupitia mikutano hiyo chama huvuna wanachama wapya wasio na vyama na wale wanaovutiwa na chama hiki..

Wewe unadhani ni kwanini CCM kupitia kwa mpuuzi wao yule aliyekuwa anajiita Rais hayati John P. Magufuli aliamua kuvunja katiba na sheria za nchi Kwa ubabe tu hata akapiga marufuku shughuli halali za siasa za vyama VINGINE vya siasa isipokuwa CCM tu..?

Kama ulikuwa hujui, basi sababu ni hii ambayo hata wewe naona imekutia hofu ----- yaani vyama kama CHADEMA kujaza nyomi na kueleza udhaifu au mapungufu ya serikali ya CCM...!!

Na honestly, Mimi sijakuelewa kwanini unaonekana kubeza nyomi la watu ambalo CHADEMA inakusanya Kila mahali huku ukitambua kabisa kuwa, hiyo ndiyo ishara kuu ya kukubalika Kwa chama Cha siasa chochote...!!
 
Back
Top Bottom