CHADEMA hatutaki mjisifie kujaza watu mikutanoni, bali kuwatoa Kimkakati CCM Madarakani

Sasa CDM wana hao watu wa kuingia nao msituni hata kama wakiwa na silaha? Maandamano tu huwa yanakosa watu na hiyo ina tafsiri nyingi ila nyie huwa mnatoa jibu moja tu la kwamba watu wanaogopa silaha za jeshi la polisi. Chadema haiwezi kujilinganisha na ccm hata ccm isipotumia dola.
 
Hujui unachoongea, kama CCM ingekuwa na sifa hizo ambazo CDM haiwezi kujilinganisha nayo, tusingeona chaguzi za kishenzi vile. Labda kitu pekee ambacho CDM haiwezi kujilinganisha na CCM ni umri wa chama kuanzishwa, sio kwa ubora au zaidi ya hapo.

Na kwa taarifa yako hata hao CCM hawana uwezo wowote wa kupambana na mtu mwenye silaha, zaidi ya kufaidika na hiyo mbeleko ya vyombo vya dola. Ushahidi ni uvamizi wa hawa panya road, ilitakiwa tuone wanaccm wakijitokeza kupambana na watu wenye silaha, lakini sio mtendaji wa kijiji wala mtaa hujitokeza kupambana nao.
 
Sijui huwa mna akili gani yani? Mnakubali kuwa ccm bado ipo madarakani hadi leo kwa sababu ya kutumia dola ila hapo hapo unataka kuniambia Magufuli aliogopa mikusanyiko ya watu kwenye kampeni za chadema kwa lipi? Kwamba wale wote ni walipigia kura chadema au ile nyomi inafanya chadema kuwa na nguvu ya umma na kuweza kufanya lolote?

Kitendo cha kushindana kwa nyomi na chama ambacho mnasema kinategemea dola unatakiwa uwatafakari hao watu wenye kujaa maana nilitegemea ccm kukosa watu kabisa hata wa kuwabeba kwenye magari.
 
Eti ukweli. Ukweli gani kutoka kwa uvccm kama wewe. Kwani wamekutuma uwaambie huo ukweli? Kaa nao huo ukweli ukusaidie wewe. Chadema wamejitosheleza.
 
Upewe mikakati kama nani? Watu kwa kujipa umaarufu hamjambo. Waache Chadema na Chadema yao. Hawahitaji ushauri kutoka kwa mtu anayejificha nyuma ya keyboard kama wewe.
 
Sasa chadema inaweza kujilinganisha nini na ccm au chadema inamzidi nini ccm nje ya kutumia dola?

Chama ambacho hadi sasa wenyewe wanakiri hakina mbadala wa mtu kama Mbowe tu.
 
CCM haiwezi kukosa watu ama kukosa kura kabisa kutokana na sababu za kihistoria, na ufaidika wake wa vyombo vya dola. Lakini CCM haiwezi kukubali matokeo halali kutangazwa, maana wanajua huo ndio utakuwa mwisho wake. Nyomi si ndio kura boss, au kwakuwa kura kwenu zinatoka na kunajisi uchaguzi ndio maana unaona nyomi haina maana?

Isitoshe hakuna chama chochote kinachokosa watu au kura kabisa, tofauti ipo kwenye wingi wa watu na kura. Ndio maana tunasisitiza tume huru ya uchaguzi ili ukweli wa nguvu ya kila chama ufahamike. Haya mambo ya mwenyekiti wa CCM na kigenge chake wanaojiita system kupanga uongozi, yamepitwa na wakati.
 
Why CDM wakupiganie wewe kama unaona ccm imekuchosha?,why uzuzu huu umekua sehemu ya middle class ya kuamini watu wengine wakupiganie, mtoa hoja kama unaona haki yako imesitishwa push back mwenyewe usisubiri wengine wakupiganie
 
Sasa chadema inaweza kujilinganisha nini na ccm au chadema inamzidi nini ccm nje ya kutumia dola?

Chama ambacho hadi sasa wenyewe wanakiri hakina mbadala wa mtu kama Mbowe tu.

Narudia tofauti ipo ila sio ya ubora boss. Inaonekana unataka kuonyesha kuwa CCM ni bora kuliko CDM, lakini kiuhalisia CCM ni kubwa na ukubwa wake umetokana na sababu za kihistoria zaidi na sio ubora. Na iwapo CCM itatoka madarakani na kukosa mbeleko ya vyombo vya dola, chama hicho kitakufa kama yalivyokufa mashirika ya umma. Akili iliyoua mashirika ya umma yaliyokuwa katika uzalishaji, ndio akili itakayiongoza ccm baada ya kupoteza madaraka, ambapo kifo hakitaepukika.

Na kwa kukusaidia zaidi katazame majengo na viwanja vya mpira ilivyorithi toka mfuko wa chama kimoja yana hali gani, na hapo bado iko madarakani muda wote. Je ikitoka madarakani itakuwaje?
 
Mleta mada kasema Kweli,

CCM Ina mtandao Hadi chini kabisa, mabalozi wa nyumba kumi ni CCM,

Majiji yote CDM waliposhinda ni walipata uungwaji mkono Kutoka Wanachama wa CCM baada ya kugawanyika kimaslahi.

CDM inafanya vizuri, bt jitihada zaidi zinahitajika,

Mm kijijini aliko Babu yangu Huwa nikimuuliza habari ya CDM hata hafahamu kuwa Kuna chama kama hicho.
 
Eleza basi huo ubora wa chadema uliyomzidi ccm?
 
Sasa kama hizo sababu za kihistoria bado zinaendelea kufanya ccm kuwa na nyomi la watu basi hilo ni la kulitizama kuliko kuendelea kutaka kutuaminisha kwamba ccm si lolote inategemea dola tu.
 
Huyo babu yako si ndio wale wanaoenda na mtu kumuonyesha wapi aweke alama ya mgombea anayemtaka? Katika zama hizi bado unategemea wazee ndio walete mabadiliko?! CDM hata isipopata kura ya mzee hata mmoja bado inaweza kuingia ikulu kwa kura halali. Vijana walioko chini ya miaka 35 ni 75% ya watanzania wote. Sasa wana haja gani ya kuhangaika na huyo babu yako asiyeijua cdm?
 
Eleza basi huo ubora wa chadema uliyomzidi ccm?

Sijasema CDM ni bora, labda ww useme huo ubora wa CCM maana mimi siuoni zaidi ya ukubwa unaochangiwa na mazingira ya katiba outdated.
 
Sasa kama hizo sababu za kihistoria bado zinaendelea kufanya ccm kuwa na nyomi la watu basi hilo ni la kulitizama kuliko kuendelea kutaka kutuaminisha kwamba ccm si lolote inategemea dola tu.

Ndio maana nasema iwepo tume huru ya uchaguzi ili ukweli wa kukubalika kwa chama ufahamike. Sio unasema una ukubwa na unakubalika, kisha wakati wa uchaguzi tunaona mabox ya kura yanaletwa vituoni yakiwa yamejazwa kura za CCM kwa uratibu wa vyombo vya dola.
 
Uko sawa.

CDM yaweza shinda uchaguzi Kwa kura za vijana pekee.

Bt uongozi ni kuongoza Marika na kufika maeneo yote.

So haja ya kwenda deep na ground Zaid inabaki pale pale.
 
Sijasema CDM ni bora, labda ww useme huo ubora wa CCM maana mimi siuoni zaidi ya ukubwa unaochangiwa na mazingira ya katiba outdated.
Kumbe hata hiyo chadema yako huoni ubora wake sasa sijui unapiga kelele za nini? Imarisheni chama chenu kiwe bora sio kutwa kuimba wimbo wa ccm kutegemea dola mara sijui ccm imechokwa halafu hapo hapo mnashindana kwa nyomi.
 
Uko sawa.

CDM yaweza shinda uchaguzi Kwa kura za vijana pekee.

Bt uongozi ni kuongoza Marika na kufika maeneo yote.

So haja ya kwenda deep na ground Zaid inabaki pale pale.

Ni kweli, lakini sio kufuata hao wazee uliosema wala hawaijui CDM. Naona propaganda mfu za CCM zimekupoteza, na sasa unazitumia kujenga hoja zako hadi unaonekana kichekesho.
 
Kumbe hata hiyo chadema yako huoni ubora wake sasa sijui unapiga kelele za nini? Imarisheni chama chenu kiwe bora sio kutwa kuimba wimbo wa ccm kutegemea dola mara sijui ccm imechokwa halafu hapo hapo mnashindana kwa nyomi.

Kuwa CCM inategemea vyombo vya dola wala hilo halihitaji mjadala. CDM haiwezi kuwa bora iwapo bado katiba inatoa mwanya kwa chama kilichochoka kupanga nchi iendeshwe vipi.
 
Ni kweli, lakini sio kufuata hao wazee uliosema wala hawaijui CDM. Naona propaganda mfu za CCM zimekupoteza, na sasa unazitumia kujenga hoja zako hadi unaonekana kichekesho.
No,

Sina upande ndomana unaweza niona hivyo,

CCM naiombea ife haraka iwezekanavyo, Bt napoangalia vyama vyenye uwezo wa kuiua CCM haviko serious napata hasira zaidi.

CDM naikubali na kuipenda ndomana naisema iongeze ubora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…