Mimi sijakuuliza kuhusu chadema bali nakuhabarisha kuwa chadema hadi sasa hakina mbadala wa Mbowe.Sasa mimi sio msemaji wa CDM, ni wazi ukiniuliza mimi nitakupa maoni yangu sio ya CDM. Sina popote nakubaliana na kiongozi yoyote kukaa madarakani zaidi ya miaka 10, ikiwemo huyo Mbowe. Hao wanaoamini kwa Mbowe nenda ukawaulize wao.
Onyesha popote tunapokubaliana na wizi, 2020 haukuwa wizi bali uporaji wa mchakato.
Usitake kuwafanya viongozi wa chadema ni wapumbavu kwamba wewe ndio unajua sana kuliko wao, wao wameona wakichanganya nguvu ya chadema na kukubalika kwa Lowassa kutaongeza nguvu na kweli tumeona ongezeko la idadi ya kura halafu wewe unasema ni uongo.
Mimi sijakuuliza kuhusu chadema bali nakuhabarisha kuwa chadema hadi sasa hakina mbadala wa Mbowe.
Nguvu kubwa inatumika kuusema uchaguzi wa 2020 kiasi kwamba kwa mtu mgeni anaweza kufikiri chaguzi za nyuma zilikuwa shwari ndio maana unasema haukuwa wizi(ambao mlishauzoea) bali ni uporaji wa mchakato.
Wewe unaleta ubishi tu, nimekwambia chadema kama chama kina nguvu yake na Lowassa ana nguvu yake wameunganisha hizo nguvu. Sasa unaponitajia TLP na Chauma inaonesha hautaki kuelewa.Ww kwako viongozi ni watu wenye akili sana, hivyo wakisema au kufanya lolote wako sawa. Kama ww uko hivyo, mimi siko hivyo. Kuongezeka kwa kura lilikuwa ni jambo lisilokwepeka kwa CDM. Huyo Lowassa angeenda kupandisha kura za TLP au Chauma.
Wewe unaleta ubishi tu, nimekwambia chadema kama chama kina nguvu yake na Lowassa ana nguvu yake wameunganisha hizo nguvu. Sasa unaponitajia TLP na Chauma inaonesha hautaki kuelewa.
Kama viongozi wa chama ambao wanayajua ya ndani ya chama kuliko wewe wanaona uhitaji wa kuvuta watu kutoka upande wa pili ili kuongeza nguvu ila wewe uliyo nje kabisa ndio unajifanya unajua sana kuliko wao tena bila hoja zozote.
Chadema haiwezi kuitoa CCM madarakani, kama nyie wananchi hamtoi ushiriakiano.Kila nikimsikia mwana CHADEMA simsikii akinipa mikakati yenu ya kuitoa (kuing'oa) CCM madarakani bali nasikia tu wakijisifia kujaza watu (nyomi) katika mikutano yao huko mkoani/mikoani.
Nilishawahi kuwashaurini huko nyuma kuwa jiimarisheni sana katika kujijenga ngazi za chini ila nasikitika hili hamjalifanyia kazi na mnambwelambwela tu huku mkitafuta umaarufu na uungwaji mkono na Watanzania walioko mijini na wale wa mitandaoni wakati tafiti zinasema 85% ya wapiga kura wako vijijini.
Kwa Upuuzi wenu huu wa kila mwana CHADEMA kujisifia kujaza watu badala ya kuja na mikakati kabambe kupambana na kuitoa CCM,niwahakikishieni CCM iliyosheheni mafundi wa siasa na mikakati itaendelea kuitawala/kutawala Tanzania hata kwa miaka milioni 100 ijayo.