kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Haki za wanawake: Dunia inafanya majaribio (pilot study) kuhusu wanawake (women empowerment) kushika nafasi kubwa duniani. Dunia nzima inawaona chadema (wanaume) kama vile wanachukua advantage kwa Rais kuwa mwanamke wakidhani kuwa wanawake ni dhaifu kuliko wanaume. Walitumia watu dhaifu sana kama mange, mzee warioba, malisa, dini kufanikisha jambo lao huku wao wenyewe wakijificha kwenye shamba la karanga wasionekane.
Vipaumbele vya dunia: masikio, macho, akili na vipaumbele vya dunia sasa hivi ni Ukrane, Urusi, Israel, Palestine, Sudan, DRC na Venezuela; sio Tanzania. Matukio yanayotokea tz sio habari ya maana kidunia. Walitua njia duni sana kutaka kulivusha jambo lao kimataifa, lakini waliambulia patupu. Halikupata nafasi kidunia, waliishia kuhatarisha maisha ya vijana wasiokuwa na hatia wala maslahi na jambo lao.
Kuvuka redlines: Samia hakuwa mbaya kwenye haki za binadamu na demokrasia kwa watu wake kuliko watangulizi wake JPM, JK, Mkapa, Mzee Mwinyi wala Nyerere. Anatumia Katiba na sheria zilezile kama watangulizi wake. Hajazuia haki za wazungu kuwekeza au wala kuwazuia wazungu kupora rasilimali zetu. hali imebaki ileile kama zamani (status quo) kwa watanzania na wageni. Hakuna mstari mwekundu wowote umevukwa kitaifa na kimataifa. Walitumia wahuni binafsi kuonyesha kuna mauaji ya kutisha.
Demokrasia na haki finyu Tanzania: Inafahamika kidunia kuwa Demokrasia na haki kwenye taifa letu na afrika bado ni changa sana. Demokrasia na haki lazima vionekane hata kwenye ngazi ya kifamilia, jamii, taasisi kama mashule, nk kabla ya kuonekana kwenye ngazi ya serikali kuu. Hadi sasa Tanzania tunayo makabila ambayo watoto wao wa kike wananyimwa haki ya kumiliki ardhi ya familia, lakini makabila hayohayo yanadai haki pana serikali kuu, haingii akilini. Kuna makabila yanapiga wake zao lakini yako mbele kudai haki na demokrasia serikali kuu. Jamii yetu haina haki na demokrasia pana kama ilivyo kwa nchi za Magharibi, hivyo ni vigumu kuiona haki na demokrasia pana kwenye serikali kama ilivyo kwa serikali za nchi za Magharibi. Dunia inapuuza vilio vya haki na demokrasia pana Afrika.
Mambo yote haya yamesababisha kilio cha chadema kuhusu ukosefu wa haki na demokrasia kwenye ngazi ya dunia kuonekana kama mzaha wa watoto. Kiwango chetu cha ukosefu wa haki na demokrasia tz bado ni himilivu sana kidunia kulinganisha na kinachotokea Ukrane, Urusi, Israel, Palestine, Sudan, DRC, Yemen, Somalia, Venezuela, Kashmir, Lebanon, nk. Hata mitaji ya nchi za Magharibi na wafanyakazi wa mashirika ya umoja wa mataifa wanaonekana wako salama zaidi Tanzania kuliko nchi nyingi za Afrika. Yani kama ungekuwa mchezo wa mpira wa miguu chadema wangeonekana kama vile wamemhadaa refa kwa kujiangusha kwenye kisanduku cha penati. Ndiyo maana sio UN wala AU waliotilia maanani jambo lao la uchaguzi na mauaji.
Warudi wakajipange upya.