CHADEMA haya mnayoyafanya ndio yalipelekea tukaletewa Hayati Magufuli

CHADEMA haya mnayoyafanya ndio yalipelekea tukaletewa Hayati Magufuli

Agenda ya Katiba mpya ni ya muhumu sana,lakini anayedai Katiba Mpya hana nia njema yaani anataka kutumia hiyo Katiba mpya kupata madaraka. Na anayeyekataa Katiba hana nia njema anataka kutumia Katiba iliyopo kubaki madarakani. Tatizo hili ndiyo lilivuruga mchakato wa Katiba mpya wakati wa JK.

Yule mzee JK alikuwa na nia njema kabisa akitoka madarakani awe ametuachia Katiba iliyobora lakini wanasiasa wa CCM na Upinzani(UKAWA) wakavuruga ule mchakato kwa sababu ya kupigania maslahi yao badala ya maslahi ya nchi.

Mama tokea mwanzo akiongea tu unaona nia yake ya kutuachia Katiba iliyobora kabisa lakini CCM na Upinzani (CHADEMA) watamvuraga kama walivyomvuruga JK na hakuna Katiba itakayopatika sana sana tutaiingiza nchi kwenye vurugu za kisiasa kwa maslahi ya wanasiasa.

Wanasiasa wa CCM na Upinzani acheni upumbavu wenu,wenye akili tunawachora lakini wapumbavu akina Mdude Nyagali na Sabaya watatumika kutuletea vurugu zisizo na msingi.
Umeongea ukweli mtupu..Wanasiasa wana maslahi binafsi na katiba
 
Wewe ndio mtu, kabla ya kuahidi kuingia barabarani mngekuja na sera ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kanuni mbovu zilizo kwenye katiba iliyopo, wananchi wangedai katiba wenyewe hata kama Mwenyekiti angerudi dubei...ila sio kumpiga mikwara Rais wetu na kuchallenge amani yetu.
Yote hayo unayosema yameishasemwa sana. Hamna mtu anayempiga mkwara Mwenyekiti wenu. Wanamwambia ukweli wao na hamna heshima kubwa kama mtu kukuambia ukweli hata kama utakuuma. Vurugu zinatokea pale watu wanaponyimwa haki yao ya kuwa na mawazo mbadala. Kwa sababu hiyo lawama zote zitakuwa kwenu kama vurugu zitatokea.

Amandla...
 
Mngefurahi sana kama Chadema wangekuwa kama TLP. Mtasubiri sana.

Amandla...

CDM kuwa kama TLP ni suala la muda tu...mabosi wa mwenyekiti ukifika wakati wa kukifanya kiwe kama TLP watakifanya tu hakuna wakuwazuia..
 
Wabadili kwanza katiba ya chama chao ambacho m/kiti ni kama yule wa jirani na Bukoba na makamu wake yupo kusiko julikana anapayuko payuka tu, Tupe raha mama nchi inaenda kuwa ya asali na maziwa waliopo nje ya nchi tunawaambia nyumbani kumenoga.
Kwa miaka minne tumeambiwa kuwa nchi inaelekea kuwa ya asali na maziwa na mwaka wa mwisho tulia bila tuko mlangoni tunasubiri kufunguliwa. Leo hao hao wanawaambia nchi hiyo iko mbali sana na wanahitaji muda wa kuitafuta na nyie bado mnashangilia!

Amandla...
 
CDM kuwa kama TLP ni suala la muda tu...mabosi wa mwenyekiti ukifika wakati wa kukifanya kiwe kama TLP watakifanya tu hakuna wakuwazuia..
Yale yale ya fisi kusubiri mkono uanguke. Kwa mambo yote ambayo CDM imepitia saa hizi wangeishakuwa TLP.

Amandla...
 
Kwa miaka minne tumeambiwa kuwa nchi inaelekea kuwa ya asali na maziwa na mwaka wa mwisho tulia bila tuko mlangoni tunasubiri kufunguliwa. Leo hao hao wanawaambia nchi hiyo iko mbali sana na wanahitaji muda wa kuitafuta na nyie bado mnashangilia!

Amandla...
Mbona hiyo miaka minne hamkuingia barabarani, sana sana mlikimbia nchi...sasa ndani ya miezi mitatu ndo mnaanza mikwara.
#Tunampamudamama.
 
Mbona hiyo miaka minne hamkuingia barabarani, sana sana mlikimbia nchi...sasa ndani ya miezi mitatu ndo mnaanza mikwara.
#Tunampamudamama.
Kwani wameingia barabarani? Kwani wameanza leo kuzungumzia kuingia barabarani? Nyie si mnajua jinsi mlivyokuwa mkiwashughulikia kila wakisema wataingia barabarani? Sasa kwa nini mnapanic safari hii wakati nyenzo za kuwashughulikia bado mnazo? Si mngoje waingie barabarani muwafanyie mlivyozoea? Mikwara yote ya nini? Mmeingia uoga mpaka kitchen party ya Bawacha inawaogofya! Au mnajua waliobaki Chadema hawawaogopi?

Amandla...
 
1. Wanaodai Katiba Mpya mioyoni ni wengi kuliko wanaoidai waziwazi.

2. Kama Wanaotaka Katiba Mpya ni wachache, basi nao waheshimiwe kabla hawajawa wengi. Prof. Kabudi alitushauri kwa hekima juu ya hatari ya kusubiri wawe wengi.

3. Katiba Mpya ikicheleweshwa, yanaweza kuibuka madai mengine magumu yasiyoweza kutatuliwa na katiba ya sasa.

4. Udhaifu wa katiba tuliyo nayo haujabadilika. Waliobadili msimamo ni baadhi ya watendaji. Hata hao, mchana wanasema katiba hii haina tatizo, usiku wanasema haifai tena. Ipo siku usiku utabaki tuuu bila mchana kuja.

5. Kukubalika (Legitimacy) ni kikwazo cha katiba mpya. Tuna Viongozi wengi wasiokubalika na kuaminika na vyama vyao, majimbo yao, hata na umma kwa ujumla. Bila "Legitimacy" watu wanaishi kwa kumtegemea mtawala Mkuu.

6. Rais ni mtumishi wetu. Ni mpangaji (tenant), si mwenye nyumba (Landlord). Tusimtwishe jukumu lisilo lake. Yeye ni Mwenyekiti wa mjadala katika sakata hili. Taifa lisilojadili limekufa kimaono.
Naomba rekebisha sio takwa la wananchi ni takwa la wanasiasa, wananchi tumempa muda mama, hitaji letu kwa sasa ni kuboreshewa uchumi wetu.
Mngekuwa na nia ya dhati mngetuorganize wananchi tuingie barabarani wakati ule mnaona Magufuli anavunja katiba lakini mlikimbilia dubei..,mlitukimbia. Leo tumepoa, tuna matumaini ndo mnaanza kelele, tena wakati ambao mama kutuomba tumpe muda atafute posho za kuwalipa wakati wa kuandaa hiyo katiba...hatuwaelewi
 
Kwamba?

"Maza atafanya kama Rwanda, Uganda, China nk yaani ugomvi uwe kwenye siasa sio kwenye uchumi"

Huko kote wanauwa watu kukariri na kwa kuwahisi tu.

Mama kama hajawatuma kuja kumsemea kuwa ni mwuaji kuliko majambazi, tafadhali fungeni midomo yenu!
Ndio muwe na adabu,anaweza fanya na akasefugadi maslahi ya wazungu na maisha yakaenda kama Kawa nyie mkabaki mnalia Lia hovyo kama watoto wa nguruwe.

Mkiambiwa tulieni kwanza eleweni
 
Amani iwe nanyi nyote..

Naomba niwakumbushe udugu wangu chadema, awamu ya nne mlipiga sana kelele kuwa kuna ufisadi, nchi haikuwa na Rais tunahitaji Rais Dikteta naomba niseme ukweli niliungana na CHADEMA, na katika uchaguzi niliisaidia kweli kweli kwa mapenzi ya kutoka moyoni

Mungu si Athumani tukaletewa jiwe, mwamba kweli kweli, ghafla tukashuhudia hakuna uhuru wa habari! utekaji kila kona, watumishi wakapauka na nataka niseme ukweli kura nilimpa Lissu na nilimpambania hadi kwa ndugu zangu.

Ila Mungu si mzee Hassan katikati ya giza katuletea mama, msikivu ndani ya miezi mitatu nyoyo zimetua, matumaini yamefufuka.

Mama msema kweli katwambia uchumi wetu umeyumba tupige kazi tuukuze, leo mnataka kuleta ngebe, ndani ya miezi mitatu mnataka katiba, hii ni sawa na kuoa mke kisha ndani ya mwezi unamdai mtoto hata mimba huchukua miezi 9 kuzaliwa.

Hayo mnayoyafanya ndo yalisababisha tuletewe jiwe, safari hii hatukubali, tutaenda taratibu na mama.
Tuambie kwaza KAZI YA KUJENGA UCHUMI INA MWISHO?
 
Rais Mkapa ..Chadema Mwenyekiti Mbowe
Rasi Kikwete Chadema Mwenyekiti Mbowe
Rais Magufuli Chadema Mwenyekiti Mbowe
Rais Samia Chadema Mwenyekiti Mbowe.

Huoni tatizo lilipo?

Mwenyekiti kachoka Hana mbinu mpya
Anajaribu old stunts kubaki relevant

Wakati wananchi baada ya miaka 5 ya Jiwe
Hawana interest kabisa na 'confrontational politics'..

Chadema ni outdated ...labda wamlete Malisa
Aje kuwa Mwenyekiti ataweza zungumza kitu
Watu wakamuelewa..hata Samia anamheshimu Malisa kuliko Mbowe..

Wanatakiwa kuji brand upya
Nusu ya watanzania ni under 25 years old..
Wao bado wanafikiri huu ni ni mwaka 1995..

Nikeshangaa hata muanzisha thread huna kawaida ya kuanzisha thread hapa but still wale misukule ya Mbowe itakuja kukushambulia bila ku tafakari
Duh, we jamaa umeongea kitu wasipokusikia na kukuelewa hao watu basi bana! Yaani watu wengine hawalewi kabisa, mtu kama mimi 2003 sikuwa na interest kabisa na mambo ya politics, na you can't imagine watu walioniinspire nikaingia kwenye politics ni watu wa Chadema. Enzi hizo nikiwa UDSM nilimpigia kura Mnyika alipogombea Ubungo dhidi ya Keenja, na nikampa kura Mbowe urais dhidi ya Kikwete.

Hawa jamaa tunapowaambia kwamba politics zao hazivutii kwa sasa hubaki wanawaza kwamba kila anayewacriticize ni CCM (wao huwaita maccm). Ngoja nirudie tena labda wataelewa: Mbowe hana jipya tena kwa sasa, halafu politics za Chadema za sasa zina mapungufu mengi kiasi kwamba mtu unabaki kujiuliza hivi hawa ndio waitoe CCM madarakani? Glimpse chache ni baadhi ya campaign promises za mgombea wao wa urais 2020, mfano kuweka natural resources za nchi kama bond ili tupate fedha kutoka Ulaya na Marekani. Really? Kitu ambacho hata mtoto mdogo anaona wazi wazi tu kwamba huo ni utoto!
 
Kwani wameingia barabarani? Kwani wameanza leo kuzungumzia kuingia barabarani? Nyie si mnajua jinsi mlivyokuwa mkiwashughulikia kila wakisema wataingia barabarani? Sasa kwa nini mnapanic safari hii wakati nyenzo za kuwashughulikia bado mnazo? Si mngoje waingie barabarani muwafanyie mlivyozoea? Mikwara yote ya nini? Mmeingia uoga mpaka kitchen party ya Bawacha inawaogofya! Au mnajua waliobaki Chadema hawawaogopi?

Amandla...
Hatutaki muingie barabarani mpigwe virungu, sisi ni ndugu mtatupa kazi ya kuwauguza.
 
Tokea nizaliwe sijawahi kusapoti CCM na Kura miaka yote nawapigia chadema Ila Kwa kitendo chao cha kishamba eti tuingie barabaran kudai katiba mpya ni UJINGA mtupu!

mbinu za kizamani Sana hizi za kuhamasisha Fujo angalia maneno ya mdude juzi hayana hata adabu ameshindwa kukumbuka kuwa raisi Samia kamtoa jela(shukrani ya punda kabisa hii).

sijawahi kuponda chama changu hata siku moja Ila Kwa hili tukio la mbowe nimeanza kuwachoka wapinzani na nahisi huu ndiyo mwanzo wangu wa kukataa mambo ya vyama
Muwe kama msumeno mnakata pande zote,hata mama anakosea lazima kukaa na viongozi wa vyama kama wanasisa waongelee hizi Shauku za kisiasa, anaweza akawa namalengo mazuri kupitia kukutana wanasisa nakujadili mambo ya kisiasa kutaleta utulivu
 
Huyu mwamba kidogo kanishawishi! Nahitaji point kama hizi sio kelele za Aikael na genge lake la wahuni!

Katiba ni yetu sisi wananchi.

Hatutaki kibambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka sepatation of power ya mhimili, tunataka usawa, uwajibikaji, mawazo yetu kusikilizwa nk.

Vipi mtu asiyatake hayo? Labda tu haelewi au ni mnufaika wa katiba fyongo iliyopo.
 
Back
Top Bottom