CHADEMA haya mnayoyafanya ndio yalipelekea tukaletewa Hayati Magufuli

Umeongea ukweli mtupu..Wanasiasa wana maslahi binafsi na katiba
 
Yote hayo unayosema yameishasemwa sana. Hamna mtu anayempiga mkwara Mwenyekiti wenu. Wanamwambia ukweli wao na hamna heshima kubwa kama mtu kukuambia ukweli hata kama utakuuma. Vurugu zinatokea pale watu wanaponyimwa haki yao ya kuwa na mawazo mbadala. Kwa sababu hiyo lawama zote zitakuwa kwenu kama vurugu zitatokea.

Amandla...
 
Mngefurahi sana kama Chadema wangekuwa kama TLP. Mtasubiri sana.

Amandla...

CDM kuwa kama TLP ni suala la muda tu...mabosi wa mwenyekiti ukifika wakati wa kukifanya kiwe kama TLP watakifanya tu hakuna wakuwazuia..
 
Wabadili kwanza katiba ya chama chao ambacho m/kiti ni kama yule wa jirani na Bukoba na makamu wake yupo kusiko julikana anapayuko payuka tu, Tupe raha mama nchi inaenda kuwa ya asali na maziwa waliopo nje ya nchi tunawaambia nyumbani kumenoga.
Kwa miaka minne tumeambiwa kuwa nchi inaelekea kuwa ya asali na maziwa na mwaka wa mwisho tulia bila tuko mlangoni tunasubiri kufunguliwa. Leo hao hao wanawaambia nchi hiyo iko mbali sana na wanahitaji muda wa kuitafuta na nyie bado mnashangilia!

Amandla...
 
CDM kuwa kama TLP ni suala la muda tu...mabosi wa mwenyekiti ukifika wakati wa kukifanya kiwe kama TLP watakifanya tu hakuna wakuwazuia..
Yale yale ya fisi kusubiri mkono uanguke. Kwa mambo yote ambayo CDM imepitia saa hizi wangeishakuwa TLP.

Amandla...
 
Mbona hiyo miaka minne hamkuingia barabarani, sana sana mlikimbia nchi...sasa ndani ya miezi mitatu ndo mnaanza mikwara.
#Tunampamudamama.
 
Mbona hiyo miaka minne hamkuingia barabarani, sana sana mlikimbia nchi...sasa ndani ya miezi mitatu ndo mnaanza mikwara.
#Tunampamudamama.
Kwani wameingia barabarani? Kwani wameanza leo kuzungumzia kuingia barabarani? Nyie si mnajua jinsi mlivyokuwa mkiwashughulikia kila wakisema wataingia barabarani? Sasa kwa nini mnapanic safari hii wakati nyenzo za kuwashughulikia bado mnazo? Si mngoje waingie barabarani muwafanyie mlivyozoea? Mikwara yote ya nini? Mmeingia uoga mpaka kitchen party ya Bawacha inawaogofya! Au mnajua waliobaki Chadema hawawaogopi?

Amandla...
 
1. Wanaodai Katiba Mpya mioyoni ni wengi kuliko wanaoidai waziwazi.

2. Kama Wanaotaka Katiba Mpya ni wachache, basi nao waheshimiwe kabla hawajawa wengi. Prof. Kabudi alitushauri kwa hekima juu ya hatari ya kusubiri wawe wengi.

3. Katiba Mpya ikicheleweshwa, yanaweza kuibuka madai mengine magumu yasiyoweza kutatuliwa na katiba ya sasa.

4. Udhaifu wa katiba tuliyo nayo haujabadilika. Waliobadili msimamo ni baadhi ya watendaji. Hata hao, mchana wanasema katiba hii haina tatizo, usiku wanasema haifai tena. Ipo siku usiku utabaki tuuu bila mchana kuja.

5. Kukubalika (Legitimacy) ni kikwazo cha katiba mpya. Tuna Viongozi wengi wasiokubalika na kuaminika na vyama vyao, majimbo yao, hata na umma kwa ujumla. Bila "Legitimacy" watu wanaishi kwa kumtegemea mtawala Mkuu.

6. Rais ni mtumishi wetu. Ni mpangaji (tenant), si mwenye nyumba (Landlord). Tusimtwishe jukumu lisilo lake. Yeye ni Mwenyekiti wa mjadala katika sakata hili. Taifa lisilojadili limekufa kimaono.
 
Ndio muwe na adabu,anaweza fanya na akasefugadi maslahi ya wazungu na maisha yakaenda kama Kawa nyie mkabaki mnalia Lia hovyo kama watoto wa nguruwe.

Mkiambiwa tulieni kwanza eleweni
 
Tuambie kwaza KAZI YA KUJENGA UCHUMI INA MWISHO?
 
Duh, we jamaa umeongea kitu wasipokusikia na kukuelewa hao watu basi bana! Yaani watu wengine hawalewi kabisa, mtu kama mimi 2003 sikuwa na interest kabisa na mambo ya politics, na you can't imagine watu walioniinspire nikaingia kwenye politics ni watu wa Chadema. Enzi hizo nikiwa UDSM nilimpigia kura Mnyika alipogombea Ubungo dhidi ya Keenja, na nikampa kura Mbowe urais dhidi ya Kikwete.

Hawa jamaa tunapowaambia kwamba politics zao hazivutii kwa sasa hubaki wanawaza kwamba kila anayewacriticize ni CCM (wao huwaita maccm). Ngoja nirudie tena labda wataelewa: Mbowe hana jipya tena kwa sasa, halafu politics za Chadema za sasa zina mapungufu mengi kiasi kwamba mtu unabaki kujiuliza hivi hawa ndio waitoe CCM madarakani? Glimpse chache ni baadhi ya campaign promises za mgombea wao wa urais 2020, mfano kuweka natural resources za nchi kama bond ili tupate fedha kutoka Ulaya na Marekani. Really? Kitu ambacho hata mtoto mdogo anaona wazi wazi tu kwamba huo ni utoto!
 
Hatutaki muingie barabarani mpigwe virungu, sisi ni ndugu mtatupa kazi ya kuwauguza.
 
Muwe kama msumeno mnakata pande zote,hata mama anakosea lazima kukaa na viongozi wa vyama kama wanasisa waongelee hizi Shauku za kisiasa, anaweza akawa namalengo mazuri kupitia kukutana wanasisa nakujadili mambo ya kisiasa kutaleta utulivu
 
Huyu mwamba kidogo kanishawishi! Nahitaji point kama hizi sio kelele za Aikael na genge lake la wahuni!

Katiba ni yetu sisi wananchi.

Hatutaki kibambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka sepatation of power ya mhimili, tunataka usawa, uwajibikaji, mawazo yetu kusikilizwa nk.

Vipi mtu asiyatake hayo? Labda tu haelewi au ni mnufaika wa katiba fyongo iliyopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…