CHADEMA iandae Mgombea Urais Mwanamke 2025 kuepuka ukatili wa kijinsia

CHADEMA iandae Mgombea Urais Mwanamke 2025 kuepuka ukatili wa kijinsia

Mama akituletea katiba ya Warioba inabidi tuifanyie marekebisho ili tuwe na Malkia kama Uingereza.
Mama Samia akiimarisha Utawala bora ,katiba ya warioba, Uhuru wa kutoa maoni ,Uhuru wa vyombo vya habari,haki sawa kwa wote ,Uhuru wa vyama vya siasa na tume huru ya Uchaguzi, usawa, haki za binadamu , kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma . Hakika mama huyu Samia Hasani Suluhu atafaa kuwa Malkia wa Tanzania.
Zanzibar tutachagua Rais wa SMZ na Tanganyika tutamchagua waziri Mkuu basi. Rais wa Muungano atakua ndiye amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya Ulinzi na usalama ambayo yatasimamia usalama wa nchi sio vyama kama ilivyo. Malkia atakua hana Chama.
Mama Samia atuletee uhuru ,haki na maendeleo ya watu chini ya Katiba Mpya.
Atakua Malkia kweli kweli na Katiba tutaiweka sawa tu .
Uingereza wana akili sana kumweka Mama awe ndiye mkuu wa nchi . Mama ni mama. Wanaume wanafurahia matatizo ya watu kwa manufaa binafsi. Mipango mizuri ya Nchi itafanyika bila tamaa waliyo nayo wanasiasa wanaume hasa kwenye nafasi ya Urais.

Madini ,Mafuta, ardhi, Mali asili za wanyama n.k zitasimamiwa na Malkia watekelezaji watakua ni Rais wa Zanzibar na waziri mkuu wa Tanganyika ambao hao mmoja atakua ni makamu wa kwanza wa Rais na wapili atakua makamu wa pili wa Rais.
Vyama vya siasa vitaweka wagombea kwenye Ubunge na wale wa wakilishi wa mikoa kwa ajili ya Bunge la jamhuri.

Naona dalili nzuri ya kidemokrasia na kisiasa chini ya utawala wa mama Samia.
Tumuunge mkono bila kujali vyama vyetu.

Mbowe sio gaidi ila amebambikiwa kesi kwa manufaa ya majizi ya mali za umma na waroho wa madaraka .

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Baada ya Mama 'kutangaza' nia yake ya kuingia ulingoni 2025, ni vema chama kikuu cha upinzani kikaanza jitihada za kumtengeneza mwanamke atakayepambana na Chifu Hangaya kuwania kiti namba moja hapa nchini.

Kuweka mgombea mwanaume itakuwa ni ukatili wa kijinsia na hoja hiyo itatumika kuwaangusha.
Halafu Mbowe agombee nini?
 
Sijapinga usawa wa kijinsia.Napinga Samia kusema kuwa atagombea urais mwaka 2025 kwa sababu yeye ni mwanamke.

Kutafuta uhalali wa kisiasa kwa kutumia maumbile yako ni ubaguzi. Mtu anatakiwa kugombea urais kwa sababu ya uwezo wake na wala siyo kwa sababu ya dini yake,jinsia yake,ukabila wake au rangi yake.

Usawa wa kijinsia siyo kumpa mtu uongozi kwa sababu ya jinsia yake bali ni kuwapa uongozi watu wenye uwezo bila ya kupendelea jinsia zao.
Huwa nasononeka sana mama akijificha kwwnye jinsia as if ndo aliyoitumia kufika hapo alipo,, SAMIA RAIS WANGU JIAMINI UAMINIWE.
 
Usawa wa kijinsia ni agenda ya kidunia. Tumuunge mkono mama kuhakikisha 50/50 inapatikana haraka

Sio kwa mipasho ile. Hiyo 50/50 itaishia kujaza watoto wa mjini kwenye cabinet. Halafu itakuwa mambo ya kupambana na “vigazeti” kila siku.
 
Marekani baada ya uchaguzi wagombea wanakula dinner pamoja, Tanzania baada ya uchaguzi aliyeshinda anamuinda aliyeshindwa amuue.
 
Hayo ya chama cha mtu binafsi ni kwa wenye UFINYU WA AKILI tu. Mtu binafsi yupi anaweza kuwepo lupango na ndani ya wiki moja Chadema ikachangiwa 350 million ili kulipa faini za Viongozi wa chama.
Hakuna golden chance without a new constitution and Free electoral commission. HAKUNA!
Mkuu, chadema inahitaji kufanya changes kubwa kutoka kuwa chama cha mtu binafsi/kabila na kuwa chama cha ukombozi wa wananchi wote jumuishi. Ikiwezekana hata u-turn kama ya kipindi kile(2015) inahijika kuwaondoa CCM.

2025 ni golden chance ambayo never come twice, ikishindikana ndo basi tena CCM haitaondolewa kwa amani labda mapanga yahusike.
 
Kwani maccm wana hati miliki ya Tanzania mpaka wagomee Katiba mpya? Back up ya kutosha ipi Rena zaidi ya ushiriki wa Watanzania kutoa maoni kuhusu Katiba mpya kupitia Tume ya Warioba maoni ambayo yalizaa Rasimu ya Warioba? Kwanini tena maccm yaturudishe nyuma kwa sababu yanajua Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ni KIAMA chao? 😳

Sasa mkuu, unategemea CCM kukupatia katiba na tume huru bila kuwa na backup ya kutosha ya wananchi, Kumbuka chief wa machief katangaza nia.
 
Back
Top Bottom