Nilitaraji Pasco kuja na uzi kama huu, nilichokigundua kwako wewe ni mmoja ya watu ambao bila kujijua ni wale ambao mnapenda sheria zifanye kazi kutokana na vionjo vya watawala na sio sheria. Umesema kweli kwamba katiba ya cdm kuna kifungu kilichomolewa kinyemela na watu wachache mwaka 2006 bila muhtasari kama inavyopaswa, hilo ni kosa la cdm ama msajili wa vyama? Huko kwenye vyama kuna katiba, na iwapo hukubaliani na katiba ya chama husika hakuna anayekufunga miguu. Hamia chama kingine ama ukiona hakuna chenye katiba nzuri basi anzisha chakwako.
Naona hasira yako inafanana na wanaccm wengi kwa leo kuhusu hali iliyoikuta cdm kuhusu mwanachama wake mmoja. Lakini ki ukweli mpaka kufikia leo ni kama tayari hakuwa mwanachama zaidi ya kwamba alikuwa na kadi. Kama yeye huyo unayeona kaonewa na wakati yeye mwenyewe alikuwa hawakubali wenziwe kwamba yeye ni nyota sana, anaweza kwenda pengine kwani hakuna aliyeshika nyota yake. Achia chama kinachoweza kuchukua maamuzi hata kama hayatawafurahisha walio wengi lakini mpaka sasa kwa mujibu wa katiba iliyo kwa msajili ndio iliyotumika.
Nikushauri Pasco, nadhani wewe unaweza kukutana na huyo aliyefukuzwa, mimi namkubali sana kutokana na uwezo wake kwani sina shaka nao. Sisi wengi bado tunaona uwezo na mchango wake, lakini sioni ulazima wa mchango wake autoe akiwa ndani ya cdm wakati hana maelewano mazuri na wenzie, achia mbali ameonewa sijui katiba ya udikteta na nini. Sasa ndio wakati wa yeye kuonyesha ubora wake huko aendako kwani hakuna mchaga, sijui mkristo wa kumbana. Kuliko wewe kuja na post ya jazba ili yeye awe ndani ya cdm. Mwache kijana aende pengine kwani aliona nafasi yake inabanwa sasa aende akachague nafasi huko aendako ili kama hao cdm wanaaibika waaibike vizuri kwa kumkosa yeye. Vinginevyo ndugu yangu unajiaibisha na kujipunguzia heshima yako kwa kumlazimishia mtu mahali asipopata nafasi, au wewe una mpango wa kuua kipaji chake ndo maana unataka abaki cdm?