Pre GE2025 CHADEMA imedhoofika na kunyong'onyea mno kisiasa nchini haina maono tena

Pre GE2025 CHADEMA imedhoofika na kunyong'onyea mno kisiasa nchini haina maono tena

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni dhahiri haina washauri kabisa, haina malengo, mipango, dira wala uelekeo wa kueleweka. Unaweza kusema imebumba.

Hebu check, hakuna wanachama, mashabiki au wakereketwa, wanaojali, wanaostuka wala kutaka kujua kwamba viongozi wao wote waandamizi wa chama chao wametiwa nguvuni na nini kinaendelea kwao.

Ni ndugu, jamaa na marafiki za waliotiwa nguvuni ndio pekee wana sumbuka , wana haha na kuhangaika huko na huko, kutaka walau kujua au kufahamu kulikoni, na kufuatilia kinachoendelea huko mahabusu wanakosota..

Wanachama wao hawana kabisa habari nao, wala hawana muda wa kupoteza nao, wanapambana na shughuli na kazi zao za kila siku za kuwapatia riziki wao na familia zao kama kawaida..

Watu wameichoka chadema, watu hawana tena imani na chadema, watu wameamua kujitenga na chadema inayochochea migawanyiko, fujo, na kulazimisha hata mambo yasiyo na maana wala umuhimu kama vile maandamano...

Wapendwa, haya mambo yanahitaji umakini, hekima na busara sana kuyafanya. Vinginevyo utateseka, utahangaika, utasumbuka na kuhangaisha familia, ndugu, jamaa na marafiki zako bure tu, huku ukiwatesa zaidi watoto na wanafamilia wako nyumbani...

Siasa ni sayansi sio uhalifu au fujo.

Je, hali hii ni uthibitisho ya kwamba chadema is no more?🐒
 
Watanzania walishawapuuza muda mrefu sana CHADEMA baada ya kugundua kuwa ni chama kilichojaa viongozi wasaka Tonge na wachumia tumbo tu.ndio maana kwa sasa watanzania wapo karibu sana katika kufuatilia taarifa za serikali yao na mipango ya serikali yao katika Maisha yao. Wana imani na CCM na wana amini na matumaini Kuwa ndio chama chenye uwezo wa kuwaongoza na kuwaletea maendeleo endelevu
 
Kweli mkuu,

Hata nashangaa kwa nini mnatumia hadi police,,,,,ni kama kupiga bomu mortuary

Wewe uko sahihi sana,

Mshauri Rais awaache wafanye hayo makongamano hawana madhara.
 
Mnaogopa nini

Tutagawana mbao.
hujapewa zakwako kwani gentleman?🐒

Kwan wew uko upande wa chairman Taifa au vice chairman Taifa ili nikuelekeze kwa atakae kupa mbao zako, halafu ulikua wap wakati wenzio wanagawana mbao?

acha kuzubaa sasa 🐒
 
Kama imeshoofika kulikuwa na sababu ya kutumia jeshi lako tanzania nzima kuwazuia vijana? Si mngewaacha tu kama hawana impact....CCM bila dola ni dhaifu sana
ni dhaifu sio dhaifu?🐒
 
Hu rafiki yangu ila sio mda tutagombana , upo na akili kubwa why wajitoa hufaham? Nijibu na usipo nijibu urafiki ufe wa hapa jf japo mwana ccm
gentleman,

hii akili kubwa ambae niko nayo ni kwa manufaa ya wananchi na waTanzania wote kwa ujumla,

na by the way, ni kidogo sana nimetumia hii akili kubwa na halafu mbona huu ni mwanzo sana tu gentleman na vitisho ni kwanini kwenye mambo rahisi na mepesi kama haya?

na tafadhali sana,
nisingependa kuhusika kwa namna yoyote ile katika mauaji ya kitu chochote kile hata kama ni urafiki, samahani sana 🐒
 
gentleman,

hii akili kubwa ambae niko nayo ni kwa manufaa ya wananchi na waTanzania wote kwa ujumla...
Wewe hutakiwi kuwa ccm , ccm huaribu vipaji, na akili za watu wenye akili, njoo chadema au waogopa kamata ya police , 2025 watanyoka kama rula mda mwalim mkuu
 
Kwamba wewe na wenzio huko ccm ndio mnaweza kuassess uhai wa chadema, hebu waulize wale form four failure mnaowaita polis kama chadema is no more.
 
Ni kweli Hadi mnawakamata na kujikosha eti muwaache Tena!
uhalifu wa aina yoyote haupaswi kuvumiliwa wala kufumbiwa macho hasa na Jeshi letu la police ambalo ni la kisasa zaidi 🐒
Kweli mkuu,,,,
Hata nashangaa kwa nini mnatumia hadi police,,,,,ni kama kupiga bomu mortuary….
Wewe uko sahihi sana,,,,,
Mshauri ⏱️100,,,, awaache wafanye hayo makongamano hawana madhara.
Yes,
kwa magenge ya kihalifu ni muhimu kutumia nguvu kuyadhibiti yasisababishe uharibifu, usumbufu na uvunjifu wa amani na utulivu wa wananchi 🐒
 
Ni kweli kabisa lakini cjui kwanini mnawakamata
unazungumzia wahalifu?

ni dhahiri hakuna huruma wala mzaha katika kukubaliana na kudhibiti magenge ya kihalifu popote nchini 🐒

kuhusu siasa,
ndio kama nilivyosema chadema is no more relevant in political scene 🐒
 
Wewe hutakiwi kuwa ccm , ccm huaribu vipaji, na akili za watu wenye akili, njoo chadema au waogopa kamata ya police , 2025 watanyoka kama rula mda mwalim mkuu
nani hanitaki huko CCM ambako siko?🐒

kipawa, akili, utashi, nguvu, uchaji wangu kimwili na kiroho, ni Neema na Baraka za Mungu, nimepewa bure nami nitasaidia wengine bure...

sio CCM, chadema, chauma CUF n.k inaweza kwa namna yoyote kuharibu haiba yangu kwa namna yoyote ile,

ninapopambania wananchi na waTanzania wote, huwa siko pekeyangu, daima niko na Mungu na amenihakikishia kumaliza na kufika salama katika safari yangu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa maslahi mapana ya wananchi 🐒

sina hofu wala woga, nina ujasiri na uhakika wa kufika ninakokwenda, bila police, chadema, CCM ama vinginevyo, don't be confused please 🐒
 
Watanzania walishawapuuza muda mrefu sana CHADEMA baada ya kugundua kuwa ni chama kilichojaa viongozi wasaka Tonge na wachumia tumbo tu.ndio maana kwa sasa watanzania wapo karibu sana katika kufuatilia taarifa za serikali yao na mipango ya serikali yao katika Maisha yao. Wana imani na CCM na wana amini na matumaini Kuwa ndio chama chenye uwezo wa kuwaongoza na kuwaletea maendeleo endelevu
Pwagu na pwaguzi mpo kazinikitetea buku7
 
Back
Top Bottom