Agosti 2024
Mbeya, Tanzania
DKT. MWAKAJUMILO - TUNA UHURU WA BENDERA WATANZANIA TUBADILI MITAZAMO YETU
View: https://m.youtube.com/watch?v=qYReffkC0a8
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Dr. Stephen Laurent Isaac Mwakajumilo MNEC mjumbe halmashauri kuu ya taifa CCM, aliyevuliwa madaraka kwa kutofautiana na chama dola kongwe na kupelekwa kuwa DC wilaya ya Namyumbu kisha nako kutumbuliwa aongea kuhusu uhuru wa bandia yaani wa bendera .... tuna wakoloni weusi baada ya kuondoka wazungu ... afafanua uhuru wa bendera kwa kina ...
DC DR.MWAKAJUMILO ATENGULIWA
By Simba Editor | tokea miezi 2
Na Mwandishi wetu.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya ya Namyumbu Dr Stephen Mwakajumilo.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mwakajumilo alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya.
Utenguzi wa nafasi yake umefanyika Leo June 11,2024
TASWIRA YA WILAYA YA NANYUMBU
Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, ni moja kati ya Halmashauri tisa za mkoa wa Mtwara. Halmashauri hii ilianzishwa chini ya Sheria namba 7 ya mwaka 1982 ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) na kutangazwa rasmi katika Gazeti la Serikali Na. 190 la tarehe 01 Julai 2007. Makao makuu ya Wilaya yapo mji wa Mangaka ambao upo umbali wa kilomita 54 kutoka Masasi kwenye barabara ya Mtwara-Songea.
Asili ya wenyeji wa wilaya ya Nanyumbu ni makabila ya wamakua, wayao, na wamatambwe ambao huzungumza lugha zao za asili pamoja na Kiswahili.
1.2 MIPAKA YA ENEO
Wilaya hii iko kati ya latitudo 360 na 380 mashariki mwa Greenwich na latitudo 100 na 120 kusini mwa Ikweta. Nanyumbu inapakana na wilaya ya Nachingwea upande wa kaskazini, wilaya ya Masasi kwa upande wa mashariki, wilaya ya Tunduru upande wa magharibi na Jamhuri ya Msumbiji kwa upande wa kusini