Uchaguzi 2020 CHADEMA imeomba vyombo husika vifuatilie tetesi za kuwepo mipango ya kuvuruga mchakato wa kuelekea katika hatua za kurudisha fomu

Uchaguzi 2020 CHADEMA imeomba vyombo husika vifuatilie tetesi za kuwepo mipango ya kuvuruga mchakato wa kuelekea katika hatua za kurudisha fomu

Uraia Ni suala mtambuka wewe
Anatory Amani wa ccm alishawahi kupokwa uraia wake katika mazingirq Kama haya ya uchaguzi,Kama uraia wako hauna utata ya nini kujipa presha?
Ndugu haya yanafanyika kwa nia uvu.
 
Bagamoyo
Nimekua nikitazama video mbalimbali za mapokezi ya Lissu,watu wanaompokea Ni maelfu kwa maelfu.
Ila hi ya Songwe nimeitazama mwanzo mwisho,aisee hi naona imevunja rekodi,watu mi wengi Sana.
Sioni Lissu atashindwa Uchaguzi huu.
Nakuhakikishia kuwa,kwa kura za kudumbukiza ndani ya ballot box Lisu atashinda.
Narudia Tena Lissu atashinda.
Naomba tume itende Hali tu.
 
Bagamoyo
Nimekua nikitazama video mbalimbali za mapokezi ya Lissu,watu wanaompokea Ni maelfu kwa maelfu.
Ila hi ya Songwe nimeitazama mwanzo mwisho,aisee hi naona imevunja rekodi,watu mi wengi Sana.
Sioni Lissu atashindwa Uchaguzi huu.
Nakuhakikishia kuwa,kwa kura za kudumbukiza ndani ya ballot box Lisu atashinda.
Narudia Tena Lissu atashinda.
Naomba tume itende Hali tu.
Lisu kwanza anazunguka kwenye majimbo yaliyokuwa na wabunge wa chadema hivyo Ni rahisi kukusanya watu, pili watu wanaenda kumwangalia Kama kweli kawa kilema, Ila wanakatishwa tamaa na kauli zake,
 
Uraia Waweza hojiwa muda wowote kabla 2015 Magufuli hakuwa madarakani rushwa na ufisadi ulikuwa nje nje kaingia kuhoji ruksa Kama mtu raia Hana Cha kuogopa
Magufuli Huyu aliyejifungia juzi dodoma na kupitisha Watoa rushwa wakawe wagombea ubunge ndiyo anapimwa kwa kupambana na ufisadi? Nitajie mgombea wa Ccm ambaye hajatoa RUSHWA nikuwekee hapa na majina na viwango.
 
Aisee acheni kulia lia basi haitowasaidia..Chukueni hatua kama hamuwezi kaeni kimya maisha yaendelee...CDM miaka yote nyie mnalalamika tu mnaonewa kwenye hili lile kila siku, miaka yote..CHUKUENI HATUA KAMA MNA UHAKIKA MKO UPANDE WA HAKI...

Hebu toa ushauri ni hatua ipi ichukuliwe boss, maana hii kulalamika ni hatua moja. Hatua nyingine ndio huyo Lisu kasema iwapo hatapata haki yake hatuamiachia Mungu, na sasa ndio unaona makongamano ya kuiombea nchi iwe na amani, na hao waombea amani ndio hao wanaibrand cdm kama wavuruga amani.
 
Kwa hili lililotokea Tunduma inatakiwa refa mkuu anayesimamia zoezi zima la mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu atoe muongozo kwa nchi nzima jinsi ya vyombo vya dola vifanye kazi yake kipindi hiki.

Kwani Uchaguzi siyo kupiga kura tu bali mchakato wa uchaguzi unaanza pale vyama vinapofanya mikutano miku kupendekeza wapeperusha bendera wao, uchukuaji fomu, kutafuta wadhamini, kupitishwa na Tume, kupiga mikutano ya kampeni na hatimaye wananchi kupiga kura.
 
Lisu kwanza anazunguka kwenye majimbo yaliyokuwa na wabunge wa chadema hivyo Ni rahisi kukusanya watu, pili watu wanaenda kumwangalia Kama kweli kawa kilema, Ila wanakatishwa tamaa na kauli zake,
Mhhuu Eddy watu wanakatishwa tamaa umepata wapi data hizo au wewe umekata tamaa usiwasemee watu.
 
22 August 2020
Tunduma, Songwe
Tanzania



CHADEMA imeomba vyombo husika vifuatilie tetesi za kuwepo mipango ya kuvuruga mchakato wa kuelekea katika hatua za kurudisha fomu za wagombea. Hivyo wameomba uchunguzi na hatua za haraka za kiuchunguzi zifanyike ili kama kweli mipango hiyo ipo basi vyombo husika vilivyoahidi kusimamia uchaguzi huru na haki vizuie njama hizo ovu.

Tayari wagombea kadhaa wa udiwani wa CHADEMA waliohudumu muda mrefu kabla mabaraza ya madiwani hayajavunjwa kufuatia kumalizika kwa kazi zao 2015 -2020 wameitwa kuhojiwa uraia wao.

CHADEMA inashangaa vipi viongozi hao waliohudumu katika Baraza la Madiwani la Halmashauri waanze kuhojiwa kipindi hiki kuelekea mchakato wa kurudisha fomu unaotarajiwa kuhitimishwa tarehe 25 Agosti 2020 ili waweze kuomba kuchaguliwa na wananchi wa Tunduma.

Madiwani teule waliopendekezwa na CHADEMA, mbele ya waandishi wa habari waongea kuhusu kupokea simu zilizopigwa na watu waliojitambulisha ni maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuitwa kwenda kuhojiwa uraia wao. Diwani wa kata ya Sogea Tunduma alihojiwa kwa masaa kadhaa ktk ofisi za Uhamiaji Tunduma na kutakiwa kupeleka viambatisho vya vyeti vya kuzaliwa kesho kutwa Jumatatu tarehe 24 Agosti huku madiwani wengine wa CHADEMA walioshindwa kufika ofisi za Uhamiaji wakiendelea kuombwa kufika ofisi za Uhamiaji.

Viongozi wa CHADEMA Tunduma wanasema hizo ni njama za kutengeneza mazingira madiwani wa CCM wapite bila kupingwa katika uchaguzi wa Oktoba 2020. Kwani mmoja wa wagombea wa udiwani wa CHADEMA aliyeitwa Uhamiaji ana kaka yake ambaye ni mgombea wa udiwani wa CCM lakini huyu wa CCM hajaitwa kuhojiwa uraia.
Source : DSS Tunduma

mpango umekamilika.
wagombea wote wa udiwani CHADEMA wamekamatwa, wakaambiwa siyo raia, baadae wamebadilishiwa mashitaka na kuambiwa "Ujambazi wa milioni saba, kwenye mabano(2,000,000/-)

Yaani Mungu wa Israel kama kweli unaishi, japo ulisha apa hutateketeza dunia kwa moto ila tunakuomba ee Mungu baba, "Shusha Moto wako , tufanye msiba wa Kitaifa"
 
Back
Top Bottom