Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,386
- 5,325
Kama tunavyosherekea wagunduzi wa vitu mbalimbali na kuwapa tuzo, mfano akina Einstein, Tesla basi hapa Tanzania mnamo mwaka 2015 mara baada ya mzee wa nywele nyeupe kuwa mgombea wa chama fulani ambacho kilimtaja kwenye list of shame, hivyo mashabiki wa chama hicho kulazimishwa kumsafisha na kumpigia kampeni ili awe rais na wao wakakubali kwa kufuta list of shame kwenye tovuti ya chama chao na mara moja wakaanza kuzunguka nchi nzima wakiimba kwa kuzungusha mikono kuwa kama mtu huyu angekuwa fisadi kweli basi angefungwa maana yake walikiri kuwa walimsingizia tu!.
Baada ya mkengeuko huo ndipo akajitokeza mgunduzi wa jina la nyumbu akiwafananisha na mnyama nyumbu ambaye hanaga akili ya kufikiri mara mbili pale wanapokatiza mto Mara, hata mto uwe umejaa mamba, nyumbu kiongozi akishajirusha humo basi wote wanaofuatia watajirusha humo na kuliwa.
Leo miaka 5 imepita lakini jina la nyumbu linaendelea kuwafaa wafuasi hawa. Wao kila kitu ni kupinga na kutetea kila aina ya ujinga ili mradi tu huo ujinga umeungwa mkono na kiongozi wao.
Basi napendekeza aliyebuni jina la nyumbu asakwe huko aliko na apewe tuzo.