Uchaguzi 2020 CHADEMA inakuwaje mtu anagombea Kiti cha Ubunge wa Jimbo na Viti Maalumu kwa mpigo na anashinda vyote? Kwanini asigombee moja?

Uchaguzi 2020 CHADEMA inakuwaje mtu anagombea Kiti cha Ubunge wa Jimbo na Viti Maalumu kwa mpigo na anashinda vyote? Kwanini asigombee moja?

Walijaribu huku na kule wasipoteze mkate wao kirahisi, ila aliepata nafasi ya pili ndie atapewa hiyo nafasi ya Viti Maalum, sioni kama kuna ubaya hapo.
Hivi hii ina maana gani sasa ya kupoteza muda kufanya uchaguzi?
 
CHADEMA nakuwaje mtu anagombea viti vyote cha Ubunge wa Jimbo na Viti Maalumu kwa mpigo na anashinda vyote? Kwanini asigombee moja?

Mifano michache ni hii hapa Devota Minja na Grace Kiwelu

MATOKEO YA KURA ZA MAONI JIMBO LA MOROGORO MJINI

1. Jimbo

Idadi ya Wapiga kura 125
Kura zilizoharibika 6

a. DEVOTHA MINJA 83 sawa na 66.4%
b. SHABAN DIMOSO 33 sawa na 26.4%
c. WILFRED NGINDU 2 sawa na 1.6%
c. JUMA TEMBO 1 sawa na 0.8%

VITI MAALUMU
Idadi ya Wapiga Kura 55
Kura zilizoharibika 02

a. DEVOTHA MINJA 38 sawa na 70.3%
b. ESTHER TAWETE 11 sawa na 20%
c. MARIA MIHANJO 4 sawa na 7%
d. DOROTH NAMUNASHI 0 sawa na 0%.

Gwamaka Mbughi
Msimamizi

MATOKEO YA KURA ZA MAONI - JIMBO LA VUNJO (KILIMANJARO)

Ubunge wa Jimbo

Mgombea;
1) Grace Kiwelu Kura 80 =95.23%
2) Peter Msophe 4

UBUNGE Viti Maalum
1) Mh Grace Kiwelu kura 25 = 83.33%
2) Aziza Mohammed 05 =16%
Wacha ujinga mwamba, huko kwingine kukoje? Kwani CCM hawagombei vyote? Acha ujinga aisee huo ni uchaguzi na mtu yuko huru kuchagua vyote. Unafikri uchaguzi wa jimbo ni rahisi unavyofikria?
 
Muulize Mama Salma Kikwete kwanini na yeye Viti Maalum ameomba na huku kwny kinyanganyiro anagombea pia.
giphy.gif
 
Je, kanuni za vyama zinasemaje? Kanuni za Uchaguzi zinasemaje? Kuna Sheria imekiukwa? Kuna kanuni imekiukwa? Kama hakuna kuvunjwa kwa kanuni au sheria basi usilalamikie Chadema wala CCM lalamikia kanuni na Sheria zinazotoa loophole hiyo

Hizo sheria na kanuni zinazoruhusu hayo tusipozikemea zitaendelea. Hivyo hapa ninafanya kitendo sahihi kuhakikisha kuwa sheria zisizofaa zinaondolewa.
 
Inaweza kuwa kweli,kama walifanya mikusanyiko isiyohalali unategemea nini?

Hakuna mikusanyiko isiyo halali, cdm sio chama cha kigaidi, mikutano yake kinafanya mchana kweupe, kila mtu akiwaona. Kinachofanyika ni matumizi mabaya ya madaraka, ili kuwatisha watu kutoshiriki mikutano ya cdm, kisha zipigwe propaganda za kizee kuwa cdm haikubaliki.
 
big up men, hilo jibu limefunga uzi mkuu! ni uroho wa madaraka na kutokujiamini!
Ni kweli hali hii ina ukakasi, na hali hiyo haipo cdm tu, hata ccm ipo. Tabia hii ni kutokujiamini na ni dalili za uchu wa madaraka. Ila tatizo langu kubwa ni mtu kuwa kwenye viti maalum zaidi ya miaka kumi. Hili kwangu ni tatizo kubwa na siko tayari kulivumilia kwa utetezi wa aina yoyote.
 
Je, kanuni za vyama zinasemaje? Kanuni za Uchaguzi zinasemaje? Kuna Sheria imekiukwa? Kuna kanuni imekiukwa? Kama hakuna kuvunjwa kwa kanuni au sheria basi usilalamikie Chadema wala CCM lalamikia kanuni na Sheria zinazotoa loophole hiyo
Hakuna kanuni yoyote iliyovunjwa ndio maana hayo mambo yapo, kama wakiona kuna tatizo labda ndio wakabadilishe kanuni.
 
Kuna watu chadema viti maalumu ni kama walizaliwa navyo hata ile maana ya kuwapa uzoefu imepotea
 
Kwahiyo mama salma yy kajiamini maana naona kachukua fomu anagombania ubunge na kwenye viti maalum pia kagombania
Huyo ndio hajiamini zaidi level yake ya first lady mpaka kwenye hayo matakataka ni kukosa washaur tu bora angefungua darasa!
 
Hakuna mikusanyiko isiyo halali, cdm sio chama cha kigaidi, mikutano yake kinafanya mchana kweupe, kila mtu akiwaona. Kinachofanyika ni matumizi mabaya ya madaraka, ili kuwatisha watu kutoshiriki mikutano ya cdm, kisha zipigwe propaganda za kizee kuwa cdm haikubaliki.
Mikusanyiko halali lazima iwe na kibali cha Officer commanding division. Zaidi ya hapo ni kinyume cha sheria. Na Chadema huwa wanakiuka kwa kujifanya wababe.
 
Mbona wewe unaomba kazi makampuni matano-mia moja kwa wakati mmoja?
 
Mikusanyiko halali lazima iwe na kibali cha Officer commanding division. Zaidi ya hapo ni kinyume cha sheria. Na Chadema huwa wanakiuka kwa kujifanya wababe.

Ndio hapo ninapokuambia matumizi mabaya ya madaraka yanapoanzia. Cdm huwa wanafuata taratibu zote, ila hao polisi huwa wanapewa amri za kuwakatalia kimakusudi, kwa lengo la kuwadhoofisha. Hilo limekuwa likifanyika mara zote kwa nia ovu. Na kwakuwa cdm huwa wanajua kuwa wanafanyiwa Katazo kama hujuma za kisiasa, hawana jinsi zaidi ya kukutana kwa lazima.

Kimsingi haki haiombwi, na iwapo cdm wataendelea kusubiri hao viongozi wa polisi wanaojivunia kuwa wanaccm hadharani, kinyume cha maadili ya kazi, hawatakaa wafanye mikutano. Kwa sasa ccm inategemea vyombo vya dola kwa asilimia mia moja kufanya siasa, na vyombo vya dola vinajiona vina haki ya kuitetea ccm, hiyo ndio inayopelekea cdm kunyimwa haki ya kukutana.
 
Kwa nini hao Ocd's wawakatalie bila sababu? Hizo amri toka juu anazitoa nani? Chadema wana nini kipya mpaka amri zitoke juu kuwazuia? Maana hawana mvuto wala nguvu kama 2010-2015, na walipewa vibali vya mikutano iweje hii leo ambapo wameanguka kifo cha mende wanyimwe vibali.
 
Unaongea nini ww? Hiyo ambayo unasema hawana nguvu imetokana na kunyimwa vibali ya kufanya mikutano. Kwahiyo kwakuwa walikuwa wanapewa vibali huko nyuma, sasa hivi hawawezi kunyimwa, tena kwa sababu ya mikakati ya kisiasa? Hebu kaa kimya maana huna jipya.
 
Back
Top Bottom