Ndio hapo ninapokuambia matumizi mabaya ya madaraka yanapoanzia. Cdm huwa wanafuata taratibu zote, ila hao polisi huwa wanapewa amri za kuwakatalia kimakusudi, kwa lengo la kuwadhoofisha. Hilo limekuwa likifanyika mara zote kwa nia ovu. Na kwakuwa cdm huwa wanajua kuwa wanafanyiwa Katazo kama hujuma za kisiasa, hawana jinsi zaidi ya kukutana kwa lazima.
Kimsingi haki haiombwi, na iwapo cdm wataendelea kusubiri hao viongozi wa polisi wanaojivunia kuwa wanaccm hadharani, kinyume cha maadili ya kazi, hawatakaa wafanye mikutano. Kwa sasa ccm inategemea vyombo vya dola kwa asilimia mia moja kufanya siasa, na vyombo vya dola vinajiona vina haki ya kuitetea ccm, hiyo ndio inayopelekea cdm kunyimwa haki ya kukutana.