CHADEMA inapokea Ruzuku ya Tsh. Millioni 107 kwa mwezi sawa na Tsh. Billion 1 na Millioni 284 Kwa mwaka!

CHADEMA inapokea Ruzuku ya Tsh. Millioni 107 kwa mwezi sawa na Tsh. Billion 1 na Millioni 284 Kwa mwaka!

..kama Ccm ina vyanzo vyote hivyo vya mapato kwanini inatukamua BILLIONI 3 kila mwezi?
Hata ingekuwa inapokea Ruzuku ya Billion kumi ingeendelea kuchukua maana wanayoipatia ni wananchi kwa upendo wao mkubwa kwa CCM,.
 
Mwakani ni mteremko tu na mwendo wa kuzoa kura katika kila ngazi ya uchaguzi.
Kwa njia ya wizi wa kura!
Mkishawadanganya vitenge,kofia na shati za kijani wakiwapigia kura mnawatelekeza!
 

Attachments

  • FB_IMG_1478834455434.jpg
    FB_IMG_1478834455434.jpg
    55.6 KB · Views: 1
Ndugu zangu Watanzania,

Chama kikuu cha upinzani hapa Nchini CHADEMA kinapokea Ruzuku kutoka serikalini ya takribani Millioni 107 kwa Mwezi ambayo ni sawa na Billion 1 na Millioni 284 kwa mwaka. Yaani:

107,000,000 x 12= 1,284,000,000/=.

Ambapo hata hivyo CHADEMA inasema kiasi hicho ni kidogo sana ukilinganisha na mahitaji na matumizi ya chama. Hiyo ni kwa mujibu wa John Mrema ambaye anasema pesa hiyo haitoshi na haiwatoshi.

Anasema ni ndogo kwa sababu chama kina ofisi ya makao makuu Dar es salaam, makao makuu ndogo Zanzibar pamoja na ofisi 10 za kanda ambazo zina waajiriwa rasmi wanaolipwa mishahara.

Swali linalokuja kwangu na ambalo ningependa kuwauliza CHADEMA ni kuwa kama Million 107 kwa mwezi ni ndogo. Je, CHADEMA walitaka walipwe shilingi ngapi ambazo ndio wataona ni nyingi? Mbona wakati wanapokea nyingi hususani 2015-2020 walipokuwa na wabunge wengi napo hawakuwahi kusema kuwa wanapokea nyingi na badala yake tuliona ofisi za chama huku mikoani zikiwa zimechoka sana na hali mbaya sana.

Hali ambayo ilionyesha na kutoa ishara ya kuwa ofisi hizi zilikuwa hazipati pesa au pesa zilikuwa hazifiki katika ofisi hizi. Lakini ikumbukwe kuwa pamoja na kupokea kwake Ruzuku kubwa bado wabunge wake nao walikuwa wakikatwa pesa kila Mwezi kuchangia chama. na ajabu zaidi ikifika wakati wa uchaguzi wagombea wake wa ubunge wamekuwa wakikabiliwa na ukata mkubwa sana wa kifedha na kupelekea kusuasua kwa kampeni.

Lakini pia kama CHADEMA inaona pesa hizo ni ndogo jambo ambalo linaweza kuwa kweli katika kujiendesha kitaasisi. Je, imefanya mikakati gani na mipango gani kuwekeza katika miradi ya chama itakayokiingizia na kukiongezea chama kipato? Miradi ya chama ipo wapi? Kwanini chama hakina miradi wakati kimepokea pesa nyingi sana kwa miaka kadhaa iliyopita?

Ikumbukwe ya kuwa pamoja na kupokea pesa kwa wingi lakini chama hakina hata tu kituo cha Tv au hata redio .yaani CHADEMA nzima inazidiwa maarifa na uthubutu na wasanii kama Diamond aliye na kituo cha Tv pamoja na Redio. Inazidiwa hadi na Millard Ayo.

Unaweza kuona udogo wa mawazo kiliyo nayo chama hiki. Maana jambo kubwa linaanza kujengwa katika fikira kwanza yaani kichwani. Lakini chama hiki cha CHADEMA hakina fikira kubwa kichwani mwake za kujiongezea kipato kupitia miradi na vitega uchumi vyake na badala yake kinategemea kikinge mikono kutoka kwa serikali hii hii ya Jemedari wetu shupavu na imara Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Ili sasa wakalipane mishahara na posho nene nene halafu wanarudi wanasema pesa ni kidogo na wakati mwingine wanaitukana na serikali inayowapa shibe na jeuri. CHADEMA hata wapewe kuongoza nchi kwa wiki moja kazi wanayoweza kuifanya ni kukomba na kukausha pesa zote hazina kama nyasi zilizopigwa dawa ya glamakisoni.

CHADEMA ni chama kisicho na ubunifu wala mikakati wala mbinu, wala njia ya kukiongezea na kutunisha mfuko wa pesa. Na lazima ifahamike ya kuwa siasa inahitaji uchumi ,chama kinahitaji kiwe na misuli ya kiuchumi na kifedha kwasababu huwezi kueneza chama kama huna pesa.

Kama huna pesa utashindwa hata kulipia ofisi wilayani na kwenye kata huko, kama ambavyo tumeshuhudia CHADEMA ikikosa ofisi ngazi hizo na pale ambapo zipo unakuta zimefungwa na kubaki maandishi nje tu, kwa sababu ya kukosa kodi ya nyumba ambayo unakuta ni ndogo tu lakini chama kimeshindwa kulipia, mpaka wenye nyumba wanaamua kuweka makufuri juu ya makufuri.

Naweka kalamu yangu chini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
mradi pekee mkubwa sana na wa kutegemewa wa Chadema ni ule wa aibu na fedheha wa kuomba kuchangiwa pesa , basi!🐒
 
mradi pekee mkubwa sana na wa kutegemewa wa Chadema ni ule wa aibu na fedheha wa kuomba kuchangiwa pesa , basi!🐒
Akipata gari ataanza kuomba tena achangiwe mafuta. Maana CHADEMA wanapenda sana mserereko na walishawaona wafuasi wao hawajitambui.
 
CCM wanapokea sh ngapi? Act wanapokea sh ngapi? Hebu niwekee data kwanza na kazi yake ni Nini kama siyo kulipana posho. Au unadhani hatuwaoni au hatuishi nao? Unapotoa hoja watu wachangie use your common sense.
CCM wanategemea zaidi kwenye kuiba fedha za umma
 
Acha kuichafua CCM Chama imara na kiongozi barani Afrika.
Chama cha matapeli tupu, Mkapa alikiri kuiba bilioni 130 ajili ya uchaguzi wa 2005 tena kwenye kitabu chake, wewe huna akili huwezi kuelewa upo upo tu sababu ya njaa zako na kukosa akili hujui kinachoendelea. Hata Makonda juzi kakiri kuwa wafanyabiashara wanaichangia CCM siyo kwa kupenda kwa lazima. Mjinga sn wewe
 
Akipata gari ataanza kuomba tena achangiwe mafuta. Maana CHADEMA wanapenda sana mserereko na walishawaona wafuasi wao hawajitambui.
yaani jamaa ni watu wa ajabu sana,

hivi kweli kuna mtu anaweza kuchagua kiongozi mwenye tabia na mazoea mabaya ya kuombaomba tu mara kwa mara eti aje kua kiongozi wake kweli?🐒

Labda sio Tanzania...
 
Back
Top Bottom