Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,075
Anatapatapa kuna uzi wake upo jukwaa la katiba anasema watanzania kataeni serikali tatu, hapa Mbowe anataka serikali tatu, wewe unataka serikali ngapi?
Mbona nishasema mara kibao humu. Mi nataka serekali tatu: Serekali ya Tanganyika, serekali ya Unguja na serekali ya Pemba. Serekali tatu ndo jibu la utata wote ulipo hapa Mkuu. Nje ya hapo labda serekali moja naweza kuifikiria. Na hili ndo lilikuwa wazo la Mwanakijiji. Naamini hata chadema wanawaza hilo pia la uwezekano wa serekali moja. Lakini kwa kuwa Wazenji hawataki hilo wazo, dawa ni serekali tatu tu. Tanganyika, Unguja na Pemba. Hiyo nyingine unayoisemasema hapa mi siitaki. Huo ni mwanya wa usumbufu na utapeli kama wa awali tu hapo.