CHADEMA inaunga mkono Rasimu ya Katiba mpya - Mbowe

CHADEMA inaunga mkono Rasimu ya Katiba mpya - Mbowe

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema chama chake kinaunga mkono rasimu ya Katiba mpya iliyotolewa na Jaji Joseph Warioba.

Mwenyekiti huyo alikuwa akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa jiji la Mbeya katika mkutano wa kumnadi mgombea udiwani wa kata ya Iyela kwa tiketi ya Chadema Charles Nkelwa.

Kiongozi huyo wa upinzani bungeni amesema sababu kubwa ya kuunga mkono rasimu hiyo ni kwamba mambo mengi yaliyoorodheshwai na chama hicho yamekubaliwa.

Mbowe amesema jambo kubwa lililofanyiwa kazi ni kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika.Mbowe amesema amesikitika kuona baadhi ya wanaCCM wakiipinga serikali ya Tanganyika na kung'ang'ania serikali mbili na kudai watu hao ni wanafiki wanaopaswa kupuuzwa na wananchi.

Kauli ya Mbowe imekuja wakati ambapo mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Dr Kitila Mkumbo alinukuliwa kusema rasimu mpya ya Katiba iliyotolewa na Warioba ni bora mara mia mbili akilinganisha na katiba ya sasa.

Mara baada ya mkutano huo maelfu ya watu walitanda barabarani kumsindikiza kiongozi huyo anayependwa sana jijini Mbeya.

Source:Mwananchi Jumatatu.
Sijui kama CDM wanajifunza ! hivi hii ni kauli ya Mbowe au ya chama?
Ile ya Kitila ni yake, hii ya Mbowe je? Kwanini kusiwe na taarifa ya chama kuhusu msimamo wa Chadema

Ina maana wao wamekubali kila kitu, kama sivyo kipi wanadhani kiboreshwe kipi kiachwe n.k. na kwanini wanadhani msimamo wao umekidhiwa katika katiba mpya.

Je, tatizo la katiba ililikuwa kurudi kwa Tanganyika? Mambo mangapi ni muhimu sana katika katiba.
Wameridhika na tume ya uchaguzi, wameridhika na mfumo wa mahakama?

Nadhani walitakiwa watoe statement ya chama na si kila mmoja kivyake. Hivi akiibuka mwingine akasema anapinga, je atakuwa anapingana na chama, mwenyekiti au atakuwa sahihi.
 
Mkuu Ben serikali tatu ndio mwanzo wa majimbo. Nakuapia CCM hawatoweza kukwepa sera ya CDM ya kuigawanya hii nchi kwenye majimbo yetu macho Mkuu

wewe, kibaraka wa ben, umeelezwa kuwa majimbo ni chanzo kikuu cha udini,ukabila na ukanda na mgawanyiko katika nchi..acha kukariri na kukopi na ku paste hata mambo yasiyo na maana..acha u mr yes.
 
Hii ni staki na nataka style of doing politics..mara tunajitoa maa tunaiunga mkono mara baregu ondoka kwenye tume, chama hakina msimamo kimebaki kuyumba na kuweweseka tu
 
Anatapatapa kuna uzi wake upo jukwaa la katiba anasema watanzania kataeni serikali tatu, hapa Mbowe anataka serikali tatu, wewe unataka serikali ngapi?

Mzee Mwanakijiji sio mshauri wala afisa wa Chama. Chama kupitia kwa mwenyekiti wake Mbowe kimeunga mkono mfumo wa serikali 3 kama njia ya kutatua migongano wa kiutendaji. Pia ni msimamo wa chama (rejea waraka wa CDM kwa Rais). Lakin pia kuna marekebisho yatahitajika kufanyika
 
kwani ni lazima kila mtu aunge mkono Serikali tatu? Inawezekana wale wanaodai serikali moja wana hoja zaidi kuliko wanaodai serikali tatu. KUtofautiana huku haina maana wenye kudai serikali tatu basi wanaitakia Tanzania mema zaidi kuliko wanaotaka serikali moja.
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa sana. Maana mimi ni mmojawapo wa wale wasiounga mkono serikali tatu. Badala ya kufikiria kuwa na serikali tatu tungefikiria kuwa na optiona ya ama serikali moja au kuvunja muungano. Si lazima sana kuwa na muungano. Kuna nchi ngapi duniani hazina muungano? Kwanini sisi tunaung'ang'ania muungano? Halafu muungano wenyewe ni kati ya nchi yenye watu milioni 44 na ka nchi kenye watu milioni moja na nusu. Halafu zinataka hizi nchi mbili zipate equal share and representation kwenye muungano? Si uhuni huu? Angalia kwenye pendekezo tu la wabunge wa muungano; eti watu milioni 44 wawakilishwe na wabunge 50 halafu watu milioni moja na nusu wawakilishwe na wabunge 20. Hivi kuna usawa wowote hapo? Yaani ka nchi kenye idadi ndogo ya watu kuliko hata mkoa wa Mwanza au Mbeya, achilia mbali Dar es salaam kawe na wawakilishi 20 kwenye muungano huku watu bara ikiwa na wawakilishi 50 ambao ni kama wawakilishi wa mikoa miwili tu kama tukitaka kuchukua uwiano sawa? Halafu kwanini tuingie gharama kubwa hivyo za kuongoza nchi serikali? Kama muungano ni lazima basi tuform states kama za marekani. Kila mkoa uwe ni state, na Zanzibar iwe ni mojawapo ya hizo states zinazounda Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hii ni staki na nataka style of doing politics..mara tunajitoa maa tunaiunga mkono mara baregu ondoka kwenye tume, chama hakina msimamo kimebaki kuyumba na kuweweseka tu

Ungejua rasimu iliyokuwa imeandalia kabla ya hii, machoz yangekutoka. Ushukuru msimamo wa chadema ndo umeleta mabadiliko katika rasimu hiyo....
 
wewe, kibaraka wa ben, umeelezwa kuwa majimbo ni chanzo kikuu cha udini,ukabila na ukanda na mgawanyiko katika nchi..acha kukariri na kukopi na ku paste hata mambo yasiyo na maana..acha u mr yes.
Majimbo ni mpango mzima!!!! unataka niwe kibaraka wa Mwigulu kama wewe? Au nishabikie CCM kwaajili ya kupata Buku saba Lumumba? au nishabikie chama cha kiliberali kama CUF? kwa hayo haminipati
 
Lakini 3 ni nzuri ila maraisi wa 3 ni janga!
Itifaki itakuwaje?
Hii itakuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na serikali 3 na maraisi wa 3! Tusubiri tuone
 
Serikali tatu ni kuongeza mzigo usio kuwa na manufaa kwa umma na si lazima. Nadhani heri tufanye mawili kuwe na muungano kamili yaani hakuna Zanzibar wala Tanzania bara ibaki Tanzania tu ama hilo likishindikana basi kila upande kivyake yaani Tanzania pekee na Zanzibar kivyao. Nilitegemea uungwana na upendo utawale ili sehemu ambazo hazikuwa za muungano ziunganishwe kuleta muungano kamili lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo. Sasa hata yale ya muungano yanatawanywa. Je huku ni kuimalisha ama kudhoofisha afya ya "waawale" wa muungano?
 
Sio Kweli kuwa watu wanaipenda tatu isipokuwa wanajua ikija itasaidia kuvunja muungano kama ilivyotokea URUSI ENZI YA AKINA YESTIN hivyo wanataka serikari angalau kuepuka kuilea Zanzibar

Tangu awali Wazanzibari ndio walikuwa wanatatizwa zaidi na muundo wa Muungano wa serikali mbili ikilinganishwa na wenzao wa Tanganyika. Hatma ya muundo wa serikali tatu bado iko mikononi mwa wazanzibari endapo wataridhia. Wazanzibari ndio pia hawataki kusikia habari ya muundo wa serikali moja ambayo Watanganyika wangependa.
 
Serikali moja tu ya Tanganyika pale juu achana na hawa walalamishi Kamanda Mbowe

Achaneni kabisa na hii habari ya Katiba ya Muungano haina maana tuhangaike na yetu ya Tanganyika

Watu milioni 44 kwa Vijitu Milioni 1 ni UJINGA!
 
kwani ni lazima kila mtu aunge mkono Serikali tatu? Inawezekana wale wanaodai serikali moja wana hoja zaidi kuliko wanaodai serikali tatu. KUtofautiana huku haina maana wenye kudai serikali tatu basi wanaitakia Tanzania mema zaidi kuliko wanaotaka serikali moja.
Mkuu, kwa sasa hivi suala la serikali moja sio option kabisa (labda kama serikali hiyo itaitwa "serikali ya mapinduzi zanzibar"). Katika hadidu za rejea kwa tume ya Warioba, mojawapo ni kuhakikisha uwepo wa "Serikali ya Mapinduzi Zanzibar".

Kwa hiyo labda kama kwanza tunakataa mchakato huu wa katiba mpya kama ulivyo. Lakini kama tunaukubali mchakato huo kama ulivyo, ni lazima tukubali pia ni mchakato ambao, technically, hauna namna ya kutuletea serikali moja kwa sababu ya Zanzibar kimsingi ni lazima iwepo/iendelee kuwepo.

Ukisoma michango ya watu humu, unapata hisia kama vile hawakuwepo wakati mchakato huu unaanza (kama nakumbuka vizuri, wewe uliupinga!🙂). Tulifanya kosa kubwa kukubali mchakato huu kufungwa na hadidu za rejea zilizoandaliwa na mtu mmoja - Rais (au tuseme kikundi cha watu wachache!).

Tume itaongozwa na misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha mambo yafuatayo:-
i. kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano;
ii. uwepo wa Serikali, Bunge na Mahakama;
iii. mfumo wa kiutawala wa kijamhuri;
iv. uwepo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
v. umoja wa kitaifa, amani na utulivu;
vi. uchaguzi wa kidemokrasia wa mara kwa mara katika vipindi maalum kwa kuzingatia haki ya watu wote wenye sifa ya kupiga kura;
vii. ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu;
viii. utu, usawa mbele ya Sheria na mwenendo wa sheria;
ix. uwepo wa Jamhuri ya Muungano isiyofungamana na dini yoyote na inayoheshimu uhuru wa kuabudu; na x. kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao kwa uhuru kwa lengo la kuendeleza na kuboresha masuala hayo 9(3).
 
Mimi ni katika wa2 wasioamini katika uongo no mater umepambwa namnagani.kwa tanganyika tunahitaji serikali 1.muungano ni kama ndoa kama mnahitajiana hamna maana ya kujadili hii nyumba iandikwe jina la nani?muungano una kupoteza baadhi ya mambo.
 
Sijui kama CDM wanajifunza ! hivi hii ni kauli ya Mbowe au ya chama?
Ile ya Kitila ni yake, hii ya Mbowe je? Kwanini kusiwe na taarifa ya chama kuhusu msimamo wa Chadema

Ina maana wao wamekubali kila kitu, kama sivyo kipi wanadhani kiboreshwe kipi kiachwe n.k. na kwanini wanadhani msimamo wao umekidhiwa katika katiba mpya.

Je, tatizo la katiba ililikuwa kurudi kwa Tanganyika? Mambo mangapi ni muhimu sana katika katiba.
Wameridhika na tume ya uchaguzi, wameridhika na mfumo wa mahakama?

Nadhani walitakiwa watoe statement ya chama na si kila mmoja kivyake. Hivi akiibuka mwingine akasema anapinga, je atakuwa anapingana na chama, mwenyekiti au atakuwa sahihi.
Mkuu wewe nadhani ni mdau wa haya mambo ya siasa utakuwa unakijua vema chadema kila mtu mkubwa pale wenje aliwahi kutangaza baraza la mawaziri la chadema baada ya 2015 hata uchaguzi mkuu bado haujafika kwa hiyo usitegemee muongozo wowote toka chadema.
 
Mbeya/Dar. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman ameweka bayana kuwa wanaunga mkono Rasimu ya Katiba na hasa suala la Muungano wa Tanzania kuundwa na Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Amesema mambo mengi yaliyopendekezwa na chama chake yamefanyiwa kazi na Tume ya Mabadiliko na kuishangaa CCM akidai kwamba inapinga rasimu hiyo hususan suala la Serikali tatu wakati kimsingi watu wa Tanzania Bara wamekuwa wakipunjika kwenye muundo wa sasa wa Muungano.

Akihutubia mkutano wa kampeni ya kuwania udiwani wa Kata ya Iyela katika Uwanja wa Bongonela, Mbeya jana jioni, Mbowe alisema chama chake kinataka kuona Serikali ya Tanganyika ikifufuliwa. Alikuwa akimnadi mgombea wa Chadema, Charles Mkela.

Alisema Chadema kinataka kuona Wazanzibari wakiwa na Serikali yao ili wajiamulie mambo yao na pia Watanganyika wawe na uongozi wao lakini waunganishwe na Serikali ya Muungano.

Alisema muundo wa sasa wa Muungano una matatizo. Kwa mfano, mbunge wa Zanzibar anawakilisha watu wachache zaidi ukilinganisha na mbunge wa Bara. Wananchi mtashangaa sote tunalipwa sawa."

"Ila zikija Serikali tatu ina maana kuwa kila upande wa Muungano utatumia rasilimali zake. Haya mambo kulipana fedha nyingi kwa kazi kidogo yatakoma."

Msimamo wa Sumaye

Sumaye alisema muungano wa Serikali tatu haufai akisema utasababisha mvutano mkubwa wa kimadaraka na rasilimali.

Sumaye anaungana na wanasiasa wengine waliopinga muundo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wengine wakiwa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM) Profesa Juma Kapuya, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba na Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Maua Daftari.

Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), akiwa Johannesburg, Afrika Kusini mwishoni mwa wiki, alisema Serikali tatu zinaweza kutikisa Muungano.

"Huwezi kutatua matatizo kwa Serikali tatu... unaweza kuyaongeza kwani kutakuwa na Serikali tatu na marais watatu... kama kuna mvutano baina ya Serikali mbili ukiongeza ya tatu inaweza kuwa na mvutano zaidi," alisema na kuongeza:

Lipumba: Katiba ya Bara kwanza

Profesa Lipumba alisema hakuna mantiki ya kupiga kura ya maoni ya Katiba ya Muungano bila kuwa na Katiba ya Tanzania Bara na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mapendekezo ya msingi ya CUF ni kwamba, kura ya maoni isubiri kukamilishwa kwa rasimu ya Katiba ya Tanzania Bara na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar.

Alisema licha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kufanya kazi nzuri ya kuratibu maoni bila kushinikizwa na matakwa ya CCM, kuna baadhi ya mambo ya msingi ambayo yameachwa kwenye rasimu.

"Huwezi kuacha vitu kama umilikaji wa ardhi, maliasili na rasilimali za nchi, elimu, afya na mazingira ya kukuza uchumi na uhuru wa Serikali za mitaa. Rasimu imeshughulikia mambo ya Muungano."

"Maoni ambayo CUF tuliyatoa ikiwamo muundo wa Serikali tatu, kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, Rais kutangazwa baada ya kushinda kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, Spika kutokuwa mbunge na mengineyo yamepata nafasi."

Imeandikwa na Brandy Nelson, Ibrahim Yamola na Aidan Mhando.


 
Big up both CHADEMA and CIVIL UNITED FRONT (CUF) kwa kuona mbali .....mimi nakubaliana na serikali tatu Muunganio wa Tanzania, Tanganyika na Zanzibar
 
Back
Top Bottom