CHADEMA inaunga mkono Rasimu ya Katiba mpya - Mbowe

CHADEMA inaunga mkono Rasimu ya Katiba mpya - Mbowe

Kwa rasimu hii kuna kila ishara ya CCM kufa haraka ndiyo maana viongozi wake wanaipinga!
 
Serikali tatu ni mzigo kwa taifa letu maskini,napinga vikali serikali tatu,napinga serikali mbili.
Tuwe na serikali moja au tuvunje muungano.
Tanganyika bila muungano inawezekana!!!!
 
Ritz,

Acha hizo.Kila mtu ana mawazo yake.Hata ndani ya vyama CCM na Chadema kuna watu wenye mawazo tofauti.Ni muda mrefu nilikua nikiongelea Serikali Moja ambayo ni Federal.Tugawanye Tanganyika na Zanzibar kwenye majimbo na yapewe nguvu kama ilivyo India na hata Kenya walivyofanya juzi ingawa kuna tofauti kidogo.

So kila mtu ana mtazamo wake lakini mwisho wa siku mtatoka na msimamo wa pamoja kama chama.Acha jaribio hili la upotoshaji na propaganda

Ben Saanane,

Ni ache hizo vipi ndugu yangu wakati mnatofautiana hata kuwayumbisha wafuasi wenu, kwa nini mlitaka Prof. Baregu ajitoe kwenye ujumbe, na kwa nini mlitishia kujitoa kwenye mchakato wa katiba.
 
Last edited by a moderator:
Kwa haya CCM na CDM wataungana tu, Serikali tatu ni mwiba kwa CCM na kupita kwake ina maana kuvunjika kwa muunganano kwa maana haitakuwa ni busara kuwa na sekali ya shirikisho ndani ya shirikisho jingine la EAC, hii italazimisha Zanzibar kuingia shirikisho la EAC kama Nchi na hapo ndipo utabili wa Baba wa taifa wa kuvunjwa Muungano utakapo kuwa umeanza mwendo. lakini pia Mgombea binafsi kwa CCM ni ahueni kwa sababu inawezekana mgombea huyo akawa mwana CCM ambaye hatataka mizengwe ya ndani ya chama, lakini kwa CDM hawana mtu anayeweza kwa sasa kugombea na kupata ushindi 2015 kwa muda uliobaki. hapa wapatane tu serikali iwe moja au mbili lakini mgombea binafsi iwekewe veto.
 
Jamani hembu naomba mnisaidie kujua faida na hasara ya serikali tatu, binafsi nimeulizwa hili swali nimeishia kujilamba midomo......
 
Habari ndiyo hiyo na leo CCM nao wanaunga mkono rasimu ya katiba basi shughuli imeisha, Mbowe ndiyo kaishaamua nani atapinga.

Ina maana Mbowe hakufanya mawasiliano kwanza na baba mkwe wake, manake baba mkwe wake yeye kaipinga.
 
GAMBA moja limeleta POST likimpa pole kamanda wa anga kwamba alihutubia watoto wa shule ya msingi na yeye kama mtoa taarifa akiwa mbali na eneo asije kunyang'anywa kadi yake!
Sasa ili kukata mzizi wa fitina tunaomba uweke picha tuhukumu!
 
kwani ni lazima kila mtu aunge mkono Serikali tatu? Inawezekana wale wanaodai serikali moja wana hoja zaidi kuliko wanaodai serikali tatu. KUtofautiana huku haina maana wenye kudai serikali tatu basi wanaitakia Tanzania mema zaidi kuliko wanaotaka serikali moja.
Serikali moja hoja zipo tena zenye mantiki ktk Muungano ila sasa hizo hoja Wazenji wanaweza kukubali...?
 
Mimi naunga mkono rasimu ya katiba iliyotolewa na tume ya Jaji warioba lakini sikubaliani na kipengele kinachokataa uwajibikaji wa Rais kwa yale atakayoyafanya akiwa madarakani kinyume na sheria!! Viongozi wengi wa kiafrika wanafanya uongozi na hasa urais kama njia ya kuibia nchi zao kwavile tu katiba zinawahakikishia kuwa hawatashtakiwa mara wanapotoka madarakani; ili kuwazuia wasifanye ufisadi ni bora katiba yetu mpya ikaweka wazi kuwa Rais is not above the law na kwamba anaweza kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayohusu kukiuka sheria wakati wa utawala wake.

Mwanya wa viongozi wa nchi kutowajibika kwa makosa wanayoyafanya wakiwa madarakani ndio sababu kubwa ya wanasiasa wengi wasiokuwa waadilifu kukimbilia kuusaka uongozi na hasa ukuu wa nchi; hivyo basi kama kutakuwa na kipengele cha uwajibikaji na kushitakiwa baada ya kutoka madarakani, kasi ya wanasiasa wanaotaka kutumia uongozi kama njia ya kujitajilisha itapungua kwani watajua kuwa mwisho wa siku wanaweza kupelekwa lupango!!! Kama we are serious about fighting corruption and impunity then we must must have an article in our constitution tha t will hold presidents accountable for breaking the law while in office. Naomba kutoa hoja.
 
Serikali 3 ndio suluhisho pekee la kuunusuru Muungano usiende na maji lakini kwa Mwenye akili
 
CDM huwa wananifurahisha yaani wamekuwa watumwa wa kifikira kuwa atakachosema Mbowe, Silaa na Lema basi hakuna wa kukipinga yaani wamenyimwa ufahamu kabisa wa kufikiri na kuchambua. Nafikiri hata wakiambiwa hata wakiambiwa watembee kinyumenyume watatembea ili iradi kauli hii iwe imetoka kwa waziri wa mambo ya ndani Lema, Mwenyekiti Mbowe na Katibu Slaa a.k.a Mzee wa onyo.
 
Mbona mnapingana na mshauri wenu wa chama Mzee Mwanakijiji.

Kabla ya kudakia msimamo wa wengine ingekuwa bora zaidi kama ungeanza kujadili msimamo wa chama chako (ccm), na kauli ya km kinana na akina nape kama kweli wanaitakia mema nchi yetu
 
someni kwanza rasimu ndo mtoe maoni, tume ya uchaguzi sasa imekuwa tume huru ya uchaguzi, mwenyekiti wa wa tume atatuma maombi kwa kamati teuzi ambayo mwenyeki wake ni jaji mkuu wajumbe ni spika na naibu na m\kiti wa tume ya haki za binadamu.
 
CDM huwa wananifurahisha yaani wamekuwa watumwa wa kifikira kuwa atakachosema Mbowe, Silaa na Lema basi hakuna wa kukipinga yaani wamenyimwa ufahamu kabisa wa kufikiri na kuchambua. Nafikiri hata wakiambiwa hata wakiambiwa watembee kinyumenyume watatembea ili iradi kauli hii iwe imetoka kwa waziri wa mambo ya ndani Lema, Mwenyekiti Mbowe na Katibu Slaa a.k.a Mzee wa onyo.

Yani we ndo umenifurahisha zaidi kwa Ujinga uliongea hapa.
 
Back
Top Bottom