Katika maswala nyeti ndani ya chama kwa mstakabali wa nchi kama hili la katiba, CCM huwa inaonyesha tofauti kubwa na vyama vingine vya siasa.
Hapa ndipo nidhamu ya chama inapotakiwa kufanya kazi ndani ya corrective responsibility. CCM kwa hili wanastahili pongezi.
Hata wale waropokaji ndani ya CCM huwezi kuwasikia kwenye maswala kama haya. CCM kwa sasa wako kimya kana kwamba hawajui kile kinachoendelea katika mchakato wa katiba.
Chama cha CHADEMA ambacho watu wangetegemea kiwe na nidhamu kutokana na kuwa na nafasi ya kuyajua makosa ya CCM na kujifunza, ndiyo kinakuwa na tatizo la political discipline. Mpaka sasa kauli mbali mbali za viongozi wake tumeishazisikia kuhusiana na rasimu ya katiba bila kujua kama ni kauli za chama au za kwao binafsi ikichukuliwa zinatolewa kwenye majukwaa ya siasa ili mladi kila mmoja anasema kwa kadri anavyopenda.
Ama kweli kijana ni kijana tu, na mzee ni mzee tu.