CHADEMA inawezaje kuwa na wastaafu wa Jeshi au viongozi waliowahi kuwa karibu sana na Usalama wa Taifa?

Kalimanzila Amemaliza kila kitu 🙌🙏🙏
 
Kumbe askari wastaafu hawatakiwi kuwa na uanachama wa chama cha siasa?
 
CCM ni Chama tawala cha Muda mrefu , usalama kuwepo CCM siri nyigi zinahusu nchi na Wao
Siri za nini..dunia ya leo unaweza kuwa na siri? siri za aina ya silaha mlizo nazo km nchi, au siri gani hasa unazodhani zipo na ni wajibu zilindwe..! toa mfano..
 
Kuna miongozo na taratibu za kufanya shughuli mbali mbali hapa nchini. Mf. Kufungua Shile, hospitali, kampuni mbalimbali, kulima, kuvua,...........
Miongozo hiyo izingatiwe.
Marehemu angejipambanua kama mwana ccm asingeuliwa!?., pamoja na nafasi alokuwanayo.
Kama mfumo wa vyama vingi tulilazimishwa kwanini tuendelee kuwa wanafaki kwa gharama ya uhai wa baadhi ya wenzetu?, Tena kikatili namna hii!. Tunashindwa nini kujitangaza kuwa sisi ni wajamaa na dunia ituelewe hivyo kama wachina?
Kwa mwenendo huu tumeamuwa kuwa jamii ya watu wa hovyoooo.
 
Kwa akili yako huwezi kujua hata unayoyaandika.
 
Kuwa Upinzani Sio Dhambi
 
Huwa nawashangaa sana wanasema wanatoa Siri.Hivi Nchi masikini hivi ya Tanzania inasiri Gani ya maana ambayo haitakiwi kutolewa?Kila kitu Nchi ni tegemezi kwa Nchi matajiri na unadai unasiri
Ni mambo ya kushangaza sana, uko nchi maskini km Tanzania unadai kuna siri, wewe omba omba uwe na siri, siri gani?? labda siri za kuua raia wema watanzania wasio na kosa km Mzee Kibao, na hizohuwezi kufanya ziwe siri za nchi!
 
Watu kama wewe inabidi Kwenda shule tena, lazima una elimu ya chini sana! CCM na Chadema vyote ni vyama vya siasa, tofauti iliyopo ni kuwa CCM ipo madarakani na Chadema haipo kwa hiyo inabaki opposition. Chadema kama inatatawala CCM itakuwa opposition. Wanajeshi wako NEUTRAL; wakistaafu anaweza kuchagua chama atakacho.
 
mbona hata ccm wametajwa hapo au
Ukiwa na kadi ya chama cha mapinduzi au ukiwa chama cha mapinduzi hakuna tatizo lolote..

Nikuulize tu unahisi wakuu wa Mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wengine wa Kisiasa, mawaziri na viongozi wa vyama unaowasikia wa CCM ambao walikuwa wanajeshi au ni wanajeshi ni wangapi????
kama kikwete na wengine kibao (Sina haja ya kuwataja) Kina capt John komba na wengineo wengi Hwakuwa CCM?

MImi ni mtu mzima na naelewa ulikuwa umelenga Kundi gani??
 
nimesema vyema hapo mwishoni kwamba nadhani ni vyema baadhi ya watu wakistaafu wasiingie kwenye siasa
 
basi tuseme kuwa na mipaka kati ya idara ya usalama na siasa .
Mkuu Unafahamu Kuwa Jeshi lilikuwa Chini ya CCM kabla ya Vyama Vingi??

Na hata katiba tulio nayo bado ina ukakasi na haijabadilika kuhusu hilo na ndo maana Watu wanataka katiba mpya ili hayo yote yawekwe wazi kwenye katiba...

Unahisi kwanini kenya ina nguvu sasa baada ya kupata katiba mpya??

Mambo kama haya yalikuwa mengi sana..

Katiba iliyopo ni katiba ya Chama kimoja
 
Hata maiti haiwezi kuwaza kama unavyowaza.
Kwani Chadema ni chama cha magaidi ila Ccm ndo chama cha siasa.
Elimu mbovu tunayopewa ndo matokeo ya wananchi kama Hawa.
Si mruhusu Katiba mpya,mbona mmeganda na Katiba iliyopitwana wakati.😡😡
 
We bumunda
! Nadhani chama tawala dhaifu wemechoka sana hawajui pa kushika Kila mtu wanamhisi ni mpinzani

Wameanzisha kitengo Cha mauaji ili kuleta hofu na kuwatisha wapinzani na kuua demokrasia ili waendele kula bila bugdha huku nchi ikizidi kufidia kiuchumi na kisiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…