Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Badamu batachuruzika safari hii!
=====
Wajumbe wa Mkutano Mkuu CHADEMA kutoka Mkoa wa Iringa wakiongozwa na makatibu kutoka jimbo la Kilolo, Iringa mjini na wilaya ya Iringa pamoja na viongozi wengine wameibuka kupinga kauli ya mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa, William Mungai aliyeueleza umma kuwa mkoa huo unamtaka Freeman Mbowe kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa chama Taifa.
Ikumbukwe William Mungai pamoja na wenyeviti wa CHADEMA kutoka Mikoa 21 nchini, Desemba 18, 2024 walikwenda nyumbani kwa Mbowe(Dar Es Salaam) kumuomba agombee.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Mwenyekiti CHADEMA Iringa: Mbowe ni role model, asiogope mtu yeyote hata we nje ya nchi
Ujumbe wa wenyeviti hao ulisomwa na Mungai ambapo kauli yake imepingwa vikali na makatibu hao Disemba 20, 2024 wakisisitiza kauli aliyoitoa ni maoni yake binafsi na sio wajumbe wa mkutano Mkuu wa CHADEMA Iringa.
David Mfugwa katibu wa CHADEMA, Wilaya ya Kilolo kwa niaba ya mwenzake amesema "Mungai ametoa kauli ambayo yeye anasema ni msimamo wetu kitu ambacho sio kweli hatukuwahi kukubaliana kwa kauli moja ya kumuunga mkono Mbowe sisi tunasimama na Tundu Lissu kwani tunaamini anatosha kukiongoza chama chetu"