Chadema isipokufa mwaka huu basi 2021 kitakuwa chama " halisi" cha Upinzani

Chadema isipokufa mwaka huu basi 2021 kitakuwa chama " halisi" cha Upinzani

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Mwaka uliopita 2019 Chadema imepita katika mapito magumu lakini kwa kuwa kinapokea ruzuku ya serikali kimeweza kusurvive.

Mwaka huu ni wa uchaguzi na ruzuku itakata rasmi baada ya bunge kuvunjwa hivyo chama kitaendeshwa na wananchi.
Endapo Chadema itaingia mwaka 2021 ikiwa imara basi haitakufa tena kama ilivyo TLP ya Lyatonga Mrema!

Maendeleo hayana vyama!
 
Si huwa ninasikia kuna mtu anang'ang'ania uongozi kwa sababu ya ruzuku!!?
 
Wewe sio wa kwanza kuja na kauli kama hizi. Kabla ya mwaka 2015 kuna mtu mmoja mzito alikuwa anaitwa Steven wassira au Tyson alikuja na kauli kama zako. Ajabu leo hii yeye ndiye hajulikanai yuko wapi na chadema inaendelea kuwepo
 
Kutokana na ubaya wa wenye msimamo wa chuki kwa wapinzani wanadhani CHADEMA ikifa na upinzani umekufa, watu wote watawaunga mkono ccm, na kumbe hayo si kweli.

Na tena si kweli kwamba wale wasioipenda ccm wanakosa uzalendo, kuwa mzalendo ni kuipenda nchi yako.
Hata kule kuwa na mawazo tofauti na wana ccm bado ni uzalendo kwa sababu tunashindanisha mawazo yetu, tunashindanisha hoja zetu na mwishoni wananchi wanaamua.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 1995 kulitokea dhoruba kali sana kwenye vyama vya upinzani na hata ndani ya CCM kutokana na kilichoitwa upepo wa Mrema akiwa NCCR Mageuzi! Aliweza kukusanya wafuasi wengi kutoka vyama vyote na wengi waliamini vyama vingine vingekufa, lakini mara baada ya uchaguzi ule ambao Mrema hakufanikiwa kushinda, chama chake ndicho kilichokuwa cha kwanza kuanza kuporomoka ingawa wengi tunaamini lile gogoro kati yake na katibu mkuu wake lilichangia zaidi kukiua chama hicho! Pia wanachama wengi waliohamia ndani ya chama hicho cha NCCR Mageuzi, ndio haohao waliokuja kukiua chama hicho,

Hivyo sidhani kama CCM ipo salama kwa utamaduni iliouanzisha miaka ya sasa kuona kuwa njia ya kukijenga chama ni kuvuna viongozi na wanachama wa kutoka vyama vya upinzani tena kwa njia za ushawishi wa kutumia zawadi badala ya sera na mipango madhubuti, Ni haohao ndio watakaovisaidia vyama vya upinzani kukiang'oa chama hicho. Na CDM itabaki imara siku zote.

Kwa hiyo watu wanaozani au kufikiri kuwa CDM itakufa kwa kuamini kuwa itakosa viti vya ubunge na hivyo kukosa Ruzuku wanapiga hesabu za kutumia vihesabio! Kwanza kikubwa ni kwamba tayari CDM ilishazindua mfumo na mkakati wa kukusanya michango yake toka kwa wanachama , hivyo kama mkakati huo utasimamiwa vizuri, unaweza kukivusha chama hicho bila kutegemea ruzuku.
 
.
Mwaka uliopita 2019 Chadema imepita katika mapito magumu lakini kwa kuwa kinapokea ruzuku ya serikali kimeweza kusurvive.

Mwaka huu ni wa uchaguzi na ruzuku itakata rasmi baada ya bunge kuvunjwa hivyo chama kitaendeshwa na wananchi.
Endapo Chadema itaingia mwaka 2021 ikiwa imara basi haitakufa tena kama ilivyo TLP ya Lyatonga Mrema!

Maendeleo hayana vyama!
tapatalk_jpeg_1583347042165.jpeg


Jr[emoji769]
 
Chadema wamekuwa wakiendelea na aina moja ya siasa kwa muda mrefu mno.

Inapaswa wabadilike ama itawawia vigume kuendelea kushindana na vyama vingine, Ukichukulia kwamba baadhi ya manguli wake wamekihama, katika hali ya kawaida kitendo cha kuhamwa na wanachama wengi kwa muda mfupi utahitajika muda tena ili kurudia katika hali yake.

Naona madhara ya kukimbiwa katika ziara za mbowe, gap lipo kubwa sana. Chama kimetikisika.
 
Si huwa ninasikia kuna mtu anang'ang'ania uongozi kwa sababu ya ruzuku!!?
Ndo maana anataka kuzipiga za mara ya mwisho alishausoma mchezo kuwa akiziachia za mwaka huu kabla ya uchaguzi basi itakuwa basi tena

Kwahiyo anapiga za lala sarama mzee wa kazi.
 
Wewe sio wa kwanza kuja na kauli kama hizi. Kabla ya mwaka 2015 kuna mtu mmoja mzito alikuwa anaitwa Steven wassira au Tyson alikuja na kauli kama zako. Ajabu leo hii yeye ndiye hajulikanai yuko wapi na chadema inaendelea kuwepo
Hatimaye ye ndo kafa kisiasa anapelekwa puta na mjukuu wake
 
Chadema wamekuwa wakiendelea na aina moja ya siasa kwa muda mrefu mno.

Inapaswa wabadilike ama itawawia vigume kuendelea kushindana na vyama vingine, Ukichukulia kwamba baadhi ya manguli wake wamekihama, katika hali ya kawaida kitendo cha kuhamwa na wanachama wengi kwa muda mfupi utahitajika muda tena ili kurudia katika hali yake.

Naona madhara ya kukimbiwa katika ziara za mbowe, gap lipo kubwa sana. Chama kimetikisika.
Waliohama waliikuta wameacha pia.Timu haifi Kwa kuondokewa na wachezaji bali makocha na mashabiki
 
Mwaka uliopita 2019 Chadema imepita katika mapito magumu lakini kwa kuwa kinapokea ruzuku ya serikali kimeweza kusurvive.

Mwaka huu ni wa uchaguzi na ruzuku itakata rasmi baada ya bunge kuvunjwa hivyo chama kitaendeshwa na wananchi.
Endapo Chadema itaingia mwaka 2021 ikiwa imara basi haitakufa tena kama ilivyo TLP ya Lyatonga Mrema!

Maendeleo hayana vyama!
Mlisema 2020 upinzani utakuwa umekufa vipi tena 2021 na si 2020.Tuwasaidie njia nyepesi ya kuuwa upinzani sio kutumia polisi mtachelewa,waondoleeni njaa wananchi Kwa kufanya hivo tu upinzani utakufa
 
stroke,
Inawezekana hiyo ndio siasa halisi, CHADEMA ndio chama chenye idadi kubwa zaidi ya wanachama na tena wanachama wake wanajitambua!

Huwezi kuiua CHADEMA wala kuififisha! Utakufa wewe mwenyewe na Mwenye upeo yeyote itakuwa analijua hilo! Ila mbumbumbu, na watafuna upepo hawalijui na hawajui watendelo!!

CHADEMA bila ya tume magumashi kuanzua 2010 wangekuwa magogoni, achana na 2015! Mtu yeyote Mwenye upeo angelitambua hili!
 
Ruzuku sio chama,chama ni wafuasi. Chukulia mfano chama dola kama CCM,limebaki kwenye ngazi ya juu lakini grassroot imekufa kitambo.Na chama bila grassroot si chama cha siasa.

Eti leo unajiandikisha uanachama CCM unapewa kadi faster faster! Wapi miezi 3 ya kusomea ukada wa chama?
Hata katibu mkuu wa CCM Bashiru analiona hilo alivyodai mkuu wa mkoa fulani apelekwe Kivukoni.
 
Back
Top Bottom