Pre GE2025 CHADEMA itaingia Uchaguzi wa 2025 ikiwa Imesambaratika na kupasuka vipande vipande kama kioo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndugu zangu Watanzania,

Hili ni jambo la wazi kabisa lisilo hitaji shahada ya sayansi ya siasa
kutoka UDSM au Elimu kubwa sana.hili ni jambo ambalo kwa mwenye akili timamu na mwenye akili huru na kufikiri vyema anaona wazi kabisa kuwa chama hiki kilichopata kujizolea umaarufu na kuwa na ushawishi hasa kwa vijana, kinakwenda kuingia uchaguzi mkuu hapo mwakani kikiwa Kimesambaratika na kupasuka pasuka vipande vipande kama kioo.

CHADEMA inakwenda kuingia katika uchaguzi Mkuu ikiwa haina umoja wala mshikamano wala malengo mamoja. kila mtu anakwenda akiwa na lengo la kusaka Tonge lake kwa ajili ya tumbo lake.kila mtu anakwenda kugombea fito yake.hakutakuwa na mipango au mapambano ya kupigania na kupambania ushindi wa chama,bali kila mmoja ataangalia maslahi yake binafsi.kila mtu atajiangalia anapata nini na siyo chama kinashinda nini na kupata nini.

Kila mtu ndani ya chama atakuwa anaangalia awe upande wa kiongozi yupi ili apate Tonge lake,badala ya kusimama katika nguzo zilizoshikilia chama. Ukiona viongozi wa juu kama wajumbe wa kamati kuu pamoja na wanachama wao wanatoka hadharani kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii wanatupiana maneno ya kukejeliana,kudhalauliana, kudhalilishana,kuongelea maisha binafsi baina yao,kushutumiana,kurushiana Madongo na kushushiana heshima.

Basi ujuwe mahali hapo hakuna chama wala umoja wa kichama.bali kuna Mpasuko mkubwa sana na mashindano ya kupigania maslahi binafsi ya kila mmoja na tumbo lake. Ukiona mambo yaliyopaswa kuzungumzwa katika vikao vya chama yanazungumzwa hadharani ,basi ujuwe huko ndani kunawaka moto mkali sana ambapo hakuna anayetaka kukaa huko ndani kupeleka jambo lake maana hakukaliki wala kuaminika kwa usalama wa kila mtu.

Kwa sababu chama imara kinachojiendesha kitaasisi na chenye kuheshimu katiba na maadili ya chama huwezi ukaona malumbano ya viongozi kwa viongozi au viongozi na wanachama yakifanyika hadharani na kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.ikifika hapo maana yake ni kuwa ndani ya chama hakuna kuaminiana wala kuheshimiana zaidi ya kila mtu kujiona ni beberu au jogoo anayewika au kila mtu anajiona yeye ndiye chama.

Athari ya hali hii ni kuwa chama hakiwezi kuwa na nguvu na wala hakiwezi kushinda uchaguzi wowote ule.kwa sababu ushindi wa chama unaanzia ndani ya chama kikiwa imara na umoja nakwenda pamoja nje kupambana na vyama vingine kikiwa kimeshikamana na kuungana.Ibada njema huanzia ndani. Sasa kama mmegawanyika ninyi kwa ninyi ni vipi mtamshinda mshindani wenu aliye na nguvu,umoja, mshikamano na hamasa ya juu? Ni vipi utashindana na na jeshi lililo na umoja , morali na kiu ya ushindi wakati wewe unakwenda vitani ukiwa huna morali wala nguvu wala umoja wala hamasa?

Halafu kwa upofu wa akili na macho utasikia baada ya uchaguzi mkuu mtu anatoka hadharani na mdomo wake anaropoka bila aibu wala haya kuwa ameibiwa kura.

Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wewe na mintunga wenzio mtangoja na kuhudhuria gambosh hadi mujitoe kafara mkingojea upumbavu wako utimie!
 
Nimebubujikwa na machozi na masikitiko Njoo nisaide ephen_ mtu wako ataniua kwa kububujikwa.
 
Dua la Kuku halimpati Mwewe!
Ni kweli wanachama wa Chama pendwa wanasali usiku kucha kuomba CDM isambaratike. Chawa hawalali.
Hakuna Chama kinachoitesa CCM kisaikolojia kama CHADEMA.
Ilivyo CHADEMA ni Jinamizi kwa CCM.
 
Kama JIWE hakuweza,mdogo wangu tuliza kijambio chako kula mihogo na ujambe kwa raha zako na mwenza wako.
Unaweza kufa na kusambaratika wewe kabla ya kufika hiyo 2025.
 
Binafsi nilishapoteza tumaini kabisa na hiki chama. Ccm itatutawala sanaaa, hakuna chama pinzani ambacho kipo serious kuitoa Ccm madarakani. Hapa tusidanganyane wandugu. Ccm ata haiwez kupata presha ya uchaguzi kabisa. Tutatalalamika sanaa. Saizi n kuombea tu kupata viongozi walio na uchungu na hii nchi basi. Suala la kuitoa Ccm madarakan litabaki kuwa ndoto ya muotaji mwenye shida ya kusahau sahau!
 
Dua la Kuku halimpati Mwewe!
Ni kweli wanachama wa Chama pendwa wanasali usiku kucha kuomba CDM isambaratike. Chawa hawalali.
Hakuna Chama kinachoitesa CCM kisaikolojia kama CHADEMA.
Ilivyo CHADEMA ni Jinamizi kwa CCM.
CHADEMA hii dhaifu itawezaje kuwa tishio kwa CCM?
 
Kama JIWE hakuweza,mdogo wangu tuliza kijambio chako kula mihogo na ujambe kwa raha zako na mwenza wako.
Unaweza kufa na kusambaratika wewe kabla ya kufika hiyo 2025.
Kwa hiyo mimi ndio nimewatuma CHADEMA kushambuliana hadharani?
 
IMG_20240605_130850.jpg
Haya ndio maendeleo ya serikali ya mama yenu daktari wa mikopo.
 
Chama kilichofukuza majembe yake 19 ya BAWACHA kisitegemee chochote kwenye uchaguzi. Eti kwa sasa Mdude na Martine Maranja ndo wanategemewa kueneza itikadi ya CHADEMA....!! Yaani watu wanaoporomosha matusi kwa yeyote yule ndo wamekuwa tegemeo la chama
 
CHADEMA kwa sasa haiwezi na wala haina ubavu wala nguvu ya kuweza kushindana na CCM katika sanduku la kura.maana imeshasambaratika na kujidhoofisha yenyewe kwa yenyewe na ndio maana unaona viongozi na wanachama wakishambuliana wenyewe kwa wenyewe hadharani.
Umeona wapi pandisha ushshidi tuone
 
Chama kilichofukuza majembe yake 19 ya BAWACHA kisitegemee chochote kwenye uchaguzi. Eti kwa sasa Mdude na Martine Maranja ndo wanategemewa kueneza itikadi ya CHADEMA....!! Yaani watu wanaoporomosha matusi kwa yeyote yule ndo wamekuwa tegemeo la chama
Ndio maana kwa sasa chama kinakwenda kama kipofu gizani.
 
Back
Top Bottom