Mbona nishaongea kwamba hakuna chama kisicho uongozi, hakuna chama kisicho na trust katika uongozi, hata hao wabunge mnaotaka kuwachagua nao ni wawakilishi.Kama huamini katika uwakilishi na unataka wanachama waamue kila kitu, ondoa hata hilo bunge basi, kwa nini unapeleka watu kuwakilisha wengine? Si turudi kwenye democracy ya Athens, nchi nzima ikutane pale Dodoma kuamua mambo ya nchi, tuone kama itakuwa democracy au anarchy.
Nishasema, uongozi una wajibu wa kutetea interests za wanachama, na wanachama wana wajibu wa ku pressure uongozi kufanya hivyo.Zaidi ya hapo, mkiona uongozi hautekelezi wajibu huu, mna u vote off, au mnajiondoa na kuanzisha chama kingine.
Lakini there is no point ya kuwa na chama halafu wanachama totally hawana trust na uongozi wao, wanataka kufanya kila kitu wenyewe. Inafikia wakati, for the sake of chama kuweza kufanya vitu smoothly, the best informed people at the top of the party, wanafanya maamuzi kwa niaba ya wanachama wote. This is totally acceptable as long as there is reasonable transparency.
Tukitaka kila kitu kifanywe na wanachama wote itakuwa anarchy na vyama vitapoteza maana yake.
Nnajua tatizo ni kwamba tumekuwa stung vibaya sana kiasi kwamba hakuna kuaminiana kabisa, well, kama huamini mtu kuwa kama mimi, usiingie katika chama cha siasa.Ukishaingia katika chama cha siasa maana yake unaamini uongozi wa chama.
Huwezi kusema wewe mkatoliki, halafu ukasema maamuzi ya papa na conclave yake yatoke kwa waumini, utakuwa huelewi maana ya kuwa mkatoliki. Kama vipi uwe mpagani tu kama mimi, the minute ukikubali kuwa mkatoliki maana yake umeukubali uongozi wa busara wa papa.