Kiranga,
First off, uchaguzi nchini hauwapi ushindi wagombea wenye popular vote, unawapa ushindi wagombea waliopitishwa na vyama na kupata popular vote, big difference, so do not try to misrepresent that.
Ninachouliza ni kwamba, kama watu ni purist wa democracy kihivyo na wanataka watu wenye popular support bila chujio la chama, what is the point of having these parties? Kwa nini tusiviondoe vyama vyote na kuwashindanisha wagombea kama watu tu, na atakayepata popular vote awe mbunge, no chama no middleman's b.s ?
Mkuu nilitoka kwenda beba box na hivi sasa nimerudi..
Nadhani ni vizuri zaidi ikiwa kila mmoja wetu ataelewa swali la mwenzake kabla hajatoa jibu na hakika mimi sikukuelewa hivyo mwanzoni. Nilichokuelewa mimi ni kwamba kila chama kinafahamu kwamba uchaguzi mkuu mshindi ni yule anayepata Popular vote..hivyo mkazo wa maeleoz yangu uliegemea mgombea kama dereva na Chama kama shirika la usafiri.
Hivyo sielewi unachojaribu kusema hapo kwani kila dereva anahitaji bus la kusafirishia abiria na bus ni lazima liwe registered ndani ya shirika... Na unaponiuliza mimi kwa nini watu wasisafiri tu pasipo kuhitaji shirika la bus au hata bus lenyewe mkuu wangu unanipoteza kabisa.
Kwa mfano huo huo.. ma bus mengi Tanzania yanapata abiria kutokana na uzuri wa dereva (popualr vote) ambaye kachaguliwa na shirika (chama) kuliendesha na pia wapo watu wanavutiwa na shirika lenyewe pasipo kujali dereva..
Na hakika kila dereva kupitia interview na waajiri wake pia bus analoendesha ni mali ya shirika na sio yake. Hata kama dereva ni mzuri kiasi gani na anao uwezo wa kununua bus lake mwenyewe, bado anahitajika kusajiri bus lake na yapo masharti ya usajiri ambayo yanahusika shirika lenyewe to be registered, kisha njia anayokwenda, uimara wa bus lenyewe (safety check) na mengineyo mengi..
Kama mkuu wangu hujanielewa ktk mfano huu na ukajaribu kunambia kwamba vyama havina maana kuwepo hali unajua fika kwamba ndio utaratibu wa uchaguzi wetu leo hii. hakika wakati wa Nyerere wagom,bvea waliikuwa ni watu sio chama maanake wote walitoka CCM na kila mgombea alipewa alama ya nyumba au jembe. Mwenye shirika alikuwa CCM na huwezi kunambia sti maadam wagombea walikuwa watu binafsi basi hapa kuwepo na sababu ya kuwepo kwa CCM!.
Mkuu wangu itikadi ndio huunda Chama na kikapata wafuasi, hao wafuasi ndio huwa viongozi na wengine ni maamuma wanaochaguliwa u hata kupewa majukumu mengineyo. Na kwa kumalizia ni sawa na unananmbia kwamba maadam kila mmoja wetu anaamini Mungu basi hapakuwepo na sababu ya kuwa na dini, ukisahau kwamba dini zimetokana na wahi wa Mwenyezi Mungu ulowekwa ktk vitabu ambavyo ndivyo sote tunavifuata.
Nina hakika Chadema sii wajinga hivyo, hawa jamaa wamepitiwa file zao na kuonekana ni madereva wazuri ambao pengine wanakuja na wateja wao kama wale wasusi wa kizaire hapo Bongo. Tuwape support Chadema badala ya kutafuta makosa hali sisi wenyewe hatuna majibu sahihi.