Uchaguzi 2020 CHADEMA: Jeshi la polisi limeomba majina ya wagombea wetu

Uchaguzi 2020 CHADEMA: Jeshi la polisi limeomba majina ya wagombea wetu

CHADEMA

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
490
Reaction score
2,471
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taarifa kwa Umma

Jeshi la Polisi maeneo mbalimbali ya nchi yetu limepeleka barua kwa viongozi wetu ngazi za Wilaya wakiwataka kuwapelekea Majina ya Wagombea wetu ndani ya Chama wa nafasi ya Ubunge.

Barua hizo ambazo zimesainiwa na Wakuu wa Polisi wa Wilaya hazitaji sababu za kuhitaji Majina ya Wagombea wetu wala kuelezea Nia na misingi ya kisheria ya kutaka kupelekewa Majina hayo.

Kwa hatua za sasa tumewaelekeza viongozi wetu nchi nzima kuwa wasipeleke Majina hayo hadi hapo Polisi watakapotoa sababu na misingi ya kisheria za kuhitaji Majina ya watia Nia na Wagombea wa Chama chetu.

Pili tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi awachukulie hatua mara moja wakuu wa polisi wa Wilaya ambao wameandika barua hizo huku wakijua kuwa hawana mamlaka ya kisheria ya kuingilia michakato ya uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa.

Aidha tunamtaka IGP atengue barua hizo na aliongoze Jeshi la Polisi Kwa mujibu wa sheria na weledi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Octoba.

Mwisho tunaendelea kufuatilia kwa karibu hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Jeshi la Polisi dhidi ya watia nia na wagombea wetu maeneo mbalimbali nchini kama vile kuwakamata, kuwalaza mahabusu na wengine wanatakiwa kusalimisha magari yao binafsi Polisi bila kuelezea sababu za hatua hiyo.

Tunalitaka Jeshi la Polisi litimize wajibu wake kwa mujibu wa sheria za nchi yetu na liache Mara moja tabia ya kukandamiza Chama chetu kwa kushusha bendera za Chama chetu kama ilivyofanyika kule Same,Mkoani Kilimanjaro.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

Limetolewa Leo Alhamisi 16 Julai,2020.

1594907481197.png
 
Aisee.

Itabidi waombe na picha ya jesy zao mpya za CHADEMA ambazo zitatumika wakati wa kampeni!

Hakuna kumchekea mtu araaa!
 
swali 2: Siasa ni mchezo mchafu-elezea marks 20 Hili swali kipindi hicho tulikuwa tunashindwa kulielewa sijui kwa nini sasa hivi majibu yake unaweza jaza karatasi 5.
Siasa siyo mchezo mchafu sema watu wanapofanya siasa ndiyo wachafu.

Na siasa ikijaa watu wachafu inakuwa haina lengo la kuleta mabadiliko yoyote kwa wananchi zaidi ya kuiba Mali za umma tu
 
Hivi Chadema ni wa kuandika barua ya hivi kweli asee? Au ni mkakati wa kuichafua chadame ionekane kutoa tuhuma za ovyo?

Na kama ni kweli hii ni ya Chadema mbona hawakuweka ushahidi wa hizo barua za polisi zinazolalamikiwa hapa?

Wasipo ziweka hizo barua tutaamini kuwa hizo ni propaganda tu kama ilivyokuwa kwenye tukio la kupigwa na kuvunjwa kwa KUB huku watu wakitamka "tumetumwa kukuvunja mkuu na unamsumbua Rais".
 
Jamani wapeni Ili wachunguzwe nyendo zao, hatutaki kabisa rushwa.
 
Back
Top Bottom