Chadema jifunzeni Kenya Tume Huru ya Uchaguzi inavyopatika. Ruto ateua Watu 7 kuanzisha Mchakato na kumpeleka Majina kwa Uteuzi!

Chadema jifunzeni Kenya Tume Huru ya Uchaguzi inavyopatika. Ruto ateua Watu 7 kuanzisha Mchakato na kumpeleka Majina kwa Uteuzi!

Chadema wamekuwa wakiitolea mfano Tume ya Chebukati (IEBC) kama mfano wa Tume Huru ya Uchaguzi bora kabisa barani Africa

Chebukati na baadhi ya makamisha Muda wao umekwisha hivyo Rais Ruto ameunda timu ya Watu 7 kuanzisha Mchakato wa kupata Watendaji wapya wa IEBC

Kikosi Kazi hicho kitapendekeza majina yatakayofikishwa mbele ya Rais Ruto kwa Uteuzi

Chadema tumeni wataalamu wenu Nairobi wakajifunze ili mpate hoja za Katiba mpya

Kwaresma Njema!
Umechanganyikiwa, alafu bado unatoto mwingi
 
CHADEMA wamekuwa wakiitolea mfano Tume ya Chebukati (IEBC) kama mfano wa Tume Huru ya Uchaguzi bora kabisa barani Africa.

Chebukati na baadhi ya makamisha muda wao umekwisha hivyo Rais Ruto ameunda timu ya watu 7 kuanzisha Mchakato wa kupata Watendaji wapya wa IEBC.

Kikosi Kazi hicho kitapendekeza majina yatakayofikishwa mbele ya Rais Ruto kwa Uteuzi.

CHADEMA tumeni wataalamu wenu Nairobi wakajifunze ili mpate hoja za Katiba mpya.

Kwaresma Njema!
John, huwa unakimbilia kuanzisha nyuzi nyingi ambazo baadhi zake zanakosa maudhui yenye kuonyesha upo makini katika kuakisi uhalisia wa jambo ama hata kufikirisha na kuchokoza mijadala yenye kuvutia. Ni lazima utofautishe kuhusu muundo wa tume huru ya uchaguzi, utaratibu unaotumika kuteua timu ya makamishina, na pia maadili na weledi wa utendaji wa makamishina ni vitu vitatu ambavyo vipo tofauti kabisa.

Dai la CDM ni kuhusu katiba mpya na muundo wa tume ya uchaguzi ni kuwa wenye kuaminika katika kutenda haki, bila kujali utaratibu unaotumika kuwateua timu ya makamishina, isipokuwa maadili na weledi wao unapaswa kuwa usiokuwa na shaka yoyote mbele ya jamii.
 
CHADEMA wamekuwa wakiitolea mfano Tume ya Chebukati (IEBC) kama mfano wa Tume Huru ya Uchaguzi bora kabisa barani Africa.

Chebukati na baadhi ya makamisha muda wao umekwisha hivyo Rais Ruto ameunda timu ya watu 7 kuanzisha Mchakato wa kupata Watendaji wapya wa IEBC.

Kikosi Kazi hicho kitapendekeza majina yatakayofikishwa mbele ya Rais Ruto kwa Uteuzi.

CHADEMA tumeni wataalamu wenu Nairobi wakajifunze ili mpate hoja za Katiba mpya.

Kwaresma Njema!
Katiba mpya si kwa ajili ya CD tu.Tubadili mtazamo.
 
Hatua gani?

Mkiendelea na uwoga wenu hakuna Tume yoyote itakayowafaa
Tume huru ya uchaguzi ya Kenya ya Chebukati ilimtangaza Ruto kuwa Mshindi wa kiti cha URais japo Rais aliyekuwa madarakani Kenyatta alikuwa anamuunga mkono Raila Odinga. !! Hapo utaona ni kwa kiasi gani tume ipo huru !! Pamoja na mapungufu yake lakini ipo huru !!
 
Back
Top Bottom