Chadema jifunzeni Kenya Tume Huru ya Uchaguzi inavyopatika. Ruto ateua Watu 7 kuanzisha Mchakato na kumpeleka Majina kwa Uteuzi!

Umechanganyikiwa, alafu bado unatoto mwingi
 
John, huwa unakimbilia kuanzisha nyuzi nyingi ambazo baadhi zake zanakosa maudhui yenye kuonyesha upo makini katika kuakisi uhalisia wa jambo ama hata kufikirisha na kuchokoza mijadala yenye kuvutia. Ni lazima utofautishe kuhusu muundo wa tume huru ya uchaguzi, utaratibu unaotumika kuteua timu ya makamishina, na pia maadili na weledi wa utendaji wa makamishina ni vitu vitatu ambavyo vipo tofauti kabisa.

Dai la CDM ni kuhusu katiba mpya na muundo wa tume ya uchaguzi ni kuwa wenye kuaminika katika kutenda haki, bila kujali utaratibu unaotumika kuwateua timu ya makamishina, isipokuwa maadili na weledi wao unapaswa kuwa usiokuwa na shaka yoyote mbele ya jamii.
 
Katiba mpya si kwa ajili ya CD tu.Tubadili mtazamo.
 
Hatua gani?

Mkiendelea na uwoga wenu hakuna Tume yoyote itakayowafaa
Tume huru ya uchaguzi ya Kenya ya Chebukati ilimtangaza Ruto kuwa Mshindi wa kiti cha URais japo Rais aliyekuwa madarakani Kenyatta alikuwa anamuunga mkono Raila Odinga. !! Hapo utaona ni kwa kiasi gani tume ipo huru !! Pamoja na mapungufu yake lakini ipo huru !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…