CHADEMA: Kikosi Kazi kiliundwa ili kuchelewesha mchakato wa Katiba Mpya

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika ameitaka Serikali kuweka wazi gharama ambazo kikosi kazi kimetumia huku akisema hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi hicho kwa sababu kazi ya kutafuta maoni ya wananchi ilifanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Mnyika ameeleza hayo leo Jumamosi Oktoba 22, 2022 Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wananchi kuhusu demokrasia ya vyama vingi, kukabidhi ripoti yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika ripoti hiyo, kikosi kazi kimetoa mapendekezo 18 kwa Serikali ikiwemo kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, mchakato wa katiba mpya kuendelezwa na ruzuku kwa vyama vyote vya siasa.

Hata hivyo, Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo amri kwa Serikali kuyatekeleza. Alisisitiza kwamba wameyapokea na watayafanyia kazi hasa yale ambayo hayahusishi mabadiliko ya sheria.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mnyika amesema kikosi kazi hicho kiliundwa ili kuchelewesha mchakato wa katiba mpya na kwamba hilo limejidhihirisha kwenye mapendekezo waliyoyatoa.

Amesema maoni ya wananchi yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi kazi, bali wangerejea kwenye kitabu cha maoni ya wananchi kilichoandaliwa na Tume ya Warioba.

"Kuundwa kwa kikosi kazi ni matumizi mabaya ya fedha za Watanzania. Tunaitaka Serikali itoke hadharani ituambie kikosi kazi kimetumia fedha kiasi gani," amesema Mnyika.

Amesema walikuwa wakipigania kuruhusiwa mikutano ya hadhara lakini baada ya kuundwa kwa kikosi kazi waliamua kukipa muda ili waone matokeo yake, lakini wameshangazwa na kauli ya Rais Samia wakati akijibu hoja hiyo akisema kuna haja ya kufanyia mabadiliko sheria na kanuni kabla mikutano haijaruhusiwa.

"Tunaitaka Serikali iruhusu mikutano ya hadhara bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, bila kusubiri mabadiliko ya kanuni za mwaka 2019, bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Jeshi la Polisi.

"Zuio la mikutano ya hadhara ni haramu kwa sababu liko kinyume na Katiba ya nchi, liko kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa," amesema Mnyika.

Amesema wameshangazwa na kauli ya Rais Samia kwamba mapendekezo ya kikosi kazi siyo amri kwa Serikali, huku akisisitiza kwamba wanataka kujua gharama zilizotumiwa na kikosi kazi.

Mwananchi
 
JK alibuni mbinu hii ila naona imekwama.

Atakuja na agenda ya kuunda Tume ya kuchunguza mikutano ya kisiasa iweje Ili Muda uendelea kupita kufikia mwaka 2025 tuwe hatuna katiba mpya na uchaguzi umekatibia.

Siasa ni Mahesabu.
 
Katibu Makini wa Chama Makini Cha Siasa kuwahi kutokea katika Ukanda wa Maziwa Makuu, mwenye kumuweka Mungu Mbele Katika Kila Jambo.

Jiwe alihangaika sana kutaka Kumnunua na Kumtishia Ili aunge Mkono Juhudi kwenye ile Project yake Haramu ya Kununua Wapinzani Uchwara.

Mnyika alisimamia Msimamo wake madhubuti kabisa, Vitisho vya Jiwe vilijibiwa na Sala za Mnyika Kwa Israel Mtoa Roho kumuibukia Jiwe Kwa kutumia Corona
 
Mnyika ana hoja ya msingi sana.
Zijibiwe kifasana,ni maswali wengi wanajiuliza
Hoja yake imekuwa "overtaken by time". Kwa nini hakuhoji mapema, akangoja mpaka kikosi kimalize kazi ndiyo ahoji? Hoja yake itasaidi nini.
 
JK alibuni mbinu hii ila naona imekwama.

Atakuja na agenda ya kuunda Tume ya kuchunguza mikutano ya kisiasa iweje Ili Muda uendelea kupita kufikia mwaka 2025 tuwe hatuna katiba mpya na uchaguzi umekatibia.

Siasa ni Mahesabu.
Time hii hakuna Mahali watatorokea.

Bila TUME huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya hapatakuwa na UCHAGUZI wowote.

Amen.
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA amesema kuundwa kwa Kikosi Kazi ni matumizi mabaya ya fedha za Watanzania na hivyo Serikali itoke hadharani na iseme kimetumia fedha kiasi gani.

Mnyika ameongeza kuwa maoni ya wananchi kuhusu Katiba yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa Kikosi Kazi zaidi ya kurudi kwenye kitabu cha Maoni ya Mananchi kilichoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba.

Ripoti imetoa Mapendekezo 18 ikiwemo Kuruhusiwa Mikutano ya Kisiasa na Kuendelea Mchakato wa Katiba Mpya ingawa Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo Amri kwa Serikali.

========================

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ameitaka Serikali kuweka wazi gharama ambazo kikosi kazi kimetumia huku akisema hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi hicho kwa sababu kazi ya kutafuta maoni ya wananchi ilifanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Mnyika ameeleza hayo leo Jumamosi Oktoba 22, 2022 Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wananchi kuhusu demokrasia ya vyama vingi, kukabidhi ripoti yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika ripoti hiyo, kikosi kazi kimetoa mapendekezo 18 kwa Serikali ikiwemo kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, mchakato wa katiba mpya kuendelezwa na ruzuku kwa vyama vyote vya siasa.

Hata hivyo, Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo amri kwa Serikali kuyatekeleza. Alisisitiza kwamba wameyapokea na watayafanyia kazi hasa yale ambayo hayahusishi mabadiliko ya sheria.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mnyika amesema kikosi kazi hicho kiliundwa ili kuchelewesha mchakato wa katiba mpya na kwamba hilo limejidhihirisha kwenye mapendekezo waliyoyatoa.

Amesema maoni ya wananchi yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi kazi, bali wangerejea kwenye kitabu cha maoni ya wananchi kilichoandaliwa na Tume ya Warioba.

"Kuundwa kwa kikosi kazi ni matumizi mabaya ya fedha za Watanzania. Tunaitaka Serikali itoke hadharani ituambie kikosi kazi kimetumia fedha kiasi gani," amesema Mnyika.

Amesema walikuwa wakipigania kuruhusiwa mikutano ya hadhara lakini baada ya kuundwa kwa kikosi kazi waliamua kukipa muda ili waone matokeo yake, lakini wameshangazwa na kauli ya Rais Samia wakati akijibu hoja hiyo akisema kuna haja ya kufanyia mabadiliko sheria na kanuni kabla mikutano haijaruhusiwa.

"Tunaitaka Serikali iruhusu mikutano ya hadhara bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, bila kusubiri mabadiliko ya kanuni za mwaka 2019, bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Jeshi la Polisi.

"Zuio la mikutano ya hadhara ni haramu kwa sababu liko kinyume na Katiba ya nchi, liko kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa," amesema Mnyika.

Amesema wameshangazwa na kauli ya Rais Samia kwamba mapendekezo ya kikosi kazi siyo amri kwa Serikali, huku akisisitiza kwamba wanataka kujua gharama zilizotumiwa na kikosi kazi.

MWANANCHI
 
Chadema ni debe tupu
giphy.gif
 
Back
Top Bottom