Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ungekua na akili tungekushangaaCha msingi hakuna Tena watu wasiojulikana..,tujifunze kuona unafuu katika maisha haya..,Lile kundi lilikuwa hatari Sana mpaka watu tuliogopa kuweka maoni yetu katika mitandao ya kijamii..,hakuna serikali iliyokamilika asilimia mia Moja.., tujifunze kuwa na shukrani
Binafsi naona wale wanaoendelea kuisakama serikali ya rais Samia hata kwa makosa madogomadogo tu , wanasahau shida na mateso tuliyopewa na yule fashisti dikteta mwendakuzimu wa chato..,mungu katuokoa na kutuondolea Lile dubwana lakini lawama haziishii..,tuna kuwa kama Wana wa islaer katika safari ya nchi ya ahadi[emoji848]
Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Ujanja ni kujua nchi inaibiwa kimyakimya na mzanzibari? Nyie wajanja mmechukua hatua gani?Mama anaiba kimya kimya hataki kujulikana wajanja ndo tunajua
Hili halina uzito; lenye uzito na ambalo tayari Samia shaliweka kapuni ni "ruhusa"? ya kufanya mikutano.Pia Katibu Mkuu Mnyika ameitaka serikali kuweka wazi gharama ambazo kikosi kazi hicho kimetumia ili kukamilisha kazi yake .
Hela za umma zinapaswa kufahamika jinsi zinavyotumika
Kilianzishwa kinyemela. Kwa matakwa na hisia za raisKikosi Kazi cha Prof Mkandalla na Zitto Kabwe kilianzishwa kwa sheria?
Aiiiseeee!Kama haitoshi vile Mpokea taarifa anasema wataunda tume nyingine ndogo kushirikiana na baadhi ya waliokuwepo humo kuona wapi wafanye kazi. Huu ni upigaji wa Hela za walipa Kodi! Washauri wa mheshimiwa mwambieni hii sio sawa! Nini kinachoogopesha kutoifuata rasimu ya Warioba ambayo imechukua maoni nchi mzima na Kwa weledi na yeye mwenyewe akiwa mojawapo.
Duh!! Sasa John John Mnyika amekuwa CAG anafanya value-for-money audit? Leo anakishambuliaje KK huku CHADEMA walikataa kujiunga nacho wala kutoa maoni? Na anasifia Tume ya Warioba, why, si CHADEMA walitoka nje na kina mariasarungi? Manati ni pale anapotaka Bunge hili tulikwepe, eti lilikuwa ni Uchafuzi, na huku anamtaka Rais aanzishe mchakato. What a collection of rats, to be sure!
Bila shaka wewe ndio Sabaya ambaye ulitumika na mwendazake kutesa wananchiChadema ni debe tupu
Bila watu kufa hakuna kitakachofanyika. Afrika lazima damu, tena nyingi imwagike , jumuiya ya kimataifa iingilie ndiyo haki itatendeka. haya si rahisi kuyasikiliza CCM. But at present kupiga kelele ni muhimu sana maana ndiyo silaha iliyopo sasa ingawa ni sil;aha dhaifu! Kenya wako walivyo baada ya kufa wengi......Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika ameitaka Serikali kuweka wazi gharama ambazo kikosi kazi kimetumia huku akisema hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi hicho kwa sababu kazi ya kutafuta maoni ya wananchi ilifanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Mnyika ameeleza hayo leo Jumamosi Oktoba 22, 2022 Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wananchi kuhusu demokrasia ya vyama vingi, kukabidhi ripoti yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika ripoti hiyo, kikosi kazi kimetoa mapendekezo 18 kwa Serikali ikiwemo kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, mchakato wa katiba mpya kuendelezwa na ruzuku kwa vyama vyote vya siasa.
Hata hivyo, Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo amri kwa Serikali kuyatekeleza. Alisisitiza kwamba wameyapokea na watayafanyia kazi hasa yale ambayo hayahusishi mabadiliko ya sheria.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mnyika amesema kikosi kazi hicho kiliundwa ili kuchelewesha mchakato wa katiba mpya na kwamba hilo limejidhihirisha kwenye mapendekezo waliyoyatoa.
Amesema maoni ya wananchi yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi kazi, bali wangerejea kwenye kitabu cha maoni ya wananchi kilichoandaliwa na Tume ya Warioba.
"Kuundwa kwa kikosi kazi ni matumizi mabaya ya fedha za Watanzania. Tunaitaka Serikali itoke hadharani ituambie kikosi kazi kimetumia fedha kiasi gani," amesema Mnyika.
Amesema walikuwa wakipigania kuruhusiwa mikutano ya hadhara lakini baada ya kuundwa kwa kikosi kazi waliamua kukipa muda ili waone matokeo yake, lakini wameshangazwa na kauli ya Rais Samia wakati akijibu hoja hiyo akisema kuna haja ya kufanyia mabadiliko sheria na kanuni kabla mikutano haijaruhusiwa.
"Tunaitaka Serikali iruhusu mikutano ya hadhara bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, bila kusubiri mabadiliko ya kanuni za mwaka 2019, bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Jeshi la Polisi.
"Zuio la mikutano ya hadhara ni haramu kwa sababu liko kinyume na Katiba ya nchi, liko kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa," amesema Mnyika.
Amesema wameshangazwa na kauli ya Rais Samia kwamba mapendekezo ya kikosi kazi siyo amri kwa Serikali, huku akisisitiza kwamba wanataka kujua gharama zilizotumiwa na kikosi kazi.
Mwananchi
Na hizi hesabu za kisiasa pia wamezifanya 'kwa wale' wabunge 19Siasa ni Mahesabu.
Tusubiri mwaka uishe,huenda hii ikazidiwa na rubish nyingine ya funga mwakaBaada ya kusikiliza press conference ya Katiibu Miuu Chadema Hon. John Mnyika, nimeconclude kuwa ripoti ya the so called Prof Mkandara Ni another Professorial rubbish output of the year 2022.
Mungu wa mbinguni tuepushe na Rubbish Professors with their Professorial rubbish outputs.maana wanaongezeka kila uchao.