CHADEMA: Kikosi Kazi kiliundwa ili kuchelewesha mchakato wa Katiba Mpya

Huo ndio ukweli.
Katibu Mkuu wa CHADEMA amesema kuundwa kwa Kikosi Kazi ni matumizi mabaya ya fedha za Watanzania na hivyo Serikali itoke hadharani na iseme kimetumia fedha kiasi gani.

Mnyika ameongeza kuwa maoni ya wananchi kuhusu Katiba yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa Kikosi Kazi zaidi ya kurudi kwenye kitabu cha Maoni ya Mananchi kilichoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba.

Ripoti imetoa Mapendekezo 18 ikiwemo Kuruhusiwa Mikutano ya Kisiasa na Kuendelea Mchakato wa Katiba Mpya ingawa Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo Amri kwa Serikali.

========================

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ameitaka Serikali kuweka wazi gharama ambazo kikosi kazi kimetumia huku akisema hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi hicho kwa sababu kazi ya kutafuta maoni ya wananchi ilifanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Mnyika ameeleza hayo leo Jumamosi Oktoba 22, 2022 Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wananchi kuhusu demokrasia ya vyama vingi, kukabidhi ripoti yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika ripoti hiyo, kikosi kazi kimetoa mapendekezo 18 kwa Serikali ikiwemo kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, mchakato wa katiba mpya kuendelezwa na ruzuku kwa vyama vyote vya siasa.

Hata hivyo, Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo amri kwa Serikali kuyatekeleza. Alisisitiza kwamba wameyapokea na watayafanyia kazi hasa yale ambayo hayahusishi mabadiliko ya sheria.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mnyika amesema kikosi kazi hicho kiliundwa ili kuchelewesha mchakato wa katiba mpya na kwamba hilo limejidhihirisha kwenye mapendekezo waliyoyatoa.

Amesema maoni ya wananchi yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi kazi, bali wangerejea kwenye kitabu cha maoni ya wananchi kilichoandaliwa na Tume ya Warioba.

"Kuundwa kwa kikosi kazi ni matumizi mabaya ya fedha za Watanzania. Tunaitaka Serikali itoke hadharani ituambie kikosi kazi kimetumia fedha kiasi gani," amesema Mnyika.

Amesema walikuwa wakipigania kuruhusiwa mikutano ya hadhara lakini baada ya kuundwa kwa kikosi kazi waliamua kukipa muda ili waone matokeo yake, lakini wameshangazwa na kauli ya Rais Samia wakati akijibu hoja hiyo akisema kuna haja ya kufanyia mabadiliko sheria na kanuni kabla mikutano haijaruhusiwa.

"Tunaitaka Serikali iruhusu mikutano ya hadhara bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, bila kusubiri mabadiliko ya kanuni za mwaka 2019, bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Jeshi la Polisi.

"Zuio la mikutano ya hadhara ni haramu kwa sababu liko kinyume na Katiba ya nchi, liko kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa," amesema Mnyika.

Amesema wameshangazwa na kauli ya Rais Samia kwamba mapendekezo ya kikosi kazi siyo amri kwa Serikali, huku akisisitiza kwamba wanataka kujua gharama zilizotumiwa na kikosi kazi.

MWANANCHI
 
Nchi hii ina shida mingi sana... na nyingi zinaletanizwa na uchu wa mafaraka wa wana CCM wachache.

Wanajua fika kwamba Katiba mpya ndiyo msumari wao wa mwisho..hawatakubali kamwe.
Kweli
 
giphy.gif
Kwa mujibu wa ccm ni bora nchi ifilisike kwa ufisadi na wizi wa mali za umma kuliko Kuleta Katiba mpya
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA amesema kuundwa kwa Kikosi Kazi ni matumizi mabaya ya fedha za Watanzania na hivyo Serikali itoke hadharani na iseme kimetumia fedha kiasi gani.

Mnyika ameongeza kuwa maoni ya wananchi kuhusu Katiba yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa Kikosi Kazi zaidi ya kurudi kwenye kitabu cha Maoni ya Mananchi kilichoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba.

Ripoti imetoa Mapendekezo 18 ikiwemo Kuruhusiwa Mikutano ya Kisiasa na Kuendelea Mchakato wa Katiba Mpya ingawa Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo Amri kwa Serikali.

========================

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ameitaka Serikali kuweka wazi gharama ambazo kikosi kazi kimetumia huku akisema hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi hicho kwa sababu kazi ya kutafuta maoni ya wananchi ilifanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Mnyika ameeleza hayo leo Jumamosi Oktoba 22, 2022 Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wananchi kuhusu demokrasia ya vyama vingi, kukabidhi ripoti yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika ripoti hiyo, kikosi kazi kimetoa mapendekezo 18 kwa Serikali ikiwemo kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, mchakato wa katiba mpya kuendelezwa na ruzuku kwa vyama vyote vya siasa.

Hata hivyo, Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo amri kwa Serikali kuyatekeleza. Alisisitiza kwamba wameyapokea na watayafanyia kazi hasa yale ambayo hayahusishi mabadiliko ya sheria.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mnyika amesema kikosi kazi hicho kiliundwa ili kuchelewesha mchakato wa katiba mpya na kwamba hilo limejidhihirisha kwenye mapendekezo waliyoyatoa.

Amesema maoni ya wananchi yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi kazi, bali wangerejea kwenye kitabu cha maoni ya wananchi kilichoandaliwa na Tume ya Warioba.

"Kuundwa kwa kikosi kazi ni matumizi mabaya ya fedha za Watanzania. Tunaitaka Serikali itoke hadharani ituambie kikosi kazi kimetumia fedha kiasi gani," amesema Mnyika.

Amesema walikuwa wakipigania kuruhusiwa mikutano ya hadhara lakini baada ya kuundwa kwa kikosi kazi waliamua kukipa muda ili waone matokeo yake, lakini wameshangazwa na kauli ya Rais Samia wakati akijibu hoja hiyo akisema kuna haja ya kufanyia mabadiliko sheria na kanuni kabla mikutano haijaruhusiwa.

"Tunaitaka Serikali iruhusu mikutano ya hadhara bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, bila kusubiri mabadiliko ya kanuni za mwaka 2019, bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Jeshi la Polisi.

"Zuio la mikutano ya hadhara ni haramu kwa sababu liko kinyume na Katiba ya nchi, liko kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa," amesema Mnyika.

Amesema wameshangazwa na kauli ya Rais Samia kwamba mapendekezo ya kikosi kazi siyo amri kwa Serikali, huku akisisitiza kwamba wanataka kujua gharama zilizotumiwa na kikosi kazi.

MWANANCHI
Mama kaonja asali sasa anataka kuchonga mzinga. Madaraka ya kulevya.
 
Cha msingi hakuna Tena watu wasiojulikana..,tujifunze kuona unafuu katika maisha haya..,Lile kundi lilikuwa hatari Sana mpaka watu tuliogopa kuweka maoni yetu katika mitandao ya kijamii..,hakuna serikali iliyokamilika asilimia mia Moja.., tujifunze kuwa na shukrani

Binafsi naona wale wanaoendelea kuisakama serikali ya rais Samia hata kwa makosa madogomadogo tu , wanasahau shida na mateso tuliyopewa na yule fashisti dikteta mwendakuzimu wa chato..,mungu katuokoa na kutuondolea Lile dubwana lakini lawama haziishii..,tuna kuwa kama Wana wa islaer katika safari ya nchi ya ahadi[emoji848]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Pia Katibu Mkuu Mnyika ameitaka serikali kuweka wazi gharama ambazo kikosi kazi hicho kimetumia ili kukamilisha kazi yake .

Hela za umma zinapaswa kufahamika jinsi zinavyotumika
Kama haitoshi vile Mpokea taarifa anasema wataunda tume nyingine ndogo kushirikiana na baadhi ya waliokuwepo humo kuona wapi wafanye kazi. Huu ni upigaji wa Hela za walipa Kodi! Washauri wa mheshimiwa mwambieni hii sio sawa! Nini kinachoogopesha kutoifuata rasimu ya Warioba ambayo imechukua maoni nchi mzima na Kwa weledi na yeye mwenyewe akiwa mojawapo.
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA amesema kuundwa kwa Kikosi Kazi ni matumizi mabaya ya fedha za Watanzania na hivyo Serikali itoke hadharani na iseme kimetumia fedha kiasi gani.

Mnyika ameongeza kuwa maoni ya wananchi kuhusu Katiba yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa Kikosi Kazi zaidi ya kurudi kwenye kitabu cha Maoni ya Mananchi kilichoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba.

Ripoti imetoa Mapendekezo 18 ikiwemo Kuruhusiwa Mikutano ya Kisiasa na Kuendelea Mchakato wa Katiba Mpya ingawa Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo Amri kwa Serikali.

========================

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ameitaka Serikali kuweka wazi gharama ambazo kikosi kazi kimetumia huku akisema hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi hicho kwa sababu kazi ya kutafuta maoni ya wananchi ilifanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Mnyika ameeleza hayo leo Jumamosi Oktoba 22, 2022 Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wananchi kuhusu demokrasia ya vyama vingi, kukabidhi ripoti yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika ripoti hiyo, kikosi kazi kimetoa mapendekezo 18 kwa Serikali ikiwemo kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, mchakato wa katiba mpya kuendelezwa na ruzuku kwa vyama vyote vya siasa.

Hata hivyo, Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo amri kwa Serikali kuyatekeleza. Alisisitiza kwamba wameyapokea na watayafanyia kazi hasa yale ambayo hayahusishi mabadiliko ya sheria.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mnyika amesema kikosi kazi hicho kiliundwa ili kuchelewesha mchakato wa katiba mpya na kwamba hilo limejidhihirisha kwenye mapendekezo waliyoyatoa.

Amesema maoni ya wananchi yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa kikosi kazi, bali wangerejea kwenye kitabu cha maoni ya wananchi kilichoandaliwa na Tume ya Warioba.

"Kuundwa kwa kikosi kazi ni matumizi mabaya ya fedha za Watanzania. Tunaitaka Serikali itoke hadharani ituambie kikosi kazi kimetumia fedha kiasi gani," amesema Mnyika.

Amesema walikuwa wakipigania kuruhusiwa mikutano ya hadhara lakini baada ya kuundwa kwa kikosi kazi waliamua kukipa muda ili waone matokeo yake, lakini wameshangazwa na kauli ya Rais Samia wakati akijibu hoja hiyo akisema kuna haja ya kufanyia mabadiliko sheria na kanuni kabla mikutano haijaruhusiwa.

"Tunaitaka Serikali iruhusu mikutano ya hadhara bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, bila kusubiri mabadiliko ya kanuni za mwaka 2019, bila kusubiri mabadiliko ya Sheria ya Jeshi la Polisi.

"Zuio la mikutano ya hadhara ni haramu kwa sababu liko kinyume na Katiba ya nchi, liko kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa," amesema Mnyika.

Amesema wameshangazwa na kauli ya Rais Samia kwamba mapendekezo ya kikosi kazi siyo amri kwa Serikali, huku akisisitiza kwamba wanataka kujua gharama zilizotumiwa na kikosi kazi.

MWANANCHI
Duh!! Sasa John John Mnyika amekuwa CAG anafanya value-for-money audit? Leo anakishambuliaje KK huku CHADEMA walikataa kujiunga nacho wala kutoa maoni? Na anasifia Tume ya Warioba, why, si CHADEMA walitoka nje na kina mariasarungi? Manati ni pale anapotaka Bunge hili tulikwepe, eti lilikuwa ni Uchafuzi, na huku anamtaka Rais aanzishe mchakato. What a collection of rats, to be sure!
 
Kama haitoshi vile Mpokea taarifa anasema wataunda tume nyingine ndogo kushirikiana na baadhi ya waliokuwepo humo kuona wapi wafanye kazi. Huu ni upigaji wa Hela za walipa Kodi! Washauri wa mheshimiwa mwambieni hii sio sawa! Nini kinachoogopesha kutoifuata rasimu ya Warioba ambayo imechukua maoni nchi mzima na Kwa weledi na yeye mwenyewe akiwa mojawapo.
Mama naona anaweza kutumia Imani yetu kwake na kutibia pesa nyingi sana kuliko zile 2.4T za jpm.
 
Mnyika ameongeza kuwa maoni ya wananchi kuhusu Katiba yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa Kikosi Kazi zaidi ya kurudi kwenye kitabu cha Maoni ya Mananchi kilichoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba
Mtu yeyote anayekwepa ukweli huu atakuwa mnafiki
 
Back
Top Bottom