CHADEMA: Kikosi Kazi kiliundwa ili kuchelewesha mchakato wa Katiba Mpya

Ni wivu tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16]
 
Ungekua na akili tungekushangaa
 
Pia Katibu Mkuu Mnyika ameitaka serikali kuweka wazi gharama ambazo kikosi kazi hicho kimetumia ili kukamilisha kazi yake .

Hela za umma zinapaswa kufahamika jinsi zinavyotumika
Hili halina uzito; lenye uzito na ambalo tayari Samia shaliweka kapuni ni "ruhusa"? ya kufanya mikutano.

Ni sheria zipi zinazohitaji marekebisho ndipo vyama vianze kufanya mikutano? Hizi si ndiyo mbinu za ucheleweshaji tunazozizungumzia kaila mara humu?
 
Aiiiseeee!

"Upigaji wa hela za walipa kodi", ni jambo moja, pengine lisilo na uzito zaidi ya jambo zito zaidi..., la kucheza danadana na kupoteza muda, tena kwa maksudi mazima!

Mama wala hapepesi macho, wala kuona aibu kwa hadaa za aina hii anazozitoa mbele za watu wenye akili vichwani mwao.
 
Matumizi mabaya kabisa ya fedha, haiwezekani unaunda kikosi kazi kwa ajili ya kukuletea mapendekezo ya nini kifanyike kuhusu mambo kadhaa, halafu ukishapewa mapendekezo unasema tena mtaenda kupitia sheria [mikutano ya siasa].

Matokeo yake wamepoteza pesa kwenye kikosi kazi, na wataenda kupoteza pesa nyingine kwenye kupitia sheria.
 

Umeelewa alichozungumza J.J. Mnyika!!?!
Anasema kulikuwa na umuhimu gani wa kikosi kazi kukusanya maoni wakati Tume ya Warioba ilishamaliza kila kitu na kufikia hatua ya kuwa na Bunge la Katiba!!??

Kwani CDM & Co. walitoka nnje ya Bunge la Katiba kwa sababu ya Tume ya Warioba au kwa sababu ya sarakasi za mule bungeni!!??

Jitahidi uwe na taarifa sahihi na uzielewe kabla ya kuandika upotoshaji.
 
Bila watu kufa hakuna kitakachofanyika. Afrika lazima damu, tena nyingi imwagike , jumuiya ya kimataifa iingilie ndiyo haki itatendeka. haya si rahisi kuyasikiliza CCM. But at present kupiga kelele ni muhimu sana maana ndiyo silaha iliyopo sasa ingawa ni sil;aha dhaifu! Kenya wako walivyo baada ya kufa wengi......
 
Hawa ni maproffessors wa majalalani,eti vyama vya siasa vipate ruzuku Sawa this is craze, chama Chenye 0 MP kipate ruzuku Sawa na chama chenye 50MPs,hawa wanatuchezea sana maana kuna hatari ya kufumuka kwa utitiri wa vyama ili wapate free ruzuku, kupata ruzuku political parties lazima watoe jasho, nilitegemea wangekuja na azimio la kuvitaka vyama vya siasa kutangaza hadharani vyanzo vyao vya mapato, Nina wasiwasi ccm inatumia fedha za serikali kuendesha chama
 
Baada ya kusikiliza press conference ya Katiibu Mkuu Chadema Hon. John Mnyika, nimeconclude kuwa ripoti ya the so called Prof Mkandara Ni another Professorial rubbish output of the year 2022.

Mungu wa mbinguni tuepushe na Rubbish Professors with their Professorial rubbish outputs.maana wanaongezeka kila uchao.
 
Tusubiri mwaka uishe,huenda hii ikazidiwa na rubish nyingine ya funga mwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…