Nakubaliana na wewe kwamba Serikali, nakunuu iboreshe kwanza mazingira ya watu kuwa na uchumi mzuri ili ipate kodi kwa wingi vitu vipatikane.
Pia nakubaliana na wewe kwamba, nanukuu serekali inategemea kodi kutoka kwa watu.
Sikubaliani nawe ili kuboresha mazingira ya watu kiuchumi, nikikunukuu serikali ianze na ajira, kupunguza gharama za pembejeo, matibabu nafuu, kupunguza gharama ya zana za uvuvi, na dawa za mifugo nk. Hayo uliyotaja ni matokeo ya kukua kwa uchumi wa nchi
Kwa mfano:
√ Mwajiri mkuu hadi sasa, kwa nchi zinaxoendelea ni Serikali. Je, itaweza kuajiri watumishi wangapi wakati inapaswa kuwa ba gharama ndogo za kujiendesha?
√ Hivyo basi, mwajiri mkuu anapaswa kuwa Sekta binafsi;
√ Kwa msingi huo Serikali inapaswa kuweka mazingira rafiki na wezeshi ya sekta binafsi kujenga uchumi wa Taifa na kukua;
√ Mazingira rafiki na wezeshi kwa sekta binafsi ni Sera, Sheria, na Kanuni za uwekezaji, pamoja na miundombinu iliyo bora na imara hasa ya usafirishaji, nishati na maji.
Utekelezaji wa Ilani ya CCM, 2015, kwa kiasi kikubwa imeweza kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji kwa sekta binafsi. Ni kwa sababu hiyo makusanyo ya kodi yanaongezeka kila mwezi, kutoka bilion 800, mwaka 2015 hadi trilioni 1.8, mwaka 2020. Hiki ni kipindi cha Serikali ya awamu ya 5 inayomaliza muda wake.