Uchaguzi 2020 CHADEMA kufungua kesi kwa ajili ya kumtafuta aliyesaini Barua ya NEC inayohusu majina ya Viti Maalum

Majibu kutoka tume 2021 majibu ya forgery kutoka polisi 2022 kama ikitokea ikiwa kesi .kesi itaendelea mahakamani .hukumu 2025 ,my chadema msipoteze muda bure .tumieni maarifa .wacha wabunge wapige kazi .Na anzeni kudai katiba mpya ile ile iliopitishwa na ccm .ipigiwe kura angalau inayo tume huru na inampunguzia Rais madaraka,
 
Ni hatua nzuri,hiki ndio chama pekee makini cha upinzani kilichobaki Tanzania kwa sasa
Chama kipi mkuu, Unajua Tundu Lissu alifanya nini baada ya kufika belgium kwenye interview yake ya mwanzo? "Alimtaka Rais Magufuli ashirikiane na upinzani kuunda umoja- Sasa kwa kauli hii TL amemtambua Rais Magufuli ata akina Halima mdee hawajaenda bungeni kuapa. Ninachojifunza kwenye mambo haya wanasiasa ni watu wanafiki sana, zaidi ya sana.

Wao siku zote huwatumia wananchi kutekeleza malengo yao, Lissu alipokuwa akiutaka urais alipanda Ndege toka Belgium hadi Tanzania na akapokewa kwa maandamano pale airpot regardless waliompiga risasi bado hawajakamatwa., Alifanya kampeni usiku na mchana akiwa salama bila kudhuriwa mahali popote na hao watu wasiojulikana. Lakini mara baada ya uchafuzi alikimbilia ubalozi eti anataka kuuliwa na mtu aliyempigia simu kwamba ameagizwa kumuua na hatimae akarudi begium bila kutathmini watu waliokuwa wakimuunga mkono waliokuwa na mategemeo naye wamepata ushirikiano gani kutoka kwa kiongozi huyo ambaye yeye ndio anatakiwa atoe fatwa azijuazo kuwa pamoja na wananchi.

Na sasa nimemuamini Magufulikwenye kampeni zake alisema Lissu tayari ana visa ya kuishi belgium anataka kuwatumieni halafu yeye achomoke arudi zake belgium watu waendelee kuumia. Ndivyo sura halisi sasa inaonekana.

Yeye anadai hawezi kuja Tz sababu antaka kuuliwa sasa vipi ataiongoza Tz siku moja akiwa rais ilhali hawezi kurudi ama atawaongoza Watanzania online yeye akiwa belgium?
 
Chadema wanakosea sana kwenda mahakamani. Wabaki na msimamo wao wa kuwafukuza akina Mdee, halafu ukweli ujulikane katika baraza kuu ambapo rufaa itasikilizwa, Maana hapo Mdee atasema fomu aliletewa na nani.
Mahakama itawaumiza sana na hatapata jibu manalofikiria kulipata
 
Yeye anadai hawezi kuja Tz sababu antaka kuuliwa sasa vipi ataiongoza Tz siku moja akiwa rais ilhali hawezi kurudi ama atawaongoza Watanzania online yeye akiwa belgium?
akiwa Rais atakuwa na ulinzi kuzidi ule aliokuwa nao wakati wa kampeni
 
Dar es Salaam. CHADEMA imeanza kutumia nguvu ya mahakama kupinga mchakato wa uteuzi wa wabunge 19 wa viti maalumu na mtu aliyesaini fomu zao kwa nafasi ya katibu mkuu.
Wanataka kuvunja katiba kwa kutumia mahakama sasa!
 
Nongwa tu?...mbona hawamshughulikii yule wa Nkasi?Kuna madiwani wengi tu wameapa
 
Katika barua hiyo kwa NEC, alisema CHADEMA inataka kupatiwa nakala ya barua iliyowasilisha majina pamoja na fomu namba 8D ambazo katibu mkuu anatakiwa kujaza ili ijulikane aliyeijaza na hivyo aunganishwe kwenye kesi hiyo.
safi, kama wakigoma kuitoa hiyo form namba 8D wataitolea mahakamani.
 
Mkuu,

Are they filing a case to challenge a non-existent defaulter? This might be a guise phenomenon of the 21st century to surface on planet earth.
Mkuu: hapa kuna hesabu za permutations, how many pairs can you make out of 19 names? Tundulissu yuko mbioni kuwatafutia hifadhi Canada na Nairobi ba EU. Ilu kuongeza dau Halima atengeneze hifadhi 15, Esta A 10, Esta B 10, yule Mnyantuzu naye 10, na aliyenajinsi wimbo wa taifa naye 10 na waliobaki tano tano. CHADEMA wanataka kuitumia nafasi hii waende Canada na kupewa ruzuku watakayoipoteza iwapo "The 19 Ndungai Heroines" watashinda, of course na legal fees za kibatala. Relax, hawa ni Waarabu wa Pemba hujuaba kwa vilemba.
 
Hiyo kesi CDM waliyoifungua wakitaka wamfahamu aliyesaini barua ya kuidhinisha wabunge wa viti maalumu imeishia wapi huku wabunge 19 wakikata rufaa na hoja zao kukubalika kwenye mamlaka ya chama?

*Kitu gani kimetokea? Every talkative and provocative person against others accusing of betrayal is a chameleon to trust
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…