Mjinga wewe, mimi ni Mfwasi wa Bwana Yesu. Mungu wa Mbinguni aliye jivika uwanadamu ili aishi kati yetu wanadamu hapa duniani na atukomboe kutoka kifo cha milele yote . Kilicho sababishwa na dhambi. Akawambwa Msalabani Akafa, Akazikwa na siku ya tatu Akafufuka kutoka kwa wafu. Akashinda kaburi na kifo.
Ufuasi wangu kwa Yesu usinge kuwa na maana yeyote kama asinge fufuka. Na kama Damu yake isingemwagika pale Msalabani bado ningekuwa na tegemea damu za ndege na wanyama kondoo, mbusi, ngombe na ngamia kutoa kafara. Lakini kwa Damu yake ya Thamani Kuu kushinda hizi nyingine zote ambazo zimegeuka kuwa ni najisi kwa kuinajisi ardhi na nchi ya Huyu Mwanadamu Yesu imeniweka Huru KweliKweli.
Kuongea yanayo fanana na Gwajima sio kigezo unachoweza kunifanya mimi kuwa mfwasi wake. Itoshe tu kujua Mungu wa Mbinguni alishaniepusha naye. Bali anapoongea kweli kuwa uhiari wa chanjo na uheshimiwe na yeyote yule elewa fika kwamba hapo tutaongea lugha moja na yeye.