CHADEMA kushiriki Uchaguzi wa Diwani Handeni

CHADEMA kushiriki Uchaguzi wa Diwani Handeni

Shida yako ndio hiyo. Unaamini kushiriki ni kugombea tu. Kiongozi wa Chama akimpigia debe mgombea wa chama kingine ni ishara kuwa hicho chama kimeshiriki. Tutajuaje kuwa ni makubaliano kati ya vyama ya kupeana sapatin pale ambapo chama kingine kina nguvu zaidi? Chadema ilishiriki uchaguzi Zanzibar ingawa ilikuwa inampigia debe mgombea wa chama kingine. Kuendekeza tabia kama hizi ndio kutapelekea watu kujitokeza na kugombea kwa niaba ya Chadema katika uchaguzi ujao hata kama uongozi wa juu utasema hawashiriki.

Amandla.....

Ndio nikakuelewesha kwamba CHADEMA Kama taasisi haishiriki huo uchaguzi, ni individual kwa mapenzi yake kaamua kuipigia kampeni CUF. Halafu huyo jamaa ni katibu kweli wa CHADEMA?. Maana imeandikwa tu katibu na haijulikani ni katibu wa wapi?
 
Chadema twitter mara ya mwisho kuwa updated ni masaa 19 iliyopita kwa clips za presa ya Mwaitenda. Kabla ya hapo wametuambia kuwa Freeman anaenda Marekani. Kabla ya hapo ni wakina Lissu wako Ulaya. Na clip za Celestine Simba. Na ya ziara ya Heche Mtama. Haina tofauti na ya CCM kwa ku prioritize viongozi wake wa juu tu. Habari zinazohusu wanachama wake wa kawaida ni chache. Ukitaka kujua kuwa wanaendelea kujenga ofisi zao nenda kwa wakina Maria. Ukitaka kujua kuwa kuna watu wanapitia wakati mgumu nchini nenda tena kwa wanaharakati. Hivi karibuni wameweka clip ya msichana aliyepigwa na DC. Waziri Gwajima amejitokeza akilaani kitendo hicho na kusema kuwa wanampa msaada aliyepigwa lakini Chadema, Bawacha na Bavicha kimyaa.

Amandla...

Kafanya kosa mkuu wa Wilaya wa CCM unataka CHADEMA wafanyeje Tena. Si waziri ndio wa kulifanyia kazi?. Unailaumu CHADEMA as if ndio inayoendesha serikali be real.
 
Kote ni mtandaoni. Chadema kwenye taarifa za kwenye mtandao wako nyuma sana. Kaangalie lini wame update hiyo unayoiita official page. Ukweli ni kuwa kinachowasaidia Chadema mtandaoni ni kurasa za wakina Maria, Fatma, MM n.k. Hata wakati wa kesi ya Freeman taarifa zilikuwa zinapatikana kwa MM na sio kwao.

Amandla...

Acha uongo maria na fatma sio CHADEMA. CHADEMA Wana social media nyingi kuanzia Kanda, CHADEMA in blood na CHADEMA Taifa.
 
Kwa hiyo Chadema inaogopa kuwachukulia hatua wanachama wake kwa kuhofia serikali itawatetea? Are you serious?
Alama za nyakati ni kuwa udhabiti wa msimamo wenu unapimwa. Hawa hawa watagombea kwa niaba yenu 2025 na mtajitetea tena kuwa hamna cha kuwafanya kwa sababu watatetewa naa serikali.

Amandla....

Uwe mwelewa, CHADEMA ikiwachukulia hatua serikali inakuja kuwakingia kifua na kuwatetea.
 
Chadema ndio wanajua kama ni Katibu wao au sio. Chadema imesema haitashiriki katika uchaguzi na haijasema kuwa haitaweka mgombea. Kushiriki ni zaidi ya kuweka mgombea.

Amandla...

Ndio nimekuambia usilazimishe matakwa ya mtu binafsi kuwa ya chama. Chama kimesema hakishiriki akatokea mwehu akajiita ni CHADEMA akashiriki, hapo utakilaumu chama?. Chama kilishatoa msimamo wake.
 
Nimeona mahali mtu aliyetambulishwa kama Katibu wa CHADEMA Handeni, Kombo Matulu akihimiza wananchi wakampigie kura mgombea wa CUF.

Inaelekea CHADEMA wamebadilisha msimamo wao kuhusu kutoshiriki katika katika uchaguzi wowote mpaka Katiba mpya itakapopatikana.

Amandla.

Punguza utoto dogo.
 
Ndio nimekuambia usilazimishe matakwa ya mtu binafsi kuwa ya chama. Chama kimesema hakishiriki akatokea mwehu akajiita ni CHADEMA akashiriki, hapo utakilaumu chama?. Chama kilishatoa msimamo wake.
Naona huelewi. Mtu akijitambulisha kama mgombea wa Chadema halafu Chadema ikamuangalia tu kwa sababu iliisha toa tamko awalu basi hicho kisishangae kulaumiwa. Ni kama vile tunavyoilaumu CCM panapotekeza shabiki wake akifanya fujo ( na wao wakakaa kimya) ingawa wao kama chama wanahubiri utulivu na amani kila siku.

Amandla...
 
Uwe mwelewa, CHADEMA ikiwachukulia hatua serikali inakuja kuwakingia kifua na kuwatetea.
Swali liko pale pale. Kwa hiyo Chadema haiwachukulii hatua kwa vile serikali itawakingia kifua na kuwatetea? Kama ni hivyo basi hawastahili kuitwa chama cha upinzani.
Amandla...
 
Nimeona mahali mtu aliyetambulishwa kama Katibu wa CHADEMA Handeni, Kombo Matulu akihimiza wananchi wakampigie kura mgombea wa CUF.

Inaelekea CHADEMA wamebadilisha msimamo wao kuhusu kutoshiriki katika katika uchaguzi wowote mpaka Katiba mpya itakapopatikana.

Amandla.
Maelezo yako yanaonyesha moja kwa moja kuwa Chadema haishiriki Uchaguzi huo, tungekuelewa kama ungeandika kuwa Chadema yasimamisha mgombea.


Huyo unayemwita Katibu wa Chadema, kama ni kweli, yeye kwa maandishi yako unatuonyesha kuwa ananadi mgombea wa CUF na si Chadema. Mawimbi ya ufahamu yametikisikia wapi ndg yangu
 
Chama kinastahili lawama maana hakiwachukulii hatua watu kama hawa. Msimamo wake kuhusu wale waliokubali matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 hauko wazi. Chadema haijaweka wazi msimamo wake kuhusu madiwani na mbunge wake ambao wanakiwakilisha kwenye Halmashauri na Bungeni. Ndio maana watu kama hawa wameanza kujitokeza na watashiriki kwenye chaguzi za 2024 na 2025 bila kujali msimamo wa chama chao.

Amandla...

..tunaweza ku-suggest wafukuzwe, halafu mamlaka zikawakingia kifua kama ilivyofanyika kwa Halima na wenzake.
 
CCP sasa wanahaha kuwarubuni CHADEMA washiriki uchafuzi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
..tunaweza ku-suggest wafukuzwe, halafu mamlaka zikawakingia kifua kama ilivyofanyika kwa Halima na wenzake.
Kwa hiyo mnajuta kuwafukuza wakina Halima kwa sababu bado wako Bungeni? Mimi nadhani mmejijengea heshima kwa kuwafukuza kuliko kama mngebaki nao. Mamlaka inaweza kuwakingia kifua lakini haiwezi kuwarudishia uanachama. Hicho ndio cha msingi.
Amandla...
 
Back
Top Bottom