Uchaguzi 2020 CHADEMA kutobandika picha za Tundu Lissu ni kosa la kiufundi

Na wengine wanajamba majukwaani wakati wa kuomba kura.
Kila mwenye akili timamu anajua Lissu anafananaje iwe Kijijini au mjini.
CCM wameweka mabango ya wagombea wao ila bado wanapiga magoti, wanakuna nazi jamvini, wanajigaragaza chini bila kusahau wanaosha masufuria kwenye misiba so hii imekaa vipi?
 
Lissu ni habari nyingine yani machine ingine kabisa wapiga kura wote wana mjuwa kuliko wanavyo mjuwa magufuli
 
Hali ya kifedha mbaya?. Zimeenda wapi ruzuku, na michango ya wadau?. Chama saccos kimejaa ubadhilifu wa kutisha, huku mwenyekiti wenu akichekacheka tu. Watanzania wanawatazama mnavyojikanyaga.
Iyo hela ya mboga,unaitolea macho sababu ya umaskini wako ulioletwa na cscsmm
 
CCM wameweka mabango ya wagombea wao ila bado wanapiga magoti, wanakuna nazi jamvini, wanajigaragaza chini bila kusahau wanaosha masufuria kwenye misiba so hii imekaa vipi?

CCM wanasema "mtaka cha uvunguni sharti kuinama", lakini CHADEMA mnasema "mtaka cha uvunguni nyanyuwa matanda". Kaeni ni kiburi chenu tuone kama mtapata kura za kutosha.
 
Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni kuhusu uchaguzi huu. Hii pia imechangiwa na wengi wenu kunitumia PM kuniomba nitoe maoni yangu kuhusu mwenendo wa uchaguzi huu. Nimekubali kufanyia kazi maombi ya wengi.

Niseme kwamba kampeni hizi za mwaka huu ni za kipekee. Ziko tofauti sana. Wapiga kura wengi kwa sasa wana akili nyingi sana na hawasikilizi blah blah. Ilishazoeleka wagombea kutamka uongo ulio wazi na ahadi nyingi hewa ila kwa mwaka huu inaonekana kabla mgombea hajatamka kitu inabidi ajifikirie mara nyingi sana. Watu wanataka maelezo ya kina. Kwahiyo hakuna Chama chenye wakati mrahisi tunapoiendea tar 28 Octoba.

CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kimeonyesha kuleta changamoto kwenye uchaguzi huu hasa baada ya kupata mgombea jasiri na ambaye inaonekana wazi hakuna anachohofia. Chama hicho kina mtaji mkubwa wa kura za huruma kutoka kwa watu wanaoamini kuwa Lisu alitendewa ubaya na CCM. Bahati nyingine ya hivi karibuni ambayo inaweza kuwaongezea kura za huruma ni hiki kitendo cha NEC kumsimamisha Lisu kufanya kampeni kwa siku 7. Tukiachana na kura za huruma ni wazi CHADEMA watapata kura chache kutoka makundi mengine ya wananchi.

Kosa la kiufundi ambalo CHADEMA wamelifanya na litawagharimu kwenye sanduku la kura tar 28 ni kutobandika picha za mgombea wao kama walivyofanya vyama vingine. Ikumbukwe Lissu amekaa nje ya nchi kwa miaka kadhaa na alikuwa adimu machoni mwa wapiga kura. Au chama kimesahau kwenye karatasi ya kupigia kura kuna picha za wagombea? Mabango kwa watu wa marketing watakubaliana nami ni nyenzo kubwa sana kwenye kuitangaza bidhaa. Mtu asiyejua kusoma itamsaidia sana kwenye kupiga kura. Watu kama wahadzabe mngekuwa mmewarahisishia sana.

Mimi nionavyo ndani ya CHADEMA kuna ambao kwa makusudi waliamua kumhujumu Lisu kwa kutoweka mabango. Au pia watu hao wameona tu Rais Magufuli anatosha kwahiyo wamsaidie kinamna. Ombi langu kwa Rais JPM asimsahau Mh Tundu Lissu kwenye teuzi za serikali yake ijayo.
 
chama hakina fedha
 
Hivi ni nani anayesema kuwa chama kuu kina watu makini kuliko chadema. Mimi si mwamachama wa chama chochote lakini mara nyimgi nimeona kuwa wanachama wa chadema hata vijana wao wamekuwa na akili zaidi katika maongezi yao kuliko wa chama kuu. Wa chama kuu kazi yao ni kujisifu tu na kuamimi kuwa wao watapita tu kwa imani ya kuhodhi vyombo na taasisi zote za usalama wa taifa pamoja na NEC!
 
Ni kweli ila siku hizi hakuna anayeangalia bangos popote ! Watu wanaangalia picha kwenye simu zaidi!
 
Za mr G zimejaa kila mahali Kawe lakini kila moja anamzungumzia Halima!! Labda waibe kura!
 
Hivi unawezaje kusema ruzuku itatosha shughuli zote za chama! Mleta mada ni sahihi lakini unadhani kuwa ccm wanatumia ruzuku kwenye election??????????? Be fair!!!!
 
Please do not compare ccm na chama cho chote! Kila moja anajua kuwa wanatumia kodi zetu kwenye mambo mengi ya elevtion ! You know it! God knows it! I knowbit and everybody knows it!
 
Hali ya kifedha mbaya?. Zimeenda wapi ruzuku, na michango ya wadau?. Chama saccos kimejaa ubadhilifu wa kutisha, huku mwenyekiti wenu akichekacheka tu. Watanzania wanawatazama mnavyojikanyaga.
Unautumia uhuru wako wa kutoa maoni kipumbavu sana, no wonder kichwa chako kina kamasi tu ndiyo maana unaongea huu ujinga. CHADEMA ni taasisi imara sana, kwa taarifa yako CCM inatumia kodi zetu kuendesha campaign zake, inatumia pesa za kwenye mifuko ya mafao kuendesha campaigns zake, inatumia NEC kuomba pesa kwenye mashirika binafsi kwa ajili ya kuendeshea campaigns zake, na zaidi ni kutumia vyombo vyote vya dola kwa ajili ya kuhakikishiwa kinarudi tena madarakani. Bahati mbaya tu Jf imetoa wigo hadi vilaza kama wewe kuongea hata ujinga otherwise hukutakiwa kuwa humu kabisa!
 
Rais Magufuli amteue kwenye nyadhifa itakayomfaa. Lissu kazungukwa na watu wenye uwezo mdogo mno kwenye kufikiria. Uchaguzi ukiisha ajiunge CCM kwa wasomi wenzake.
Hii comment yako imeshaonyesha upande wako ulipo izo zingine ni polojo tu
 
Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni kuhusu uchaguzi huu. Hii pia imechangiwa na wengi wenu kunitumia PM kuniomba nitoe maoni yangu kuhusu mwenendo wa uchaguzi huu. Nimekubali kufanyia kazi maombi ya wengi.

Niseme kwamba kampeni hizi za mwaka huu ni za kipekee. Ziko tofauti sana. Wapiga kura wengi kwa sasa wana akili nyingi sana na hawasikilizi blah blah. Ilishazoeleka wagombea kutamka uongo ulio wazi na ahadi nyingi hewa ila kwa mwaka huu inaonekana kabla mgombea hajatamka kitu inabidi ajifikirie mara nyingi sana. Watu wanataka maelezo ya kina. Kwahiyo hakuna Chama chenye wakati mrahisi tunapoiendea tar 28 Octoba.

CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kimeonyesha kuleta changamoto kwenye uchaguzi huu hasa baada ya kupata mgombea jasiri na ambaye inaonekana wazi hakuna anachohofia. Chama hicho kina mtaji mkubwa wa kura za huruma kutoka kwa watu wanaoamini kuwa Lisu alitendewa ubaya na CCM. Bahati nyingine ya hivi karibuni ambayo inaweza kuwaongezea kura za huruma ni hiki kitendo cha NEC kumsimamisha Lisu kufanya kampeni kwa siku 7. Tukiachana na kura za huruma ni wazi CHADEMA watapata kura chache kutoka makundi mengine ya wananchi.

Kosa la kiufundi ambalo CHADEMA wamelifanya na litawagharimu kwenye sanduku la kura tar 28 ni kutobandika picha za mgombea wao kama walivyofanya vyama vingine. Ikumbukwe Lissu amekaa nje ya nchi kwa miaka kadhaa na alikuwa adimu machoni mwa wapiga kura. Au chama kimesahau kwenye karatasi ya kupigia kura kuna picha za wagombea? Mabango kwa watu wa marketing watakubaliana nami ni nyenzo kubwa sana kwenye kuitangaza bidhaa. Mtu asiyejua kusoma itamsaidia sana kwenye kupiga kura. Watu kama wahadzabe mngekuwa mmewarahisishia sana.

Mimi nionavyo ndani ya CHADEMA kuna ambao kwa makusudi waliamua kumhujumu Lisu kwa kutoweka mabango. Au pia watu hao wameona tu Rais Magufuli anatosha kwahiyo wamsaidie kinamna. Ombi langu kwa Rais JPM asimsahau Mh Tundu Lissu kwenye teuzi za serikali yake ijayo.
Je umeulizia gharama za kuyaweka hayo mabamgo yaani kuna gharama tu za hilo bango kwa wewe kuliangalia ama kukilining'iniza 'displaying fee '
 
Uelewa wako ni mdogo hakuna anayetaka kumhujumu Lissu ndani ya CDM ya kweli inajulikana hali ya kifedha mbaya hata Lissu alisema hilo.

Mabango hayasaidii kitu hasa siku hizi za mitandao na media nyingi. Pamoja na mabango kona zote magufuli anapiga magoti kuomba kura ni ajabu!
Mkuu acha utani,mitandao ipi hiyo unayoiongelea,ni watanzania wangapi wanao uwezo wa kununua bando ili tu kufuatilia blah blah za lissu.

Niko huku kijijini natoa huduma ya steshenari mtu kutuma tu eitha picha au kupokea picha kwa WhatsApp lazima aje kwangu ,sasa huyu mtu kwa uelewa wake kawaida atatoa wapi pesa na simu ya smart illi amskilize lissu?
 
Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni kuhusu uchaguzi huu. Hii pia imechangiwa na wengi wenu kunitumia PM kuniomba nitoe maoni yangu kuhusu mwenendo wa uchaguzi huu. Nimekubali kufanyia kazi maombi ya wengi.

Niseme kwamba kampeni hizi za mwaka huu ni za kipekee. Ziko tofauti sana. Wapiga kura wengi kwa sasa wana akili nyingi sana na hawasikilizi blah blah. Ilishazoeleka wagombea kutamka uongo ulio wazi na ahadi nyingi hewa ila kwa mwaka huu inaonekana kabla mgombea hajatamka kitu inabidi ajifikirie mara nyingi sana. Watu wanataka maelezo ya kina. Kwahiyo hakuna Chama chenye wakati mrahisi tunapoiendea tar 28 Octoba.

CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kimeonyesha kuleta changamoto kwenye uchaguzi huu hasa baada ya kupata mgombea jasiri na ambaye inaonekana wazi hakuna anachohofia. Chama hicho kina mtaji mkubwa wa kura za huruma kutoka kwa watu wanaoamini kuwa Lisu alitendewa ubaya na CCM. Bahati nyingine ya hivi karibuni ambayo inaweza kuwaongezea kura za huruma ni hiki kitendo cha NEC kumsimamisha Lisu kufanya kampeni kwa siku 7. Tukiachana na kura za huruma ni wazi CHADEMA watapata kura chache kutoka makundi mengine ya wananchi.

Kosa la kiufundi ambalo CHADEMA wamelifanya na litawagharimu kwenye sanduku la kura tar 28 ni kutobandika picha za mgombea wao kama walivyofanya vyama vingine. Ikumbukwe Lissu amekaa nje ya nchi kwa miaka kadhaa na alikuwa adimu machoni mwa wapiga kura. Au chama kimesahau kwenye karatasi ya kupigia kura kuna picha za wagombea? Mabango kwa watu wa marketing watakubaliana nami ni nyenzo kubwa sana kwenye kuitangaza bidhaa. Mtu asiyejua kusoma itamsaidia sana kwenye kupiga kura. Watu kama wahadzabe mngekuwa mmewarahisishia sana.

Mimi nionavyo ndani ya CHADEMA kuna ambao kwa makusudi waliamua kumhujumu Lisu kwa kutoweka mabango. Au pia watu hao wameona tu Rais Magufuli anatosha kwahiyo wamsaidie kinamna. Ombi langu kwa Rais JPM asimsahau Mh Tundu Lissu kwenye teuzi za serikali yake ijayo.
Tabia ya watz Ni jupika mahungu tu,

umefanya kautafiti kujua kwanini hawajabandika mabango?

Upuuzi mtupu
 
Back
Top Bottom