Uchaguzi 2020 CHADEMA kutobandika picha za Tundu Lissu ni kosa la kiufundi

Uchaguzi 2020 CHADEMA kutobandika picha za Tundu Lissu ni kosa la kiufundi

Mleta mada unataka kusema jambo zuri lakini unafiki ni kiongozi wako na unashindwa.

Hujui kuzuiliwa kwa mikutano ya hadhara na ndani, kuvukuzwa bungeni, kesi zimeelekezwa kwa chama chenye nguvu kuliko mwingine?? Kama hata bendera tu inashushwa, tangazo la mpiga kura ndio litabaki?? Hakukuwa na haja ya kutumia pesa katika jambo ambalo halina tija!

Ukitaka kusema hili, hakuna mpigakura aliyejua sura au habari ya Lissu. Atakayeacha kumpigia kura si kwa sababu atakuwa hamfahamu bali hapendi awe Rais. Period!!
 
Kwenye kura hata ya mjinga inahitajika. Kama hamtaki kura za wajinga ina maana mmekubali kushindwa.
Kwahiyo unataka kuniambia watanzania wengi ni wajinga kuliko wasio wajinga ndio maana ili chama kishinde kwenye uchaguzi lazima upate kula za hao wajinga ambao ndio wengi?
 
Hii mada inahusu Chama cha Mbowe. Usichanganye mambo
Magufuli ametuharibia nchi, wapuuzi wengi wamejipa madaraka ya kutukana wapinzani kwa ujira wa elfu saba tu.
 

Attachments

  • Lumumba Buku 7.jpg
    Lumumba Buku 7.jpg
    20.8 KB · Views: 1
Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni kuhusu uchaguzi huu. Hii pia imechangiwa na wengi wenu kunitumia PM kuniomba nitoe maoni yangu kuhusu mwenendo wa uchaguzi huu. Nimekubali kufanyia kazi maombi ya wengi.

Niseme kwamba kampeni hizi za mwaka huu ni za kipekee. Ziko tofauti sana. Wapiga kura wengi kwa sasa wana akili nyingi sana na hawasikilizi blah blah. Ilishazoeleka wagombea kutamka uongo ulio wazi na ahadi nyingi hewa ila kwa mwaka huu inaonekana kabla mgombea hajatamka kitu inabidi ajifikirie mara nyingi sana. Watu wanataka maelezo ya kina. Kwahiyo hakuna Chama chenye wakati mrahisi tunapoiendea tar 28 Octoba.

CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kimeonyesha kuleta changamoto kwenye uchaguzi huu hasa baada ya kupata mgombea jasiri na ambaye inaonekana wazi hakuna anachohofia. Chama hicho kina mtaji mkubwa wa kura za huruma kutoka kwa watu wanaoamini kuwa Lisu alitendewa ubaya na CCM. Bahati nyingine ya hivi karibuni ambayo inaweza kuwaongezea kura za huruma ni hiki kitendo cha NEC kumsimamisha Lisu kufanya kampeni kwa siku 7. Tukiachana na kura za huruma ni wazi CHADEMA watapata kura chache kutoka makundi mengine ya wananchi.

Kosa la kiufundi ambalo CHADEMA wamelifanya na litawagharimu kwenye sanduku la kura tar 28 ni kutobandika picha za mgombea wao kama walivyofanya vyama vingine. Ikumbukwe Lissu amekaa nje ya nchi kwa miaka kadhaa na alikuwa adimu machoni mwa wapiga kura. Au chama kimesahau kwenye karatasi ya kupigia kura kuna picha za wagombea? Mabango kwa watu wa marketing watakubaliana nami ni nyenzo kubwa sana kwenye kuitangaza bidhaa. Mtu asiyejua kusoma itamsaidia sana kwenye kupiga kura. Watu kama wahadzabe mngekuwa mmewarahisishia sana.

Mimi nionavyo ndani ya CHADEMA kuna ambao kwa makusudi waliamua kumhujumu Lisu kwa kutoweka mabango. Au pia watu hao wameona tu Rais Magufuli anatosha kwahiyo wamsaidie kinamna. Ombi langu kwa Rais JPM asimsahau Mh Tundu Lissu kwenye teuzi za serikali yake ijayo.
Kuweka picha ya Tundu Lissu inasaidia nini mbona watu wengi tu (including you) wanamfahamu kuwa anagombea Urais nchini Tanzania? Picha hazina impact kwa kuwa watu wanamfahamu hata asipoweka picha. Sasa aweke picha za nini? Asiyefahamika na anayetaka ajulikane uwepo wake kwa wananchi, licha ya kujinasibu kuwa ameifanyia mambo mengi nchi hii, mwacheni abandike picha kila kona. Kuweka picha sio mashindano mkuu. Kama kuweka picha tu ni ushindi, basi mgombea wa chama chenu cha CCM tayari ameshinda uchaguzi. Iambieni tume ya CCM (chini ya kada Wilson Mahela) imuapishe kuwa rais wa nchi hii.
 
Kwahiyo unataka kuniambia watanzania wengi ni wajinga kuliko wasio wajinga ndio maana ili chama kishinde kwenye uchaguzi lazima upate kula za hao wajinga ambao ndio wengi?
Ndugu yangu kwenye uchaguzi kinachohitajika ni kura za kutosha. Kwahiyo huu si muda wa kuchagua kwamba kura ni ya mwenye akili au mjinga... huoni wanasiasa wanaingia hadi vilabu vya pombe za kienyeji kusaka kura? Nikupe moyo kwamba kadiri watanzania wanavyozidi kuelimika haitachukua muda kutaka mabadiliko ya katiba kwa baadhi ya mambo ili kuondoa malalamiko.
 
Ulivyo mjinga unazania kazi ya Ruzuku ni kuendesha kampeni, CCM wanaendesha kampeni kwa 10% za ununuaji wa ndege
Ukata umesababishwa na nini? Jibu ni matumizi mabaya ya ruzuku na michango ya wanachama hasa wabunge.
 
Ngoja nimueleweshe mleta mada hapa.
Kwanza Sio kweli kuwa Lissu hana mabango au CHADEMA hawajatengeneza mabango, mabango yapo lakini yanaonekana kwa uchache kwa sababu zifuatazo:

(i)Gharama za kutengeneza mabango ni kubwa sana, kiasi ambacho Chama hakiwezi kugharamia mabango mengi kama walivyo CCM. Ikitokea CADEMA kikisaidiwa na watu/wafanyabiashara wasiotaka kujulikana wazi ili kutengeneza mabango, Chama kitaambiwa kinatumika kinatakatisha Pesa. (Kumbuka kisa cha msaidizi wa Membe kilichompata)

(ii)Kwa sasa (katika uchaguzi huu wa 2020) Kuchapisha na kubandika bango sehemu rasmi unapaswa kulipia kodi. Ukijaribu kufanya kienyeji, utaambiwa unakwepa kodi, hivyo chama kipo mtegoni. (Kumbuka kisa cha Kubenea kukamatwa akitokea Kenya).

(iii)Uchunguzi uliofanyika katika mikoa mingi ambapo mabango ya Lissu yalibandikwa, ndani ya masaa 24 tu toka yabandikwe zaidi ya 80% yalikutwa yamechanwa au kung'olewa huku ikielezwa zoezi hilo kufanywa na vijana wa CCM chini ya usimamizi wa jeshi la Polisi.

(iv)CCM imesambaza mabango ya Magufuli kila kona ya nchi (mpaka kwenye vyoo vya bar, stendi na guest house) kwa sababu wanazo means zote (pesa, serikali, mamlaka), hivyo uwepo wa mabango ya Lissu na CHADEMA itabidi yawe sambamba katika mwelekeo huo huo ili kuonekana, Otherwise mabango ya Lissu na CHADEMA hayataonekana.
Maelezo bomba.
 
Ulivyo mjinga unazania kazi ya Ruzuku ni kuendesha kampeni, CCM wanaendesha kampeni kwa 10% za ununuaji wa ndege
Wewe murusi punguza kusikiliza stori za vijiweni. Ishi kwenye uhalisia
 
Shida, mateso, njaa ya miaka 5 ni picha tosha
KWA ATAKAYE IBA KURA BORA APATE UGONJWA WA UKICHAA MILELE MAANA WATU HAWA WANATUZUNGUSHA VICHWA SANA TUTAOMBA MASAADA SOUTH KOREA (WOTE HATUWEZI KUWA WATOTO)
 
KWA ATAKAYE IBA KURA BORA APATE UGONJWA WA UKICHAA MILELE MAANA WATU HAWA WANATUZUNGUSHA VICHWA SANA TUTAOMBA MASAADA SOUTH KOREA (WOTE HATUWEZI KUWA WATOTO)
Kapige kura Hakuna kura itakayoibiwa uzuri mbinu zao za wizi Sumaye, Lowasa walishatuonyesha
 
Rais Magufuli amteue kwenye nyadhifa itakayomfaa. Lissu kazungukwa na watu wenye uwezo mdogo mno kwenye kufikiria. Uchaguzi ukiisha ajiunge CCM kwa wasomi wenzake.
akili kizibo kichwa ndoo
 
Mgombea wetu wa CCM akiwa Zanzibar anawaeleza Wazanzibar kuwa wasiondoke uwanjani hapo maana akimaliza hotuba bado Kuna show kabambe kutoka kwa wasanii na watamuona nae akicheza.... Wazenji nao viburi wakaondoka wakati anazungumza. Aisee!
bila show za wasanii ni shida sana kwa ccm
 
Back
Top Bottom