DR VRM
JF-Expert Member
- Sep 9, 2024
- 3,933
- 3,071
mbona CDM mmejibaka na kujinajisi wenyeweTumeccm na Polisiccm sasa wamebaka na kunajisi haki ya kuchagua na kuchaguliwa, uchaguzi utakuwa haramu kwani umejaa mbinu zote za kishetani

Labda pia nipanue maelezo yangu kwa vifungu:Na:Mathias Byabato
Binafsi uwa siandiki sana kuhusu mambo ya siasa. Leo nimeona nisaidie muktadha kadri ya uelewa wangu. Kwa watu wanaojua mantiki na umuhimu demokrasia katika taifa lolote wanajua hasara kadhaa zitazojitokeza iwapo itasalia hivi hivi Kwa chadema kutoshiriki uchaguzi wowote 2025 hadi 2030.
Kwa wasiojua ni kwamba jamii ya kawaida, Taifa,CCM,Serikali na Tume watapata hasara kubwa kuliko chadema yenyewe.
Twende sawa.
Chadema
Kwa chadema hasara kubwa wanayoweza kupata ni kukosa ushawishi,uongozi na kupungua nguvu iwapo tu madai yao hayatetelezwa kabisa hadi 2030. Madai makubwa ni kutokuwepo Tume huru ya Uchaguzi,uwanja sawa WA ushindani kati yao na CCM,Sheria za uchaguzi na watu wao kutopotea au kufa kutokana na michakato ya Uchaguzi.
Iwapo tu yatatekelezwa Kwa kipindi hicho chadema itapanda thamani sana. Kama Hali itasalia hivi hivi na madai yao basi chadema itakuwa imejimaliza.
Aidha Chadema itapoteza nafasi ya kushiriki katika siasa za kitaifa, hivyo kupunguza umaarufu na msaada wake kati ya wafuasi. Wengi wanaweza kuona chama kama kisichokuwa na mkakati au uwezo wa kuongoza.
Kutengwa na Mifumo ya Uongozi: Kwa kususia, chama hakitapata wabunge, madiwani, au nafasi za urais, hivyo kitapoteza fursa ya kuwa na sauti katika Bunge au mabaraza ya uongozi, na hivyo kupunguza uwezo wake wa kuleta mabadiliko.
CCM
Kwa Chama Tawala
Kukosekana kwa Ushindani wa Kisiasa: Chama tawala kitapata ushindi rahisi bila upinzani wa maana, lakini hii inaweza kusababisha ukosefu wa changamoto za kiwango cha juu, na hivyo kupunguza ubora wa sera zao na uongozi.Watajihesabu wamemaliza uchaguzi mkuu baada ya ule WA ndani. Bajeti yao ya Uchaguzi mkuu itafumuliwa sana. Watakuwa na jukumu la kuanza kusoma mbinu za kuendesha siasa Kwa kutazama hoja za vyama vingine nje ya chadema.
~Changamoto za Uhalali:~ Ushindi bila upinzani wa nguvu unaweza kutiliwa shaka kimataifa na ndani ya nchi, na kuathiri uhalali wa chama tawala kama CCM. Wanaweza kuonekana kama wamechukua mamlaka bila ridhaa ya kweli ya wananchi.
Hapatakuwepo na siasa za hoja. Kuibua hoja na kujibiwa. Kuna suala la kuibuliwa Kwa vijana wenye nguvu kisasa hapa itakuwa ngumu kuwapata. Vijana wapya wenye nguvu kisasa wanapatikana kutokana na siasa ngumu za ushindani. Mbinu za ujasusi WA kisiasa nk hazitakuwepo.Watu kama akina Katambi,Kitila Mkumbo,Kafulila,Waitara,mashinji,Wasira ,zitto,Halima mdee nk ni mazao ya kuwepo ushindani kati ya CCM na Chadema.
Itakuwa ni ngumu sana Kwa CCM kuwa na hoja Mpya za kila siku KATIKA kampeini ambazo uibuliwa na wapinzani WA kweli kwao. Wapo ACT Wazalendo,CUF nk lakini bado hawakuwa na nguvu ya mtandao kama Chadema.
Taifa
Kudhoofika kwa Demokrasia: Kukosekana kwa chama cha upinzani chenye nguvu kushiriki kutasababisha demokrasia dhaifu, kwani uchaguzi hautakuwa wa ushindani wa kweli. Hii inaweza kuleta mfumo wa karibu na chama kimoja, ambao unaweza kuathiri uhuru wa kisiasa.
Kupungua kwa Uwakilishi wa Maoni Mbalimbali: Wananchi wanaounga mkono Chadema watapoteza sauti yao katika mifumo ya utawala, na hivyo kusababisha kutokuwepo kwa uwakilishi wa maoni tofauti, ambayo ni msingi wa taifa lenye ushirikiano. Nchi yetu ni ya mfumo WA vyama vingi. Hali hii itaonesha jicho baya kimataifa.
Kwa jamii
Kutakuwa na tatizo la Uchumi kwani Mzunguko wa Fedha za Kampeni utapungua.
Kampeni za uchaguzi huchochea uchumi wa ndani kupitia matumizi ya fedha kwenye huduma kama usafiri, matangazo, mikutano, na bidhaa za kampeni. Kutoshiriki Kwa chadema kutasababisha kupungua kwa mzunguko wa fedha, na kuathiri wafanyabiashara wadogo, wauzaji wa chakula, na watoa huduma.
Pia kuna kupungua kwa Mapato ya Biashara za Ndani kwani biashara zinazotegemea kampeni, kama vile hoteli, kampuni za uchapishaji, na wauzaji wa fulana,kanga, zitapata hasara kubwa kwa sababu hakutakuwa na mahitaji makubwa ya huduma zao kwa kiwango cha kawaida.
Kwa Serikali
Kupungua kwa Imani ya Umma: Serikali inayoundwa baada ya uchaguzi usio na ushindani wa kweli inaweza kukosa imani ya umma, hasa kati ya wafuasi wa upinzani. Hii inaweza kusababisha mgawanyiko wa kijamii na kuathiri utulivu wa kisiasa.
Changamoto za Utawala wa Kimataifa: Serikali itakabiliwa na shinikizo la kimataifa kutokana na uchaguzi usioonekana kuwa huru na wa haki, na hivyo kuathiri uhusiano na wafadhili au washirika wa kimataifa.
Kwa Tume ya Uchaguzi
Kutokuwa na Uhalali: Tume ya Uchaguzi inaweza kushutumiwa kwa kushindwa kusimamia uchaguzi wa ushindani, na hivyo kupoteza uaminifu wa umma. Maswali yanaweza kujitokeza kuhusu uwezo wake wa kuendesha uchaguzi wa haki.
Kupungua kwa Maana ya Uendeshaji Uchaguzi: Bila ushiriki wa chama chenye nguvu, uchaguzi unaweza kuonekana kama wa “kawaida” badala ya tukio la kitaifa lenye maana. Hii inaweza kupunguza umuhimu wa tume na kazi yake katika kuimarisha demokrasia.
Hivyo Kwa ufupi.
Uamuzi wa chama cha upinzani chenye nguvu kama Chadema kususia au kuzuiwa kushiriki uchaguzi mkuu utaleta athari mbaya zinazoathiri wadau wote wa kisiasa na kiuchumi. Chama cha upinzani kitapoteza nguvu na ushawishi, chama tawala kitakosa changamoto za maana, taifa kitapoteza msingi wa demokrasia, uchumi utakosa mzunguko wa fedha, serikali itapoteza imani, na tume ya uchaguzi itakosa uhalali. Ili kuepuka hasara hizi, ni muhimu kwa vyama vyote kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi ili kuhakikisha ushindani wa haki na demokrasia imara.
Tukubali kupoteza?.
Mathias Byabato
Bukoba
0754527358
“Kila raia ana haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi ama moja kwa moja au kwa njia ya wawakilishi waliowachagua kwa hiari yao.”
Inampa Rais mamlaka ya kuteua Mwenyekiti wa Tume, Makamu na Wajumbe wengine wote — hali hii huondoa uhalisia wa uhuru wa tume.
"Serikali itawajibika kwa wananchi na itatoa fursa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za Serikali."
Uchaguzi si biashara ya kuuza kanga, bali ni mchakato wa kupima sera, uadilifu, na uwezo wa viongozi.
“Kila mtu anao uhuru wa kukusanyika na kushiriki katika chama chochote cha kisiasa...”
Mfumo wa vyama vingi unakuwa wa kimazoea tu iwapo:“Jamhuri ya Muungano ni ya mfumo wa vyama vingi vya siasa.”
wapiga kura waliojiandikishaKura zipi nyingi kutoka wapi? Wakati wapiga kura hawatajitokeza kwa wingi
19-1, shall never be statistically significant, hata wangeshiriki wanakuwa kama hawajashiriki tuLabda pia nipanue maelezo yangu kwa vifungu:
1. “Hasara kwa Chadema kwa kutoshiriki uchaguzi” ni hoja dhaifu – sababu ni Tume isiyo huru.
Katiba ya JMT (1977), Ibara ya 21(1):
Haki hii haiwezi kuwa halali ikiwa uchaguzi hauna usawa, mipaka imewekwa kwa upendeleo, au usalama wa wagombea haupo.
Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343:
Kwa mantiki hiyo:
Vyama vya upinzani vinapokataa kushiriki katika muktadha huo, havikiuki Katiba wala sheria, bali vinaweka msimamo wa kisiasa wa kupigania mazingira huru.
2. Demokrasia si kushiriki kwa lazima bali ni ushiriki wa haki, huru na usawa.
Katiba ya JMT, Ibara ya 8(1)(c):
Demokrasia ya kweli inahitaji:
- Uhuru wa kujieleza, kukusanyika, na kupinga bila hofu.
- Wagombea kupata fursa sawa za kutangaza sera bila kuzuiwa na vyombo vya dola.
Historia ya Afrika Mashariki (Kenya 2007, Zimbabwe 2008):
Vyama vilisusia uchaguzi au kutishia kususia, ndipo katika mazungumzo ya kisiasa (political settlements), ilizaliwa Tume huru au serikali ya mpito.
Hoja ya “mzunguko wa fedha za kampeni” ni matusi kwa akili za watu.
Sheria ya Gharama za Uchaguzi, Sura ya 6:
Inasimamia matumizi ya fedha kwenye kampeni, lakini si sababu ya msingi ya kufanya uchaguzi.
Kukataliwa kwa uchaguzi wa maigizo hakumaanishi kuvuruga uchumi, bali ni kutetea msingi wa utawala bora.
4. Kususia uchaguzi ni mbinu ya siasa safi ya kushinikiza mabadiliko.
Ibara ya 20(1) ya Katiba:
➡ Hii pia inamaanisha uhuru wa kuchagua kutoshiriki au kususia kwa malalamiko ya msingi.
Mfano wa kihistoria:
Zimbabwe (2008) – MDC ya Morgan Tsvangirai ilisusia duru ya pili ya uchaguzi baada ya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya wafuasi wao. Dunia ililazimisha majadiliano yaliyosababisha “Government of National Unity”.
5. Ushindi wa CCM bila ushindani si uthibitisho wa uimara, bali ni udhaifu wa mfumo.
Katiba Ibara ya 3(1):
Mfumo wa vyama vingi unakuwa wa kimazoea tu iwapo:
- Vyama haviruhusiwi kushindana kwa haki,
- Kimoja kinapewa rasilimali zote, na kingine kinazuiwa kiholela.
Historia ya Tanzania:
1995–2020: Uchaguzi umeendelea kuwa na dosari nyingi, huku Tume ikishindwa kusimamia haki kwa vyama vyote — lakini ni mwaka 2020 ambapo hali ilifikia kiwango cha “dola kupora uchaguzi waziwazi.”
6. Tume ya Uchaguzi haina uhalali wa kikatiba au wa kijamii katika hali ya sasa.
Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT:
Inaeleza mamlaka ya Tume, lakini haielezi uhuru wa kimuundo, wala uwakilishi wa vyama vyote.
➡ Tatizo kuu:
Hali hii ni kinyume na kanuni za Kimataifa za uchaguzi huru:
- Wajumbe wote wa Tume huteuliwa na Rais (ambaye ni mgombea).
- Wasimamizi wa uchaguzi ni Wakurugenzi walioteuliwa pia na serikali ya chama tawala.
- SADC Principles and Guidelines on Democratic Elections
- African Charter on Democracy, Elections and Governance
Hitimisho:
Kutoshiriki uchaguzi wa kidhalimu si uoga wala kukata tamaa — ni hatua ya kisiasa ya kupinga uhalali wa mfumo unaonyonya wananchi kisiasa.
Ni kutumia Katiba kwa maana yake halisi,
Ni kutumia historia kujifunza mbinu za kupigania uhuru,
Ni kushinikiza mabadiliko ya kweli, ya kudumu, kwa njia ya amani lakini thabiti.
Uchaguzi wa Tanzania ni mwenye kura nyingi Ndio anakuwa mshindi.Kura zipi nyingi kutoka wapi? Wakati wapiga kura hawatajitokeza kwa wingi
Tutashuhudia watu kusombwa na malori wakapige kurawengi hawataenda kupiga kura uchaguzi utakua na taswira nyingine
Kweli tupu...19-1, shall never be statistically significant, hata wangeshiriki wanakuwa kama hawajashiriki tu
Ndio maana halisi ya no reforms no election.19-1, shall never be statistically significant, hata wangeshiriki wanakuwa kama hawajashiriki tu
We poyoyo umeandika upupu tafuta kazi ya kufanya. Tuna vyama 19 na 18 vinashiriki uchaguzi, hao nyumbu wameamua kususa, demokrasia iko pale pale tena ni kubwa sana.Na:Mathias Byabato
Binafsi uwa siandiki sana kuhusu mambo ya siasa. Leo nimeona nisaidie muktadha kadri ya uelewa wangu. Kwa watu wanaojua mantiki na umuhimu demokrasia katika taifa lolote wanajua hasara kadhaa zitazojitokeza iwapo itasalia hivi hivi Kwa chadema kutoshiriki uchaguzi wowote 2025 hadi 2030.
Kwa wasiojua ni kwamba jamii ya kawaida, Taifa,CCM,Serikali na Tume watapata hasara kubwa kuliko chadema yenyewe.
Twende sawa.
Chadema
Kwa chadema hasara kubwa wanayoweza kupata ni kukosa ushawishi,uongozi na kupungua nguvu iwapo tu madai yao hayatetelezwa kabisa hadi 2030. Madai makubwa ni kutokuwepo Tume huru ya Uchaguzi,uwanja sawa WA ushindani kati yao na CCM,Sheria za uchaguzi na watu wao kutopotea au kufa kutokana na michakato ya Uchaguzi.
Iwapo tu yatatekelezwa Kwa kipindi hicho chadema itapanda thamani sana. Kama Hali itasalia hivi hivi na madai yao basi chadema itakuwa imejimaliza.
Aidha Chadema itapoteza nafasi ya kushiriki katika siasa za kitaifa, hivyo kupunguza umaarufu na msaada wake kati ya wafuasi. Wengi wanaweza kuona chama kama kisichokuwa na mkakati au uwezo wa kuongoza.
Kutengwa na Mifumo ya Uongozi: Kwa kususia, chama hakitapata wabunge, madiwani, au nafasi za urais, hivyo kitapoteza fursa ya kuwa na sauti katika Bunge au mabaraza ya uongozi, na hivyo kupunguza uwezo wake wa kuleta mabadiliko.
CCM
Kwa Chama Tawala
Kukosekana kwa Ushindani wa Kisiasa: Chama tawala kitapata ushindi rahisi bila upinzani wa maana, lakini hii inaweza kusababisha ukosefu wa changamoto za kiwango cha juu, na hivyo kupunguza ubora wa sera zao na uongozi.Watajihesabu wamemaliza uchaguzi mkuu baada ya ule WA ndani. Bajeti yao ya Uchaguzi mkuu itafumuliwa sana. Watakuwa na jukumu la kuanza kusoma mbinu za kuendesha siasa Kwa kutazama hoja za vyama vingine nje ya chadema.
~Changamoto za Uhalali:~ Ushindi bila upinzani wa nguvu unaweza kutiliwa shaka kimataifa na ndani ya nchi, na kuathiri uhalali wa chama tawala kama CCM. Wanaweza kuonekana kama wamechukua mamlaka bila ridhaa ya kweli ya wananchi.
Hapatakuwepo na siasa za hoja. Kuibua hoja na kujibiwa. Kuna suala la kuibuliwa Kwa vijana wenye nguvu kisasa hapa itakuwa ngumu kuwapata. Vijana wapya wenye nguvu kisasa wanapatikana kutokana na siasa ngumu za ushindani. Mbinu za ujasusi WA kisiasa nk hazitakuwepo.Watu kama akina Katambi,Kitila Mkumbo,Kafulila,Waitara,mashinji,Wasira ,zitto,Halima mdee nk ni mazao ya kuwepo ushindani kati ya CCM na Chadema.
Itakuwa ni ngumu sana Kwa CCM kuwa na hoja Mpya za kila siku KATIKA kampeini ambazo uibuliwa na wapinzani WA kweli kwao. Wapo ACT Wazalendo,CUF nk lakini bado hawakuwa na nguvu ya mtandao kama Chadema.
Taifa
Kudhoofika kwa Demokrasia: Kukosekana kwa chama cha upinzani chenye nguvu kushiriki kutasababisha demokrasia dhaifu, kwani uchaguzi hautakuwa wa ushindani wa kweli. Hii inaweza kuleta mfumo wa karibu na chama kimoja, ambao unaweza kuathiri uhuru wa kisiasa.
Kupungua kwa Uwakilishi wa Maoni Mbalimbali: Wananchi wanaounga mkono Chadema watapoteza sauti yao katika mifumo ya utawala, na hivyo kusababisha kutokuwepo kwa uwakilishi wa maoni tofauti, ambayo ni msingi wa taifa lenye ushirikiano. Nchi yetu ni ya mfumo WA vyama vingi. Hali hii itaonesha jicho baya kimataifa.
Kwa jamii
Kutakuwa na tatizo la Uchumi kwani Mzunguko wa Fedha za Kampeni utapungua.
Kampeni za uchaguzi huchochea uchumi wa ndani kupitia matumizi ya fedha kwenye huduma kama usafiri, matangazo, mikutano, na bidhaa za kampeni. Kutoshiriki Kwa chadema kutasababisha kupungua kwa mzunguko wa fedha, na kuathiri wafanyabiashara wadogo, wauzaji wa chakula, na watoa huduma.
Pia kuna kupungua kwa Mapato ya Biashara za Ndani kwani biashara zinazotegemea kampeni, kama vile hoteli, kampuni za uchapishaji, na wauzaji wa fulana,kanga, zitapata hasara kubwa kwa sababu hakutakuwa na mahitaji makubwa ya huduma zao kwa kiwango cha kawaida.
Kwa Serikali
Kupungua kwa Imani ya Umma: Serikali inayoundwa baada ya uchaguzi usio na ushindani wa kweli inaweza kukosa imani ya umma, hasa kati ya wafuasi wa upinzani. Hii inaweza kusababisha mgawanyiko wa kijamii na kuathiri utulivu wa kisiasa.
Changamoto za Utawala wa Kimataifa: Serikali itakabiliwa na shinikizo la kimataifa kutokana na uchaguzi usioonekana kuwa huru na wa haki, na hivyo kuathiri uhusiano na wafadhili au washirika wa kimataifa.
Kwa Tume ya Uchaguzi
Kutokuwa na Uhalali: Tume ya Uchaguzi inaweza kushutumiwa kwa kushindwa kusimamia uchaguzi wa ushindani, na hivyo kupoteza uaminifu wa umma. Maswali yanaweza kujitokeza kuhusu uwezo wake wa kuendesha uchaguzi wa haki.
Kupungua kwa Maana ya Uendeshaji Uchaguzi: Bila ushiriki wa chama chenye nguvu, uchaguzi unaweza kuonekana kama wa “kawaida” badala ya tukio la kitaifa lenye maana. Hii inaweza kupunguza umuhimu wa tume na kazi yake katika kuimarisha demokrasia.
Hivyo Kwa ufupi.
Uamuzi wa chama cha upinzani chenye nguvu kama Chadema kususia au kuzuiwa kushiriki uchaguzi mkuu utaleta athari mbaya zinazoathiri wadau wote wa kisiasa na kiuchumi. Chama cha upinzani kitapoteza nguvu na ushawishi, chama tawala kitakosa changamoto za maana, taifa kitapoteza msingi wa demokrasia, uchumi utakosa mzunguko wa fedha, serikali itapoteza imani, na tume ya uchaguzi itakosa uhalali. Ili kuepuka hasara hizi, ni muhimu kwa vyama vyote kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi ili kuhakikisha ushindani wa haki na demokrasia imara.
Tukubali kupoteza?.
Mathias Byabato
Bukoba
0754527358
We wachangie hao nyumbu hakuna atakayekuomba mchango wa hela ya kufanyia kampeni.Na mtashuhudia uchaguzi wa baridi kuliko barafu.
Sioni hata sababu ya kupoteza pesa za kampeni kwa mtu ambae yuko serious na nchi yake.
Na:Mathias Byabato

Wengi wapi?? Chadema wapiga kura hawanaga zaidi ya wafanya propaganda mitandaoniwengi hawataenda kupiga kura uchaguzi utakua na taswira nyingine
We ndio hautajitokeza, kimsingi wengi wenu mnaoandika humu si wapiga kura, hamna ht kadi ya kupigia kura. Watanzania wazalendo halisi wazalishaji wa nchi hii watapiga kura.Kura zipi nyingi kutoka wapi? Wakati wapiga kura hawatajitokeza kwa wingi
2. Demokrasia si “kushiriki tu”, bali ni mazingira ya haki.
Hoja yako inashabikia mfumo wa “ushiriki ili kuonekana” bila kuuliza: tuna ushindani wa haki kweli? Kama Tume inateuliwa na Rais wa chama tawala, sheria za uchaguzi zimejaa upendeleo, polisi na vyombo vya dola vinageuka maadui wa wapinzani — unategemea nini kwa usawa? Unapozungumzia “hasara ya kutoshiriki,” ni bora ujiulize: ushiriki wa aina gani? Ushiriki wa kiini macho?
Asante sana kwa ushahidi huu...
Utaenda kupoteza muda kwenye chaguzi za maigizo?? October ni mbali lkn wahusika wana matokeo tayari.kwa hiyo majority ni voters wa CDM??
Ubarikiwe wewe na uzao wako.Mathias Byabato kwa mawazo yako, ninahitaji kukujibu kwa msisitizo na kwa haki—si kwa ushabiki, bali kwa ukweli wa mambo.
1. Hoja yako ina upungufu mkubwa wa msingi wa kisheria na kisiasa.
Unazungumzia "hasara" kwa Chadema kwa kutoshiriki uchaguzi bila hata kutafakari kwa kina sababu ya msingi inayowafanya wasusie: ukosefu wa Tume huru ya uchaguzi. Hilo ni suala la msingi la kikatiba, si hoja ya kisiasa ya kawaida. Katika mazingira ambayo uchaguzi hauna usawa, kuendelea kushiriki ni kulibariki udhalimu. Kushiriki katika mazingira ya udanganyifu ni sawa na kuhalalisha uchaguzi wa kipuuzi.
2. Demokrasia si “kushiriki tu”, bali ni mazingira ya haki.
Hoja yako inashabikia mfumo wa “ushiriki ili kuonekana” bila kuuliza: tuna ushindani wa haki kweli? Kama Tume inateuliwa na Rais wa chama tawala, sheria za uchaguzi zimejaa upendeleo, polisi na vyombo vya dola vinageuka maadui wa wapinzani — unategemea nini kwa usawa? Unapozungumzia “hasara ya kutoshiriki,” ni bora ujiulize: ushiriki wa aina gani? Ushiriki wa kiini macho?
3. Hoja ya uchumi wa kampeni ni dhaifu na ya aibu kwa taifa.
Unasema kutoshiriki kwa Chadema kutapunguza mzunguko wa fedha kwa wauzaji wa kanga na chipsi. Hivi kweli tuko tayari kuuza demokrasia kwa sababu ya mzunguko wa fedha wa kampeni? Je, si aibu kwa taifa kuridhika na uchaguzi wa kisanii eti kwa sababu utawanufaisha wachuuzi wa fulana? Huu ni mtazamo wa kibiashara kwenye jambo la msingi kama uhalali wa utawala.
4. Kujitoa kwa Chadema ni hatua ya kisiasa ya kimkakati, si udhaifu.
Kujitoa kwenye uchaguzi wa kipuuzi ni siasa safi ya msimamo, si kushindwa kisiasa. Ndiyo maana hata kimataifa, wasimamizi huru wa uchaguzi hupima uhalali kwa kuangalia mazingira ya kabla ya uchaguzi, si idadi ya vyama vilivyoshiriki tu.
5. CCM si chama imara kwa kukosa wapinzani, ni dhaifu kwa kuua ushindani.
Unaposema CCM itakosa hoja, changamoto, na vijana wenye hoja — hiyo si hoja ya Chadema kujilaumu, ni aibu ya CCM yenyewe. Chama kinachoshindwa kujenga hoja bila kushindana, si chama tawala, ni chama legelege.
Kwa hiyo Mathias, tukubaliane:
Kama kweli tunataka uchaguzi huru, mahitaji ya msingi ni Tume huru, sheria ya haki, uwanja sawa wa ushindani, na usalama wa wagombea wote. Bila hayo, siyo demokrasia — ni maigizo.
Na kama kutoshiriki uchaguzi wa kipuuzi kutasaidia kufumbua macho ya Watanzania, basi ni hatua ya kishujaa, si kushindwa.
“Demokrasia si kura tu — ni mazingira ya usawa, heshima ya sheria, na uhuru wa kweli wa kushiriki.”
– MwanaDemokrasia wa kweli
Tukatae maigizo. Tukubali mabadiliko ya kweli.